Kuna dawa mpya za kisukari zimetoka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna dawa mpya za kisukari zimetoka?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mbwambo, Mar 29, 2012.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ninasumbuliwa na KISUKARI cha juu nina mwaka sasa.
  Nimekuwa nashindwa kutengeneza hasa chakula ninachotakiwa kula lakini ninajitahidi sasa maana nimekuwa nachoma insulin mara kwa mara.
  Je ni kweli kuna dawa mpya ambazo inasemekana zinasaidia sana kushusha sukari?

  Naomba msaada wenu
  :thinking:
   
 2. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  du pole sana.mimi sijawahi sikia. kisukari hakitibiki unabidi ufauate maagizo ya dk wako. lazima pia ujue kisukari kimesababishwa na nini. kama wengu lako haliwezi toa insulini(langer-hans cells zimekufa) hiyo huitwa type one diabetics na inabidi uchome insulin maisha yako yote. kama ni failure ya cell sensitivity to insulin basi waweza kuwa unafanya mazoezi huku unatumia dawa iitwayo metafomine. lakini lazima ufuate masharti yote upewayo n daktari.
   
 3. k

  kamili JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hakuna dawa mpya ya kisukari iliyodunduliwa otherwise tungeisikia kutoka vyombo tulivyovipa dhamana ya kuangalia afya zetu na kutupatia habari za ugunduzi mpya. unless kama anatengenezwa babu mwingine kama wa Loliondo.
   
 4. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Asante kwa kujibu Kamil
  Nitaendelea na hizi hizi ninazotumia. Usinitajie LOLIONDO Mungu alinusuru maisha yangu ningekufa huko LOLIONDO.
  Mungu aliruhusu nirudi salama na niliporudi tu siku hiyo hiyo nilitapika ajabu na hatimaye nililazwa kwa week 2 nikifanyiwa uchunguzi wa kila kitu nakuchomwa insulin maana sukari ilikuwa juu ajabu.
  Mungu amhurumie huyu Babu na amsamehe bure
   
 5. T

  Tsidekenu Senior Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  google 'neptunus international' then nipm nikusaidie
   
 6. K

  Kimla JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 8, 2008
  Messages: 1,508
  Likes Received: 1,392
  Trophy Points: 280
  waone kampuni ya tiens ya kichina,hawa wanatakuelekeza cha kufanya
   
 7. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  mkuu pole sana, kisukari huwa lengo la dawa na diet ni kushusha sukari kuwa karibu na level ya kawaida, pamoja na wewe kutumia dawa, pia swala la kuangalia nini unakula, kwa kiasi gani na kwa wakati gani ni la uhimu pia, sijajua upo mkoa gani ila nina hakika kila hospitali ina kliniki maalum ya sukari na hapo pamoja na kupata ushauri wa dakatari kuhusiana na dawa pia wapo wauguzi wanatoa elimu ya chakula, na namna ya kujikinga na kupata vidonda, n.k.
   
 8. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Mi nilidhani ni UKIMWI tu ndo hautibiki,kumbe hata kisukari hakitibiki!!!, hivyo utaendelea kuchomwa insulini kwa miaka yote iliyobaki???. ''Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji,hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni MAGONJWA!!!, hauumwi, una KIU, usiitibu kiu kwa madawa - dr.Batmanghelidj''.

  Hii ndiyo sababu magonjwa mengi kama siyo yote hayatibiki mahospitalini, kwakuwa mahospitalini wanatibu ishara za ugonjwa (Upungufu wa maji mwilini) na siyo ugonjwa wenyewe na hiyo ndiyo sababu madawa karibu yote hutoa nafuu tu na siyo kuukomesha ugonjwa usijirudie tena.

  Kwanini mwili unapungukiwa maji?, Ni kwa sababu tunasubiri KIU ndipo tunakunywa maji!!!. KISUKARI kinatibika tu kirahisi kwa kubadili mazoea yako ya unywaji maji na utasahau habari hizo. Kumbuka maji ni UHAI.

  Bonyeza link hii kisukari | maajabu ya maji ukajifunze namna KISUKARI kilivyo ni ishara za mwili kupungukiwa maji utajifunza pia katika tovuti hiyo namna ya kuyatumia maji kujitibu na kujikinga na magonjwa mengi mengi yanayomkabili binadamu.
   
 9. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nikumbushe ntakwambia kesho muda saa hizi umekwisha.
   
 10. B

  Bichau Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kuugua,
  Cha msingi katika maradhi haya, fuatilia sana aina ya vyakula unavyotakiwa kula pamoja na matunda stahili, pia waweza tumia mafuta ya ubuyu yanapatikana kama upo Dar ,kariakoo maeneo ya stendi ya Tegeta - Mwenge Lita Tzs 60,000/= na kwa Dodoma lita ni Tzs 40,000/= pamoja na kurekebisha kiwango cha sukari mwilini, pia yanapunguza uzito uliozidi na yana vitamin A.B,C na E. Hayachemshwi/yaani hunywewa mabichi, kwa mtu mzima kunywa vijiko vya chakula 2 mara mbili kwa siku muda wa 45 days, na kwa watoto kijiko kidogo cha chai kwa siku mara 2 kwa 14 days. Ila pia usiache kufanya mazoezi tembea mwendo wa haraka kwa muda wa saa nzima mara 3 kwa wiki inatosha.
  Muumba ataleta heri zake.
   
 11. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.

  Ingredients:
  1 – Unga wa ngano 100 gm
  2 – Gundi (umefanan na ubani wa kiarabu lakini hauna harufu) 100 gm
  3 - Shaair 100 gm
  4 - Habba Soda 100 gm


  Namna ya kutengeneza
  Chemsha hivyo vitu juu katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika 10. Zima moto na wacha ipowe. Ikisha kupowa chuja na utie katika chupa.

  Matumizi
  Kunywa kikombe kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula chochote kwa muda wa siku 7.

  Wiki ya pili kunywa siku moja na uwache siku moja.

  Insha-Allah baada hizi wiki mbili utapona na utaweza kula chakula kama dasturi. ukisha maliza kutumia nipe Feedback.

  chanzo.
  https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/180570-dawa-ya-ugonjwa-wa-kisukari.html#post2620471
   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kikombe kina ujazo gani?
   
 13. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nifikiriavyo mimi Vikombe 5 vya maji sawasawa na chupa 2 za soda ya Cocacola maji yake itakuwa hicho ndio kipimo chenyewe. Ukisha chemsha chuja hiyo dawa uweke kwenye chupa ya Orange uwe unakunywa kila siku kwenye kipimo cha kikombe cha kunywa kahawa au kikombe kidogo cha chai.
   
Loading...