Kuna dalili moja tu E. Lowassa kuhamia Upinzani

acha urongo weye, suala la ukristo na usilamu linatoka wapi - wanachotaka watanzania ni mabadiliko ya uongozi wa taifa letu.
 
Lowassa hana mbadala watake wasitake iwe ccm au ukawa au chama kinachoitwa bua lazima atinge magogoni

Huna Akili nn watu wameishasema hatukubali akili ndogo itawale akili kubwa. Wewe miaka 50 ya Uhuru bado unazungumza Lowassa , mtu kachoka kwani watu wenye akili wamekufa wote mpaka awe ni bwana mamvi tu . shame on you watz
 
Huyu jamaa hawezi nguvu yake ni ccm; mtandao wa watu wenye madaraka wasio wajibika kwa yeyote ambao kazi yao ni kuigeuza serikali ya Tanzania sehemu ya kutajirikia. Mtu kama huyu akitoka ccm amekwisha. Bila mtandao wa wenye madaraka nyuma yake, huyu ni simba wa kuchora.
 
Mtu anayetishia kuhamia upinzani ili kuwalazimisha ninyi CCM kumteua kuwa mgombea wenu wa Urais, huyu hawafai, ni wa kutupa kuleeeee! Mtu wa jinsi hii siyo mwanachama mwaminifu, atawezaje kuwa pia Mwenyekiti wa Chama chenu???? Huyu ni msakatonge!!!!


kweli mkuu,pia aliwatukana wanachama waccm kusema wasiomtaka waondoke bila kujua idadi yao na kuwambia waende wapi,kwa hali ilivyo lazima waende ukawa je anajenga chama ua anakibomoa, na je wakati wa kuomba kupitishwa atawaomba haohao ua ?jamaa matabaka sana maana anaekusema vibaya leo kesho anakusema vizuri baada ya kusahihisha lile linalomkera.
 



Si alisema wasiomtaka ccm waondoke kisa analazimisha kupendwa,ubabe wa kijinga,angelijua hilo na akataka kupendwa angebaki msafi, ataondoka yeye na ccm itashinda urais jiandaeni ukawa kupokea huo mzigo mkafe nao.
 

Ni ujinga kuamini eti upinzani utaenda ikulu mwaka huu, ni ujinga sababu mfumo wa katiba yetu hauruhusu mgombea wa upinzani kushinda hata kama atapata 90%

Lowassa anaweza kuupata urais kupitia ccm pekee,

Maalim Seif tangu 1995 anashinda Zanzibar ila mfumo wa uchaguzi na katiba yetu hauruhusu yeye kutangazwa, Lowassa akitoka CCM hali ya kuwa anajua hili vyema, atakuwa anamatatizo makubwa kuliko Mrema

upinzani tunahitaji viti vingi vya ubunge bungeni ili kuweka mkazo itungwe katiba mpya, katiba itakayoleta usawa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa, upinzani inatubidi tushinde madiwani wengi tuweze kuunda halmashauri za miji na majiji tusimamie Sera tuwaletee wananchi maendeleo

UKAWA wanaenda kuleta changamoto ila ushindi urais sio 2015.
 
Si alisema wasiomtaka ccm waondoke kisa analazimisha kupendwa,ubabe wa kijinga,angelijua hilo na akataka kupendwa angebaki msafi, ataondoka yeye na ccm itashinda urais jiandaeni ukawa kupokea huo mzigo mkafe nao.

UKAWA hakuna nafasi ya huyu aliyekusanya kila aliyechafuka , narudia tena , hana nafasi .
 

mkuu ulichokisema ndio uhalisia wenyew cha msingi ccm wateuwe mtu makin ingawa sina uhakika kama atakuwa makin kihivyo
 
mwaka huu haufanani na miaka mingine , UKAWA itashinda na itachukua madaraka ya nchi , Tanganyika na Zanzibar , wakati wa kutishana umekwisha , vinginevyo mkae tayari kwa hatari , bali hakuna fisadi atakayehifadhiwa na UKAWA .
 
Hatutafuta Raisi wa Kanisa au Msikiti!

Ikulu ni kazi tu siyo sehemu ya Ibada.Tunataka mtu msafi na asiye fisadi na anaytetamka waziwazi na kwa vitendo kuwa Ufisadi kwangu mwiko.

Jamani udini Wa nini Na sisi tusioamini kwenye dini
tumchague nani?!!!??
 
mwaka huu haufanani na miaka mingine , UKAWA itashinda na itachukua madaraka ya nchi , Tanganyika na Zanzibar , wakati wa kutishana umekwisha , vinginevyo mkae tayari kwa hatari , bali hakuna fisadi atakayehifadhiwa na UKAWA .

Sijui ndugu siasa umezianza lini, ila inawezekana ulizianza tangu enzi za Nyerere ila hujasoma nyakati vyema,

UKAWA achilia mbali Muungano, hata Zanzibar Maalim Seif anaenda kupata wakati mgumu kuliko wakati wowote!

Katiba ya Zanzibar iliyompa Maalim Seif umakamu, ndiyo hiyohiyo inaenda kumnyang'anya seif umakamu na kumpa Hamad Rashid, ila ataumia sana maalim Seif kwa maana katiba inaruhusu hata atakayepata 5% ya kura ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na chama kinachoongoza,

Hii inamaana gani? ikitokea ADC na inaweza kutokea maana inafadhiliwa na CCM, ADC "Watapewa viti kadhaa na CCM wakishirikiana na ZEC na ADC kwenye majimbo 49 ya Zanzibar we kwa fikra zako itapata mgao wa majimbo mangapi kama inapata support ya CCM na ZEC?

wakiwazidi CUF jimbo hata moja, Hamad Rashid atatangazwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Maalim seif atakosa nafasi kwenye serikali labda awe waziri!

CCM imejipanga. mwenye macho haambiwi tazama
 
Mkuu ulikuwa umenena vema,lakini umechanganya
kile kitu Gwajima anaita ''kula maharage sijui ya nini?''
Suala la university na uwezo wa kuchambua siasa ni vitu viwili
tofauti,simahanishi wale wa vitivo vingine namaanisha
wanaoitwa nguli tena waalimu wa siasa nitoe mfano wa wa Profesor yule wa kuhindi
pamoja na Dokta Bona bana,hawa ni walimu wa chuo kikuu,je uliona walivyoharibu
mchakato wa katiba? hawa wamewafanya watu wengi kuhamini
kuwa hata kama mtu ni msomi hafurukuti mbele ya njaa,tena afadhali asiye
soma ''has nothing to loose''.

Hili limepelekea vijana wa vijiweni kujiwekea utaratibu wao
wanaouamini kwamba utawaletea mabadiliko,kuliko kuendeshwa na njaa
za wanaojiita wasomi huku wakipelekeshwa na maslahi binafsi.

Nikuombe kama unajiamini kuwa unajua siasa za chuo kikuu
jitoe upite vijiweni ili utoe elimu,wakupime unachokisema
kama ni chema watakusikiliza kama kuna unazi watakutosa
maana elimu ya siasa imejaa mitaani kupitia TV
kwa kutumia watu makini kama akina Tundu LIssu.

Binafsi namtakia kila la Kheri EL
CDM,UKAWA na wapenda mabadiliko wote.
 

Kwasasa tumia zaidi jina la ukawa, usitaje chama, maana tuko katika umoja huo uliotukuka.
 

IVI HUWEZI KUWEUKA UKITAPATAPA KWA MFURULIZO MDA MREFU?? Uyu keshaweuka
 
IVI HUWEZI KUWEUKA UKITAPATAPA KWA MFURULIZO MDA MREFU?? Uyu keshaweuka

Wewe ndiye umewehuka, hapa ni uwanja great thinker nimejaribu kufafanua kwa hoja, usijifariji bila kujua unapitaje?

ifike pahala wananchi mfikirie pande zote, kuna njia mbili tu za upinzani kuingia ikulu, moja ni kupitia tume huru ya uchaguzi na kupitia vita

hii ya kwanza nimeielezea inabidi tupate viti vingi Bungeni ili tuweze kuibadili katiba iwe na tume huru ya uchaguzi

hiyo ya pili, tusiombe itokee, ikitokea tutarudi nyuma sana, na bado watanzania hawako tayari kwa njia hiyo, Watanzania ni waoga! Bhaas!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…