Kuna anayeweza kunielewesha kuhusu IMF, World Bank &Co.?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hizi Taasisi za fedha Duniani nikisoma malengo yao ni kwamba ziko kwa ajili ya kusaidia Nchi masikini kama Tanzania yetu kujikwamua na kupunguza Umaskini, lkn jambo ambalo silielewi ni kwa nini Sera zao haziendani na upambanaji dhidi ya Umaskini?

Nitatoa mfano, sasa hivi moja kati ya Taasisi kubwa ya fedha Duniani, IMF inaitaka nchi yetu kuruhusu/kulazimisha Kampuni yetu ya Tanesco kupandisha bei ya umeme kama moja ya masharti ya sisi kuendelea kupata Mikopo, sasa mbona hii inapingana na lengo la kupunguza Umaskini?

Kama bei ya umeme ikipanda, Je Umaskini utapungua au utaongezeka? Kuna anayeweza kunielewesha hapa hii paradox?
 
inadawa Tanesco wanadaiwa madeni kiasi kikubwa sana, so njia rahisi ya kulipa madeni hayo ni kupandisha gharama ya umeme ili serikali isikope tena kwa ajili ya hilo deni...anyway walitoa option hiyo inaweza ikawa sahihi au sio sahihi maana uchumi hauna solution straightfoward
 
IMF Haina lengo la kutokomoza umaskini na inakopesha nchi kwa Riba na pindi nchi inaposhindwa kulipa basi inatoa masharti kama kupandisha bei au kujenga kambi ya jeshi lao (US)ndani ya nchi.
 
Hii mizizi ya unyonyaji wala haikuanzishwa kuwasaidieni maskini, iwe WB ama IMF hakuna taasisi iliyopo kwa ajiri ya kuwakomboa maskini. Fatilia vizuri na uchambue kwa makini
 
Back
Top Bottom