Kuna anayefahamu Pesa Heshima Mjini wanafanya nini?

Mayor Slum

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
751
1,121
Habari za leo wana JamiiForums

Awali ya yote naamini kila mtu anaendelea na majukumu yake kama kawaida pia kuwa mwangalifu na kujikinga na ugonjwa wa Corona

Naomba nisiwachoshe leo nilikuwa napenda mnieleweshe au kama kuna watu wameshashiriki semina ya Pesa Heshima Mjini ambapo mpaka sasa wanapost magari wadada wame vaa pamba , pesa na vitu vya kuvutiavutia kwenye account ya instagram pia hii account inawafasi wengi sana .

Sasa leo nilikuwa naomba kama kuna watu kweli waliowahi kushiriki kwenye hizi semina nakutengeneza elfu 50 kila siku

Halafu wanasema ukijiunga kwa mtaji wa 396000 na utakuwa unatengeneza elfu 50 kila siku.Je ni kweli? Au utapeli?
Je kuna mtu yeyote ameshajiunga na hawa watu? Kama yupo naomba aeleze jinsi wanavyo fanya hili swala na ameshafanyikiwa au ni utapeli tu?

Kwa wale wote mnao fahamu kuhusu hili swala naombeni mtuambie kama ni ukweli mtu atatengeneza pesa au ni mambo ya oilflame , qnet ,foreverliving

Naamini nitapata majibu JamiiForums ni uwanja mkubwa sana na unawatu wengi na ni waelewa pia wa haya itasaidia na wengine kujua ukweli kuhusu ili swala

Nawasilisha.
Screenshot_20200326-104859.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwajui hao jamaa wala siwajibii. Ila mkuu tukumbushane tu kuwa kwa huo mtaji wa laki nne kasoro (396,000) kutengeneza faida ya 50,000 daily na consistently ni sawa na kiinimacho. Ilikuwa kukumbushana tu wakati tunawasubiri mashahidi
 
Naona hakuna shuhuda hebu ingia usisahau kuja kutupa mrejesho tu Watanzania sote ni ndugu 😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom