Hali hii utokea. Nilishawahi kupoteza kwa muda mrefu contacts za rafiki yangu ambaye nilikuwa naye sekondari; Ilikuwa mtihani kwangu jinsi ya kumpata japokuwa sikuwa na jambo lolote la maana kwake. Bahati nzuri nili bahatika kupata mawasiliano ya huyu rafiki yangu baada ya simu za mkononi kuanzishwa hapa nchini. Hii ilikuwa baada ya miaka 18 tangu tulipoonana kwa mara ya mwisho. Baada ya kupata namba ya simu ya huyu bwana kupitia kwa dada yake, siku moja nilijaribu kumpigia. Response niliyopata toka kwake hadi leo ni siri yangu! Sikuwahi kumpigia tena wala kumtafuta. Nilikoma kutafuta marafiki zangu wa zamani.