Kwa wale wafatialaji wa maswala ya siasa nchi wanaweza kujiuliza maswali. siku mbili kabla ya Kujiudhuru Ibrahim Lipumba gazeti la ccm uhuru ndio lilikuwa la kwanza kuripoti kujiudhuru kwa bwana Lipumba, na baada ya Lipumba kujiudhuru ilionekana wazi kwa wana ccm wa kada mbalimbali kumtetea na kumsifia sana kwamba kafanya vizuri, hata gazeti la chama uhuru lilimsifia sana.Bila kupepesa macho wana ccm walidhani kuwa kujiudhuru kwa Lipumba kungedhoofisha sana Cuf na harakati za Ukawa.
Hata hivyo Cuf ilibaki imara hasa ikishirikiana na vyama vilivyounda ukawa hata kuibuka na viti takribani 10 vya wabunge wa kuchaguliwa Tanzania Bara hii ikiwa ni mara ya kwanza Cuf kupata wabunge wengi tangu ilipoanzishwa kwa upande wa Bara.
Pasipo kutarajia Lipumba huyu aliyekiasi chama wakati wa uchaguzi amejitokeza hadharani kutengua kujiudhuru kwake na kuomba kurudi kwenye nafasi yake, jambo ambalo halina weledi au hekima yoyote kiuongozi.
Sasa kwa wale wafatiliaji wa maswala ya siasa watagundua kuna agenda ya siri iliyobebwa na Lipumba wakishirikiana na hao walio nyuma yake kutaka kuisambaratisha Cuf, na iwapo Lipumba atafanikiwa kurudi kwenye nafasi aliyoiacha agenda yake kubwa itakuwa kuiondoa Cuf kwenye UKAWA.
Lakini ebu tuangalie kwa makini kama kweli Lipumba ni kiongozi wa kusifiwa kuwa ameisaidia sana Cuf, je ktk kipindi cha uongozi wake Cuf imewahi kupata wabunge wangapi wa kuchaguliwa bara? Hivi Cuf ilikuwa na nguvu kweli huku bara au ilitegemea nguvu ya visiwani?
Leo walioko nyuma ya Lipumba wameanza kuingiza fitina ya Ubara na Uzanzibar, wana Cuf mwacheni Lipumba aende kupewa cheo huko anakopata msukumo kuna agenda ya siri kati ya ccm na Lipumba?