Kumwambia mchepuko wako kama una mke/mume

Jan 15, 2017
7
3
Hili linatuhusu jinsia zote.

Inawezekana umeshawahi kuchepuka au la. Lakini swali la msingi ni hili, kuna umuhimu wowote wa kumwambia mchepuko kama una mume au mke? Je ukimwambia madhara yake ni yapi na usipomwambia madhara yake ni yapi? Msije kusema nachekelea kuchepuka, but we live the reality.

Nasema hivi kwa sababu kuna rafiki yangu juzi kati yamemkuta. Alikuwa na kamchepuko kake, mimi sikujua ilikuwaje, but baada ya mambo yake kubuma akanishirikisha nimshauri la kufanya nikashindwa kabisa. Hakuwahi kumwambia mchepuko wake kama ana mke, sasa huyo mchepuko akawa anambana jamaa kweli kweli. Akawa anakagua simu ya jamaa kwa usiri wa hali ya juu bila jamaa kujua. Akanasa namba za mke wa jamaa. Na siku moja akampigia simu na kumwaga ugali na mboga kwa pamoja. Ninavyoongea jamaa ndoa imeshavurugika.

Ni hayo tu kwa leo, hodi jukwaani
 
Kuna watu wanajiona malaika ila maisha tunayoishi kila mtu anajua yake. Most people wana michepuko amini usiamini. Ni wachache waaminifu kwenye ndoa zao.
 
mchepuko unatakiwa kuabiwa ukweli.mke unamficha.hapo ndio burudani ya kuchepuka utaiona.
maana hata mke akikukagua na kumpigia mchepuko,mchepuko unampooza kuwa na rafiki wa kawaida wa kazini au kibiashara.hapo inakuwa burudani
Kumbe kuchepuka ni burudani

Mweh mweh mweh
 
Unadhindwaje kumwambia mchepuko kuwa una mke, basi humheshimu huyo mke au mme. Mchepuko ni ziada akikataa mwache unaishi maisha magumu kupita kiasi mwambie na aheshimu.
 
Back
Top Bottom