Kumwalika Ndesamburo kwamponza mchungaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumwalika Ndesamburo kwamponza mchungaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Nov 26, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limemshikilia kwa saa kadhaa mchungaji wa Kanisa la Agape kituo cha Moshi, David Mushi, kwa kilichodaiwa kuendesha mkutano wa wa injili ambao una itikadi za kisiasa.

  Mchungaji huyo alikamatwa muda mfupi baada ya Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, kumaliza kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo katika viwanja vya Mashujaa juzi ambapo Kamanda wa Polisi Wilaya ya Moshi, Silvanus Rukaga, alifika na kumkamata.


  Inadaiwa na waumini hao kuwa, katika ufunguzi huo walimualika Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, ambaye alitoa udhuru na kumwagiza mwakilishi wake ambaye pia hakufika ndipo walipoamua kumualika Ndesamburo, ambaye alikubali mwaliko wao.


  Taarifa za ndani zinabainisha kuwa katika mahubiri yake, Mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha Agape, Venon Fernandus, alipinga vikali kuwa mkutano wao ulikuwa wa kisiasa na kusema kuwa maudhui ya mkutano huo ni kuliombea Taifa.


  Mmoja kati ya Muumini ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, aliliambia NIPASHE kuwa baada ya Ndesamburo kuufungua, walishangaa kuona gari la Rukaga kufika viwanjani hapo na kumchukua mchungaji wao na kuondoka naye.


  Alisema mara baada ya kuondoka naye zililetwa taarifa kuwa mchungaji huyo, David Mushi, anahojiwa kutokana na kuendesha mkutano wenye maudhui ya kisiasa tofauti na kibali walichopatiwa, jambo ambalo walitakiwa kupeleka ushahidi.


  Baada ya mchungaji huyo kuhojiwa, alitakiwa kuwasilisha mkanda wa video wenye mahubiri yake pamoja na hotuba ya mbuge huyo
  ili waweze kuutazama jambo ambalo walifanya.


  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Absolum Mwakyoma alipofuatwa na kuulizwa kuhusu jambo hilo hakupatikana kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa nje ya ofisi kikazi na alipopigiwa simu yake ya mkononi, alisema hana taarifa hizo na kama jambo hilo lipo ataletewa na atatoa taarifa.

  CHANZO: NIPASHE


   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Angealikwa Lowasa aaah wangeufyata mkia kabisa
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mapolisi ya Tanzania yanaishi kwa kuweweseka utadhani wana majini....Kila mkutano ukiitishwa wako mimacho juu kudhani ni siasa tu. Hata kama ndio utulivu haupatikani hivyo....Pssssssuuuuuuuuuuuu!!!
   
 4. V

  Vitalino mlelwa Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ivi mbona mh. Lowasa amealikwa sehemu mbalimbali makanisani na akathubutu kutoa mtazamo wake kuhusu tanzania nakutokea vita mbona mapadre hawakukamata.
   
 5. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,674
  Likes Received: 17,731
  Trophy Points: 280
  mapolisi mafisi
   
 6. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,669
  Likes Received: 2,199
  Trophy Points: 280
  Hui indoo Tz , polis wote ni WA Chama cha magamba !Sijui lini tutapata polis WA taifa?
  Mungu okoa tz
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  huyo atakuwa ametumwa na na RC ama DC wa Moshi. Na kwasababu Polisi wetu wengi hawatumii akili akakurupuka kwenda kumkamata huyo mchungaji.
   
 8. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Polici ccm pumbavu kabisa, sasa si wende mkamata wote akina dr malasusa, mokiwa nk
   
 9. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Hapa ndo napoquery credibility ya awa askari wetu, tatizo lao wanafanya kazi kwa maelekezo ya ccm magamba.wameruhusu mkutano huo wakati kila mara raia wengine wakiomba kufanya mikutano yao wanaambiwa kuna tishio la al shahabab, mara taharifa za kiintelijensia zinaashiria hatari/ vurugu, ril hii nchi yetu inaudhi sana, au alshahaab wana bifu na chadema, au wanaharakati, kwelitutafika tuendako, ril inasikitisha sana
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hawajui kuwa ndo wanazidi kupandikiza chuki baina ya serikali na raia.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  polisi wa tanzania ni mapunguwani kuanzia igp wao
   
 12. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Acha kujifanya kipofu wewe,huoni hapo tatizo ni kualikwa kwa mb ndesamburo ambaye ni chadema na lowassa ni ccm tena gamba unategemea ni askari gani atakwenda kuvuruga mkutano wa lowassa wakati polisi siem nao ni gamba?!otherwise una chuki binafsi na mapadri
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,066
  Trophy Points: 280
  Kweli Polisi hamnazo
   
 14. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  maneno wanayotoa mashehe mikutatoni mnayajua??? hayana madhara..??? hahahahahahahaa kweli tz hakuna udini
   
 15. v

  valid statement JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Inamaana hamjui viongozi wote wa polisi ni vibaraka wa ccm?
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mipolisi ya kwetu inafanya kazi za siasa na yenewe ndiyo inaongoza kwa siasa na inatumia masaburi kufikiri na kuamua F**K you POLISI WOTE
   
 17. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Jamani,mtamfanya EL awe dili,na kuijaza schedule yake kwa kumuomba ahudhurie harambee,uzinduzi,mgeni rasmi,ili kuepuka kusakamwa na Polisi! Na kwa mtazamo wangu, NEC iliyoisha,ni kama imeshamsafisha EL. Sasa tutashuhudia watu mbalimbali wakijigonga kwake,kwa kumwona kama Rais mtarajiwa!
   
 18. S

  Sambega Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  POLICCM kazini!
   
Loading...