kumuadhibu mtoto

kumuadhibu mtoto

Kiteitei

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2009
Posts
1,600
Reaction score
1,575
Wadau naombeni ushauri,binti darasa la tatu kaenda shuleni na viatu ambavyo mwalimu anadai havitakiwi shuleni,mwalimu amemchapa sana tuu kwa.sababu hiyo, hivi hili kosa mtoto alistahili adhabu hii?shule wana.diary ambayo walimu wanafanya mawasiliano yote na wazazi kupitia humo,halijafanyika zaidi ya kumshushia kibano,hii ni sawa?!?!
 
Sio sawa.
Kama ni mara ya kwanza anatakiwa kuonywa kwanza aache hio tabia lakin kama ikiwa ni tabia endelevu anatakiwa kuadhibiwa.
Tatizo waalimu wa siku hizi wanamalizia hasira za familia na matatizo yao kwa wanafunzi.
 
Acha kumdekeza mwanao,
Wewe kama unamdekeza, akija shule na viatu visivyopaswa, sisi kama walimu hatuna budi kumshushia kipigo.
 
Chukua mtoto wako ukae nae nyumbani na umfundishe mwenyewe
Wadau naombeni ushauri,binti darasa la tatu kaenda shuleni na viatu ambavyo mwalimu anadai havitakiwi shuleni,mwalimu amemchapa sana tuu kwa.sababu hiyo, hivi hili kosa mtoto alistahili adhabu hii?shule wana.diary ambayo walimu wanafanya mawasiliano yote na wazazi kupitia humo,halijafanyika zaidi ya kumshushia kibano,hii ni sawa?!?!
 
Hawezi kusahau kumuambuia mzazi wake

Inategem na mtoto kuna mtoto mwingine kwa kumchapa anakuwa mwoga
Atatoka nyumbani vizuri akifika njian anatafuta pa kujificha haendi shule.
 
Sawa mzazi nae aplay part yake kwa kuhakikisha mtoto anafika shule

Kama ni mzazi makini atafahamu kama mtoto wake afiki shule
 
Kuchapana ni ushamba. Kwani viatu tofauti vikivaliwa mtoto haelewi akifundishwa?
Ndio maana nasema mwalimu wa kumchapa mwanangu nitalala naye mbele
 
Lakini kila sehemu ina utaratibu wake
Kwa nini mwanao aviolate alafu aachwe kama hutaki mwanao aguswe hakikisha anafuata taratibu kama zilivyo wekwa.
 
Sawa mzazi nae aplay part yake kwa kuhakikisha mtoto anafika shule

Kama ni mzazi makini atafahamu kama mtoto wake afiki shule

Kuna watu professionals zao zinawashinda
Kuna sababu za msingi za kumchapa mwanafunz
Kuna sababu za kuzungumza na mwanafunz
Na kuna sababu za kumpa adhabu mwanafunzi..

Waalimu wengi wanashindwa na hizo mbili za mwisho wamekimbilia hiyo ya kwanza.

Usipambane na matokeo ,pambana na chanzo.
 
Acha kumdekeza mwanao,
Wewe kama unamdekeza, akija shule na viatu visivyopaswa, sisi kama walimu hatuna budi kumshushia kipigo.
Kweli kabisa. Mitoto ya sasa imedekezwa sana na ndiyo maana kitu kidogo tu inakimbia shule. Na kwakuwa siasa imetawala hadi majumbani na mzazi anakuja juu.

Utakuta mtoa mada alisoma kwa msoto na adhabu kali shuleni, lakini kwakuwa siasa imemtawala anaona mtoto kaonewa.
 
Wadau naombeni ushauri,binti darasa la tatu kaenda shuleni na viatu ambavyo mwalimu anadai havitakiwi shuleni,mwalimu amemchapa sana tuu kwa.sababu hiyo, hivi hili kosa mtoto alistahili adhabu hii?shule wana.diary ambayo walimu wanafanya mawasiliano yote na wazazi kupitia humo,halijafanyika zaidi ya kumshushia kibano,hii ni sawa?!?!
Fanya utafiti kwanza unaweza kulaumu upande mmoja kumbe makosa yako upande mwingine.hivi vitoto ni kiburi Sana sijui Ni kutokana na malezi watokako au lah.huenda mwalim alikua na lengo la kutoa adhabu ndogo Sana ila ukaidi wa mwanafunzi ukapelekea mwl kugafilika.pia huenda mwl alimkanya Zaid ya Mara 2 kuhusu viatu hivyo na mwanafunzi akakaidi.mwisho je kanuni za shule zinasemaje juu ya sare hasa viatu kwa wanafunzi??? Kuna muda wazazi wenyewe pia makosa wanafanya ila kwa kutokujua zigo la lawama litamdondokea huyo mwl.
 
Kuna watu professionals zao zinawashinda
Kuna sababu za msingi za kumchapa mwanafunz
Kuna sababu za kuzungumza na mwanafunz
Na kuna sababu za kumpa adhabu mwanafunzi..

Waalimu wengi wanashindwa na hizo mbili za mwisho wamekimbilia hiyo ya kwanza.

Usipambane na matokeo ,pambana na chanzo.
Mahusiano yakiwa mazuri kati ya walimu na wazazi hili linawezekana.
Lakini unakuta mzazi hatoi ushirikiano kwa mwalimu akiitwa shule haji hii inapelekea ugumu kukomesha hicho chanzo.
 
Waalimu bwana!
Sasa ukimchapa mtoto ndo anaenunua hivyo viatu?!
Atakumbuka kumkumbusha Mzazi/ mlezi wake, mana wazazi / walezi wengine hawakumbuki hadi mtoto achapwe shule, arudi nyumbani huku analia.
 
Back
Top Bottom