Ushuhuda wa Injili
JF-Expert Member
- Nov 12, 2012
- 427
- 160
Bwana Yesu apewe sifa.
Mwana wa Mungu tumeangalia kwa namna moja au nyingine namna ya kumtolea Mungu matoleo na Zaka mbali mbali. Kwa sasa nataka nikuonyeshe maeneo kadhaa ya kumtolea Mungu ili upokee baraka katika utendaji kazi zako.
Ndugu yangu ni vizuri sana kukwambia jambo hili. Maskini, walioko katika mazingira yako ni watu muhimu sana kuwafikishia injili kwa njia ya matoleo yako. Na Mungu anapenda tuwakumbuke maskini tunaoishi nao katika mazingira yetu. Si mara nyingi sana wachungaji wetu wako tayari kutufundisha kuwakumbuka watu tunaoishi nao katika jamii. Wachungaji wetu wengi wanatamani tupeleke matoleo yote ya sadaka na zaka kanisani tu. Ni jambo jema kupeleka sadaka kanisani lakini nakuambia katika jina la Yesu wakumbuke maskini walio katika jamii yako. Huo ndiyo uinjilisti mzuri. Ndugu yangu kama hatuwezi kuwakumbuka maskini na yatima wanaotuzunguka, tunaishi nao mitaani, hivi tunawezaje kujiita sisi ni wakristo tunaomjua Yesu? Ukristo wetu uko wapi? Jirani yako maskini hapo analala njaa, wewe unamuacha hapo akifa na njaa unabeba zaka kupeleka kanisani tu. Ukristo wako uko wapi?
Mtume Paulo anajenga msingi wa kuwakumbuka maskini katika jamii. Anasema Walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa (Petro), na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; ILA NENO MOJA TU WALITUTAKIA, TUWAKUMBUKE MASKINI; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya #Gal 2:9-10
Msingi wa kanisa la kwanza la Kristo lilijengwa katika misingi ya kuwajali maskini, wajane na yatima. Lakini hapa katikati makanisa yamewasahau kabisa maskini na hata baadhi ya watumishi hawataki kabisa kuonyesha moyo wa kuwajali maskini.
Ndugu zangu maskini ni watu ambao Mungu anawapenda. Maskini wako katika mawazo ya Mungu kila wakati. Na anataka tuwajali katika mazingira tuliyonayo. Maandiko yanasema kwamba Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema #Mithali 19:17. Maandiko hayatuambii tuwakumbuke maskini walioko kanisani tu. Tunao maskini ambao tunaishi nao katika vijiji vyetu, katika mitaa yetu. Wanapaswa kuonja upendo wa Yesu kupitia mimi na wewe. Bwana Yesu anasema kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Maandiko yanasema kwamba Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia Bwana, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako #Kumb 15:7-11
Ndugu yangu ni amri ya Mungu tuwakumbuke maskini. Tena tuwape haja za mahitaji yao kama wanauhitaji pasipo kutegemea kurudishiwa nao. Bwana Yesu mwenyewe anasema Roho wa Bwana yu juu yangu,Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Si tu kwamba Bwana Yesu anawataka maskini wa kiroho tu bali na maskini na wa kimwili. Mungu pamoja na kwamba anaijari roho ya mwanadamu lakini hata mwili wake pia. Maskini ni moja ya watu ambao Mungu anawajari na anawapenda. Ndugu yangu wakumbuke maskini ulionao katika jamii yao.
Wakumbuke maskini ndugu yangu utapokea baraka sana katika familia yako. Utapokea baraka katika kazi zako.
Nimejifunza kumtolea Mungu zaka na sadaka kwa watu wenye uhitaji mbalimbali. Kwa sababu hii nimejikuta nikijenga mahusiano ya karibu sana na watu ambao hata kanisani hawaji. Lakini wakati mwingine najikuta watu hao wanatamani kuja kuabudu nasi kanisani. Nilikuwa nikimsaidia kijana mmoja wa kiislamu. Yule kijana siku moja akanishangaza sana. Akanambia brother mie nataka unipeleke kanisani kwenu. Ninatamani niwe mkristo kwa sababu ya mambo unayonitendea. Nikamshangaa sana. Lakini ndani yangu nikaelewa kwann anasema hivyo.
Ndugu zangu kaa karibu na maskini ulionao mitaani. Ukiwa karibu nao kwa matoleo yako nakuambia hata kuwahubiria injili ni kugusa tu.
Hujawaona baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakijitolea kuwa karibu na maskini? Huoni kama baraka haziachani nao?
Roho Mtakatifu kwa kinywa cha Paulo anasema 'Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema'.
Naomba nikomee hapa kwa sasa na Mungu akubariki. Ukiwa na jambo unataka utushirikishe tuombe pamoja nawe, tutumie kwenye whatsapp tu kwa namba hii 0758443873. Ikiwa unataka kutupigia au kututumia sms ya kawaida basi tumia namba 0712204937. Kama unataka tuombe kwa ajili ya mtu fulani au kwa ajili yako tafadhali utupe majina yako kamili unayoyatumia ili tuombe mbele za Baba wa mianga kwa ajili yako.
Yamkini unataka upate mafundisho haya kila siku kwa whastapp basi save namba 0758443873 na kisha tuambie majina yako ili tuwe tunakutumia mafundisho.
www.facebook.com/UshuhudawaInjili