Kusaidia Mtoto wa Nursery home work ni ngumu sana. Jana nimemuuliza swali la hesabu: "Nina pipi tano, nikiwagawia watoto watatu, kila mmoja pipi mojamoja nabakiwa na pipi ngapi?
Akaniambia, “Toa kwanza nizione…”
Hizo kusaidiwa home work na wazazi ni tatizo sana, najiuliza homework akikusaidia mshua alafu ukakosa zote sijui utamwangalia kwa jicho gani! Au unavunga kumlindia heshima.
Ndiyo yale juzi namuuliza mtoto mmoja wa jirani yangu kilo ya mawe na kilo ya manyoya ya kuku ipi nzito akasema ya mawe nilichoka na yupo darasa la tano.