Pole sana kakaDah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa youngster kichizi.
It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.
Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.
Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.
Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Pole sana sanaHili jambo lisikie kwa mwingine lisikukute.
Ilikuwa ni usiku wa kuamkia jumatatu ya tarehe 24.5.2022 ambapo nilisikia simu ikiita majira ya saa 7 kasoro usiku, kuangalia ni Baba alikuwa akinipigia nikapokea. Ujumbe ule hautawahi nitoka masikioni na kichwani mwangu milele, ulikuwa ni ujumbe wa "Mama yako amefariki usiku huu". Hapo nikiwa Dar es Salaam huku familia ikiwa Mwanza. Sijawahi safiri safari ya Taabu na Mateso kama ile, ilinibidi niondoke jumanne kwenda kumzika mama. Mara zote mama ndiye alikuwa akitufungulia mlango tulipokuwa tunarudi kutoka tutokako ama tukiwa tunasafiri alfajir ila hiyo siku nilimkuta akiwa kalala kwenye jeneza. Isikieni tu hii kitu. Nashindwa kuandika zaidi
Pole sana kaka
Mungu mbariki mama yangu na uwape amani wote waliopoteza mama zao
[emoji120][emoji120][emoji120]
Shem kumbe tunafanana.. Pole sanaPumzika kwa amani shujaa wangu mama.
Pumzika kwa amani rafiki yangu kipenzi baba.
Asante sana, pole na wewe shem.
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji173]Asante sana, pole na wewe shem.
Pole ankalHuu uzi kwann nimeuona? [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]