Mama yangu alifariki 2021 lakini nimeshindwa kabisa kufuta namba yake kwenye simu yangu pamoja na kwamba ninajua hiyo namba haitumiki tena.Utamkumbuka jambo kubwa likitokea na yeye ndiye mtu wa kwanza unayetaka kumpigia simu lakini unajua ukijaribu, haitakuwa sauti yake upande mwingine.
Wazazi wote ni muhimu hasa Baba akiwa responsible one.
Kuna wakati Mzee anafariki unaona jinsi Mama anavyolia kwa uchungu kwa kuwa anajua Kazi ya kulea watoto/mtoto peke yake itakavyokuwa kubwa.
Bahati mbaya wote hawako hai.
Leo hii nimeanza kupata maokoto ya kuweza kuwajengea nyumba ama kuwakatia bima maalumu kwaajili ya Uzee wao lakini ndiyo hawapo.
Kama kuna siku ya kukutana nao huko ahera, basi lazima nitamchana Mzee ukweli kwamba alikuwa mwoga wa maisha ama nini, kwanini aniache nikiwa na miezi 10?
Bi mkuwa naye lazima nije nimwambie, kwanini aliamua kuondoka wakati nilibakiza miaka 7 aanze kuonja matunda ya jasho lake la kunisomesha na kuniangahikia kote kule.
=======
Hongereni mlio na Mama ~ Bahati Bukuku Song
Pole mno ndugu yangu, mwenyezi Mungu awajalie pumziko lenye amani.Dah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa na umri wa miaka 10 tu.
It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.
Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.
Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.
Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Huwa ni ngumu saana mkuu kufuta namba ya mtu uliyekuwa ukimpenda kwa dhati[emoji24][emoji24][emoji24]Mama yangu alifariki 2021 lakini nimeshindwa kabisa kufuta namba yake kwenye simu yangu pamoja na kwamba ninanajua hiyo namba haitumiki tena.
R.I.P mama⚘
Asante Mkuu.Pole sana Mkuu, habari za kuwachana achana nazo, hawakuamua wao kuondoka, ni wakati ulifika kama ambavyo na sisi Iko siku tutaondoka hapa duniani Kwa nyakati tofauti tofauti.
Asante Mkuu.
Ila nilipitia kipindi kigumu sana waliponitoka.
Ni rehema tu za Mungu zimesaidia kunifikisha hapa nilipo.
Pole sana MkuuNakuelewa sana, nilimpoteza Mzee baada ya kumaliza kidato Cha sita. Ilinifanya nianze majukumu mapema sana. Kuna kipindi unatamani angekuwepo aone matunda ya jasho lake lakini unaishia kusema huko aliko atafarijika na jinsi mambo yanavyoenda.
Ni takriban miaka 18 imepita lakini Bado kumbukumbu za Hilo tukio la kuondoka kwake hazijawahi kuzoeleka.
Pole sana Mkuu
Binafsi Mzee aliniacha nina miezi 10
Bi Mkubwa aliniacha nipo Kidato cha 4.
Lakini Mungu alivyo wa ajabu nikasoma hadi nikamaliza Bachelor bila hata shilingi 10 ya ndugu.
Wacha Mungu aitwe Mungu 🙌
Upo sahihi Mkuu, Mungu ni mwema kwa kweli 🙏Kuna vitu Mungu anafanya ili uendelee kuurambua ukuu wake.
Na hicho ndio kitu kilinifanya nisikufuru wakati wa msiba. Nikajiambia, mbona Kuna watu wamefiwa na wazazi wao wangali Wadogo, wengine hawakubahatika kuonana nao kabisa na hawawafaham, kwanini Mimi nione kama nimeonewa sana?
Pole sana Mungu aendelee kukufariji.Dah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa na umri wa miaka 10 tu.
It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.
Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.
Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.
Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Nashukuru sana mkuuPole sana Mungu aendelee kukufariji.
kila mtu anarudisha upendo kwa yule aliyewahi kuwa nae karibu na kumpenda kwa dhati.[emoji419][emoji375]Poleni mnaowakumbuka Mama zenu.
Jana nilikuwa msibani mtaani kwetu, nikashuhudia katoto chenye umri wa miaka 7 kakimlilia sana Baba yake aliyekuwa amefariki na anazikwa jana.
Niliambiwa kuwa katoto kalikuwa kanapendwa sana na Baba yake, Mama wa huyu mtoto ana watoto sita, kila mtoto na Baba yake. Alikuwa hatulii Nyumbani na ni mtu wa kupombeka muda mwingi na wala hajali kuhusu watoto wake.
Baada ya mazishi kale katoto kalikuwa kanawalilia ndugu wa Baba yake kuwa waondoke wote wasimuache pale na Mama yake. Katoto hakamtaki mama yake mzazi. Hivyo uzi huu umenifikirisha sana kuwa watu hatufanani, kila mtu anarudisha upendo kwa yule aliyewahi kuwa nae karibu na kumpenda kwa dhati.
Pole sana mkuuDah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa youngster kichizi.
It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.
Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.
Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.
Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Pole sana MamndenyiMama hana mbadala.
😭😭 Nilie machozi yatoke ya damu? Haisaidii.
A day we will meet in Heaven. Tutaongea . Nitakusimulia kila kitu.
Pole sanaUjumbe mzuri sana, ujumbe umebeba hisia nzito sana zinazo gusa moyo kwa pendo la mama, tuongee kila kauli kwa mwanamke lakini mwanamke alikiwa kwenye engo ya mama aiseee!
Binafsi sijawa sikuonja upendo wa mama yangu ila kuna wakina mama walisimama kama mama yangu mpaka nipo hapa leo, kinacho niuma sijawahi kuiona taswira ya mama, wala mfanano wake isipo kuwa kaburi tu ndio nimeonyeshwa!
Mwenyezi Mungu awape mema yote mazuri wakina mama, Mungu awajalie pia mabinti wote wawe wakina mama wazuri ili kutoka kwao na watakao tokana nao watoe sifa zote njema kwa Mungu na kumshukuru.
Asante Mungu , Asante mama.
Hivi wewe msimbe umerogwa?Kumbe hata wachawi wana majonzi?