Kumpenda usiemjua

Lizzy yote haya ni mahangaiko ya moyo! Lakini si unajua mtu akipenda huku akiongozwa na imani yake?

Sasa we Yericko si uweke siredi yako ya kumzimia Lizzy?Ngoja nikusaidie.......................................................................... Tuiite...........
Yangu nafsi kwa Lizzy

Lizzy mi nakuzimia,ninahisi nakujua,
Moyo wangu waumia,tafakari kinijia,
Hakika umeingia,akili nivurugia,
Najua waikubali,yangu nafsi bila kikomo

Sasa endelea........................
 
Sasa we Yericko si uweke siredi yako ya kumzimia Lizzy?Ngoja nikusaidie.......................................................................... Tuiite........... Yangu nafsi kwa LizzyLizzy mi nakuzimia,ninahisi nakujua,Moyo wangu waumia,tafakari kinijia,Hakika umeingia,akili nivurugia,Najua waikubali,yangu nafsi bila kikomoSasa endelea........................
Hahaha...ye alishafikisha ujumbe.Amesema wazi kukupa moyo kwamba INAWEZEKANA!!
 
Dada mbona umenigusa sana! Yani mimi binafsi namzimia Lizzy kuliko ile kawaida!! Kila nikitafakari nahisi namjua na kumfahamu,vilevile nahisi ni mtu anayeikuba nafsi yangu bila kikomo!! Dada Ballerina kwakweli kulingana na kazi yako nahisi ndoto ya kumpata Lizzy inatimia!!
Nimekugoa thanks!!

Hii Lyrics uliiona Lizzy?(refer bolded)
 
Mhhh hauko peke yako

Mhhhh! Kumbe na wewe umo? hahahahahah lol! We acha! Kama moyo umeshapenda basi ni lazima tu ajulikane hata kwa udi na uvumba :) Kila la heri Ballerina.

 
Last edited by a moderator:
Inawezekana kabisa. Tena siku ukimuona unaweza kumpenda zaidi tofauti na mngeonana before hamjawa na mawasiliano.
 
Yamekua hayo?!Haya mama kwaheri...kila la kheri!

So sorry my dear,tena avatar yako inanikumbusha my best friend wa enzi hizo(TK),sipendi kukuudhi.Huyu Yericko asitugombanishe!na aje aseme alichomaanisha.Hizi hlugha za shule wengine tulishazisahau.
 
Ndotoni alinijia,rangiye nikaiona,
Hakika linivutia,physiq nikaiona,
Nasema sitajutia,ndoto zangu afanana,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Simu nakaichukua,meseji nikaandika,
Mimi wewe mekuona,rangi yako kadhalika,
Kwa vipimo nimeona,mwili wako ni hakika,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Akajibu ni hakika,afanana na ndotoni,
Hata mwili kadhalika,akasema si ndotoni,
Eti labda nina picha,nemeona kwa fulani,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?[/QUOTE]

Inawezekana ila ni mara chache sana na wakati mwingine huwa ni hatari. so be careful mydear usiendeshwe sana na hisia


Na akili ifanye kazi,eti eeh?Hapo umenistua kamshipa fulani kanakoelekea kwenye fahamu. Kamshipa haka na kale ka hisia havikai pamoja hata siku moja!Asante kwa ushauri.
 
inatia huruma sana,,,,,, kumpenda usiyemjua kwani unaongozwa na hisia,, jipe moyo,,, go straight approach the person,,, in a way ya kumchunguza zaidi,,, unaweza kuta si ndivyo udhaniavyo,,,,
best wishes
 
Jukwaani naingia,mimi naja ulizia,
Moyoni kaniingia,kijana nisomjua,
Mara nyingi nawazia,mtimani kaingia,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Si sauti wala sura,machoni sijamtia,
Nimekuja kwa hadhira,msada kunipatia,
Msidhani nadhurura,ovyo kujiokotea,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Mtandaoni tulianzana,tena kwa kuliwazana,
Tumaini kupeana,matatizoni kutoana,
Kisha namba kapeana,meseji twatumiana,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Sifichi nawaambia,moyo wangu umezama,
Naogopa kumwambia,maadili natazama,
Mwenzenu naugulia,mapenzini nimezama,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Ni mitatu imepita,miaka nilosubiri,
Alonitenda kapita,alonilisha shubiri,
Nami sikupitapita,mwema nikimsubiri,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Kwa sifa pia vigezo,katimia nawaambia,
Msidhani ni mchezo,sitanii nakazia,
Nataka yenu mawazo,nipate pa kuanzia,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Hakutendwa siku nyingi,bado anaugulia,
Yalomkuta si mengi,mpenziwe kachukuliwa,
Alimfanyia mengi,kidhani mtarajiwa,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Nitampenda alivyo,hisia zaniambia,
Akiniona nilivyo,sijui tanikimbia?
Wajua nini tatizo,kunipenda hajanitamkia!
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?


Tamati naishilia,ukingoni nimefika,
Mwenzenu navumilia,moyoni amenifika,
Hawezi hata zania,hali hii mi kufika,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?
Kuwa makini sana ballerina..wengine hali zetu mbaya kwa kupenda wanaume tusowajua!mbona nimepatikana mwaka huu!
 
Back
Top Bottom