Kumpenda usiemjua

Ballerina

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
386
187
Jukwaani naingia,mimi naja ulizia,
Moyoni kaniingia,kijana nisomjua,
Mara nyingi nawazia,mtimani kaingia,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Si sauti wala sura,machoni sijamtia,
Nimekuja kwa hadhira,msada kunipatia,
Msidhani nadhurura,ovyo kujiokotea,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Mtandaoni tulianzana,tena kwa kuliwazana,
Tumaini kupeana,matatizoni kutoana,
Kisha namba kapeana,meseji twatumiana,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Sifichi nawaambia,moyo wangu umezama,
Naogopa kumwambia,maadili natazama,
Mwenzenu naugulia,mapenzini nimezama,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Ni mitatu imepita,miaka nilosubiri,
Alonitenda kapita,alonilisha shubiri,
Nami sikupitapita,mwema nikimsubiri,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Kwa sifa pia vigezo,katimia nawaambia,
Msidhani ni mchezo,sitanii nakazia,
Nataka yenu mawazo,nipate pa kuanzia,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Hakutendwa siku nyingi,bado anaugulia,
Yalomkuta si mengi,mpenziwe kachukuliwa,
Alimfanyia mengi,kidhani mtarajiwa,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Nitampenda alivyo,hisia zaniambia,
Akiniona nilivyo,sijui tanikimbia?
Wajua nini tatizo,kunipenda hajanitamkia!
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Tamati naishilia,ukingoni nimefika,
Mwenzenu navumilia,moyoni amenifika,
Hawezi hata zania,hali hii mi kufika,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Ballerina leo umefunguka mama? This is very good na hakuna furaha kama ya kuona mtu unayemuwish mema anakuwa na furaha.....I am happy for you mama lwa angalau kumove a step forward. Hali ya kutamani kupendwa/penda tena baada ya kuumizwa ni hatua kubwa ya kukujulisha kuwa umekomaa kimapenzi kwani maisha lazima yaendelee.

BTW
1. U Malenga mzuri sana, nimelipenda shairi lako
2. Wahenga walitwambia Mwanzo wa kuni ni moja................hisia ulizozielezea hapa ni hisia njema za mapenzi but the fact kuwa humjui inakuweka kwenye kundi la kumtamani, unatamani kumjua zaidi ili uone kweli anapendeka? fungua moyo mpe nafasi ya kuwa karibu nawe kirafiki, mjue kwanza ...................kila la kheri Ballerina
 
Asante kwa ushauri ila kumbuka SIJAWAHI KUMUONA,kama nikutamani basi nimetamani sifa zake ambazo sijaziprove ie(kindhearted,openminded,mcheshi,straight forward,anayejiheshimu),tena tunashare alot of interests/hobbies.
Nitajitahidi kupata nafasi ya kuhakikisha .
 
Nikutakie kila la kheri Ballerina girl
 
Shairi zuri sana! One advice: Kama nnafikiria kwenda one step further, ni better umfahamu mtu huyo. Kuna impression ambayo utaipata pindi mtakapo onana kwa mara ya kwanza, ambayo ndiyo huamua kama kweli kuna mapenzi ya dhati kati yenu au wote mnapenda meseji ambazo mnatumiana. Kama kila mmoja wenu anapeda the way mnavyo wasiliana, nakushauri msifikirie kukutana kwa kuwa ikitokea kila mtu ameona phyisical appearance tofauti na namna alivyokuwa akifikiria, that will be the end of mawasiliano. Ingawa the reverse is true, mnaweza mkakutana na kila kitu kikaenda vizuri. That is the risk all of you have to take! GOOD LUCK!...!
 
kila la kheri mpendwa.

Fanya muonane uso kwa uso ili yatimie uyawazayo juu yake.
 
kila la kheri mpendwa.

Fanya muonane uso kwa uso ili yatimie uyawazayo juu yake.

Ndotoni alinijia,rangiye nikaiona,
Hakika linivutia,physiq nikaiona,
Nasema sitajutia,ndoto zangu afanana,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Simu nakaichukua,meseji nikaandika,
Mimi wewe mekuona,rangi yako kadhalika,
Kwa vipimo nimeona,mwili wako ni hakika,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Akajibu ni hakika,afanana na ndotoni,
Hata mwili kadhalika,akasema si ndotoni,
Eti labda nina picha,nemeona kwa fulani,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?
 
ukweli hilo limenigusaa but nimejifunza na makosa,, hauko peke yakooo,, tupo wengi,, but fimbo nilioipata mpka leo nina kidonda achiliambali kovu ,bado nina maumivu ,kua muangalifu mpenzi..
 
Whaao!! ufanikiwe kumpata huyo wa moyoni Ballerina!

btw, jina lako linanikumbusha sana wimbo huu (sorry kutoka nje ya mada ila nimeshindwa kujizuia)

Last edited by a moderator:
Ndotoni alinijia,rangiye nikaiona,
Hakika linivutia,physiq nikaiona,
Nasema sitajutia,ndoto zangu afanana,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Simu nakaichukua,meseji nikaandika,
Mimi wewe mekuona,rangi yako kadhalika,
Kwa vipimo nimeona,mwili wako ni hakika,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?

Akajibu ni hakika,afanana na ndotoni,
Hata mwili kadhalika,akasema si ndotoni,
Eti labda nina picha,nemeona kwa fulani,
Jamani yawezekana,Kumpenda somjua?[/QUOTE]

Inawezekana ila ni mara chache sana na wakati mwingine huwa ni hatari. so be careful mydear usiendeshwe sana na hisia
 
Whaao!! ufanikiwe kumpata huyo wa moyoni Ballerina!

btw, jina lako linanikumbusha sana wimbo huu (sorry kutoka nje ya mada ila nimeshindwa kujizuia)

Thankx so much BelindaJacob,the song is nice,it left me with a wide smile.Appreciated my dear!
 
Last edited by a moderator:
Dada mbona umenigusa sana! Yani mimi binafsi namzimia Lizzy kuliko ile kawaida!! Kila nikitafakari nahisi namjua na kumfahamu,vilevile nahisi ni mtu anayeikuba nafsi yangu bila kikomo!! Dada Ballerina kwakweli kulingana na kazi yako nahisi ndoto ya kumpata Lizzy inatimia!!
Nimekugoa thanks!!
 
Dada mbona umenigusa sana! Yani mimi binafsi namzimia Lizzy kuliko ile kawaida!! Kila nikitafakari nahisi namjua na kumfahamu,vilevile nahisi ni mtu anayeikuba nafsi yangu bila kikomo!! Dada Ballerina kwakweli kulingana na kazi yako nahisi ndoto ya kumpata Lizzy inatimia!!Nimekugoa thanks!!
Hahahhh!!Yericko umeamua kumwaga radhi kabisa ?!
 
Back
Top Bottom