Kumpeleka sanchez Manchester united ni kurudia makosa ya 2012

Dkileo

Member
May 23, 2017
51
46
Mwezi agosti mwaka 2012 Arsene Wenger alimpeleka Van Persie Manchester united.Hii ilikuwa baada ya mwishoni mwa msimu wa 2011-2012 Van Persie kugoma kusaini mkataba mpya na Arsenal..Utakumbuka kuwa msimu huo wa 2011-12 Van Persie alimaliza akiwa top scorer wa EPL akiwa na magoli 30..Bingwa alikuwa Man City..Ilimlazimu wenger kumuuza Van Persie kwa kuwa mkataba wake ulikuwa ukiisha mwishoni mwa msimu wa 2012-2013 hivyo angeweza kuondoka bure..Hivyo wenger kuamua kumpa Sir Alex Ferguson SMG..Na alipofika United Van Persie alifanikiwa kushinda taji la EPL katika msimu wake wa kwanza huku akiwa top scorer kwa magoli 26…

Hivi sasa kuna tetesi kuwa Man United na Arsenal wapo katika mazungumzo juu ya yhamisho wa Sanchez..Mkataba wa Alexis Sanchez unaisha mwezi june 2018..Hivyo endapo Arsenal wataamua kubaki na Sanchez mpaka mwishoni mwa msimu basi ataondoka bure kabisa…Je ni bora kubaki na Sanchez au kuchukua paundi milioni 30 kwa ajili ya mchezaji ambaye mkataba wake umebakia pungufu ya miezi sita????

Hii movie inafanana kabisa na ile ya Van Persie…Nadhani kuna tatizo ndani ya Arsenal juu ya mikataba ya wachezaji haswa wachezaji nyota wa timu

Sanchez ni tiba sahihi ya Man United

Man united wanakosa mchezaji aina ya Sanchez..Kwanza kabisa United hawana winga wa kueleweka..Martial na Rashford ni namba tisa wale vijana lakini inamlazimu Jose kuwatumia kama mawinga…Jose Mourinho ni mtu wa kupaki basi na kushambulia kwa kushtukiza…Hivyo anahitaji kuwa na mawinga wenye kasi sana..Ambapo kwa sasa hana aina ya winga kama sanchez…Kwa Mourinho kumpata mchezaji kama Sanchez ambaye anaumwezo mkubwa wa kukokota mpira,kutengeneza nafasi za kufunga,kufunga magoli na pia ni mtaalam wa mipira iliyo kufa ni kama kuokota dodo chini ya mbuyu..Sanchez ni tiba sahihi ya Man united..


Nadhani hali kama hii angekuwa nayo Mourinho Sanchez asingeweza kwenda Man united au Man city..Jose hawezi kukuuzia silaha kirahisi..Labda timu yako iwe chini sana kuliko yake…Nakumbuka hata pale alipoamua kumpeleka Petr Cech Arsenal ,Arsenal hakuwa mshindani mkuu wa ligi kwa Chelsea…


Wacha wenger alipe fadhila kwa Mourinho..Maana petr cech alikuwa na thamani ya point 15 za Epl..
 
Watu waichokukua ni kia wamiliki wa sasa hivi wa arsenal sio mashabiki wa mpira,wao ni profit kwenda mbele. Ingekua wanaumuzwa na matokeo mabaya wasingekubali kumtoa kwa mpinzani wao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom