Kumlazimisha Nassari kuomba radhi ni bora zaidi kuliko kumtetea!

Kwangu mimi CDM ni chama makini sana
Naamini sakata hili mh Mbowe alisha liona kuwa dogo katokota
nashangaa wanaokomalia kumkingia kifua nassari wakati chama chenyewe kimeiona ina muskheri
 
Wanajamiiforums wenzangu naomba muelewe kuwa siyo ridhaa ya polisi kuwabughudhi wanachama wa Chedema bali ni amri ya watawala. Karibia makamishna wa polisi wote wana degree za sheria yaani LL.B na LL.M lakini hawazitumii kwa sababu wanapokea amri toka kwa mwajiri wao a.k.a Serikali/Government of the URT. Naomba kuwasilisha
 
Kumekuwepo na maneno mengi sana juu ya tamko la mbunge wa Arumeru Mashariki J Nassari,na zana ya ukanda ama ubaguzi kwa baadhi ya watu na wanachama wa chama cha mapinduzi na hata viongozi wake kwa kuchukua hili kulifanya kuwa ni ajenda yakujadiliwa na Taifa zima,wamesahau kuwa watanzania wanataka umeme wa uhakika kudhibitiwa kwa mfumuko wa bei na kuondokana na ugumu wa maisha,pia wamesahau kuwa watanzania wanataka mabadiliko ya Katiba na kutaka mawaziri wote walio ondolewa madarakani na Rais wanachukuliwa hatua za kisheria,pia wale wote waliousishwa na tuhuma za kifisadi wanachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufikishwa mahakamani,sasa wanazunguka nchini kutangaza au kumshitaki ama kuishitaki CHADEMA pasipo kuwa na hakika au kujitoa fahamu kuwa hawajui watanzania wanataka nini. Kauli ya Joshua Nassari haiwezi kuondoa mfumuko wa bei haiwapeleki mafisadi mahakamani na wala haiondoi ugumu wa maisha kwa watanzania hata kufikia kuwagawa watanzania,kinachoweza kuwagawa watanzania ni hali ya maisha duni licha ya kuwa na Nchi yenye neema kama Tanzania. Nawashauri ccm maneno ya J Nassari sio kigezo cha ugumu wa maisha unao wafanya mashabiki wa chama chenu kuwakimbia,tekelezeni ahadi zenu katika chaguzi zilizopita kwa mujibu wa ilani ya chama chenu ili walau mrudishe matumaini kwa wananchi wanao kata shauri na kukimbilia chadema.
 
Back
Top Bottom