Kumlazimisha Nassari kuomba radhi ni bora zaidi kuliko kumtetea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumlazimisha Nassari kuomba radhi ni bora zaidi kuliko kumtetea!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, May 10, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni mbunge wa Arumeru Mashariki J. Nassari alikaririwa na vyombo vya habari akitoa matamshi fulani (yanayoonekana kama ya kichochezi) juu ya kanda ya kaskazini kujitenga na kumzuia raisi kufika/kuitembelea Arusha. Kauli hizo za Nassari kwa kiasi chake sio nzuri na wala hazipaswi kutamkwa na kiongozi yeyote na haswa haswa kutoka CHADEMA (kumbuka CHADEMA inahusishwa na ukanda).
  Wengi wamejitokeza haswa hapa JF kumtetea Nassari huku wengine wakirefer kauli nyingine mbovu zilizowahi kutolewa na viongozi mbalimbali. Mi naamini kumtetea Nassari hatumsaidii wala hatumjengi kisiasa, jambo la msingi ni wote tukubali kuwa Nassari alikosea na kama tunampenda basi tumlazimishe aombe radhi na kufuta kauli na sio kumtetea wakati kosa lipo wazi na linaonekana kwa kila mtu.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tuwaache wahusika washughulikie hilo, chadema ni chama makini ambacho kina watu wanaoweza ku-handle hii issue kikubwa zaidi kuliko ccm
   
 3. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Huu ni upepo.....
   
 4. r

  republicoftabora Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona zenji kila siku wao ndio nyimbo zao na hakuna anayewalazimisha kuomba radhi?
   
 5. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  wote mnaongea sana ila wote hamjajaliwa kuwa na uwezo wa kuona mbali. naomba msubiri kuona miujiza muda si mrefu...........................hata wana wa israel wakiwa jangwani walikataa mane wakisema heri wangekuwa misri maana walikula nyama............................unadhani Nasari arikurupuka? jibu ni HAPANA. CDM wanafanya siasa za sayari nyingine siyo hiii tunaishi.........................huwezi kuwaelewa ila wanaona mbali...................CCM bado wanasogezwa king ila wao bado hawajajua hilo........................kila japo liko planned na lina maana kwao.......
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Wewe acha ushabiki imeshazungumziwa sana naona ulikuwa na beki tatu wako ukakirupushwa unakimbilia kuandika thread
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  alikuwa nawaunganisha wale waliokwisha tengwa na serikali ya ccm.
  mery nagu alishatoa msimamo wa ccm kuwa jimbo litakalo wapa wapinzani kura linaenda likizo,sasa kosa lipo wapi kuwaunganisha walioko likizo?
   
 8. m

  mathjr New Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Mimi sijufurahishwa na kauli ya Nassari na una unapofananisha issue yake na watu Kama jussa ambaye watz tumempuuza unataka Nassari na yeye apuuzwe? Naunga mkono hoja ya kuomba radhi kwani cdm kuna watu makini wa kauli zao. Dr Slaa Nakuomba umpe assigment kamanda Myika ya kumsuka Dogo Nassari maanahofia kuendelea kubwabwaja.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa ndio huwa mimi natofautiana na wengi. Kama CCM wabaya na wanatamka mambo mabaya kwa nini CDM chama makini kiwe kinajilinganisha na CCM?
   
 10. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KIMBUNGA,Hawa sisiem inabidi tujitofautishe nao matamshi mabaya yenye kubaguana,sisi tukomae na mambo muhimu ya kijamii,hapo tutakuwa tumewaumiza vibaya sana.MPUMBAVU MPUUZIE.
   
 11. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono.Kvambua kosa ni hatua nzuri ya kujirebisha.MH:SAAAAAANA. J.NASARI.jishushe uombe radhi itakutoa ktk hatua uliyopo hv sasa mpaka hatua nyingine.
   
 12. broken ages

  broken ages Senior Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Matamshi yasiyokuwa ya adabu na yenye hamasa za uchochezi kutoka kwa viongozi wetu tuliowachagua kwa kuwaamini kuwa wanaouwezo wa kutuongoza kwa maana ya kutuvusha salama, kwa namna yeyote ile si kwamba madhara yake ni kwa hao viongozi bali ni kwetu sisi wananchi kwa hivyo hata kiongozi anapokuwa ni mzuri lakini akapotoka kutoa kauli ambazo. Mwisho wake ni vita ama vurugu tunapaswa kumwambia hapana ajirekebishe ili tuepukane na balaa
   
 13. P

  Papaya Senior Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani kunya anye kuku akinya bata kaharisha!! Mary nagu alitoa matamshi ya kibaguzi arumeru mashariki hakuna yoyote aliemwambia kitu. Lusinde nae aliongea matusi mpaka mate yakamkauka mdomoni hakuna aliesema! Dogo janja amekazia tu imekuwa nongwa. Hakuna kuomba msamaha Nasarri meseji sent
   
 14. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba inaonekana mh nassar matamshi yake haya kuwa sahihi.hapaswi kuomba msamaha kwani swala hilo liko kwenye vyombo vya sheria.kwenye sheria hakuna samahani ukiomba msamaha inamaana umekiri kosa hivyo inakupasa kuadhibiwa.cha msingi ni kwamba wapinzani wanatakiwa wawe makini na matamshi yao kwani ccm nao wako maakini kuangalia kasolo zinazojitokezo ili wawapeleke kwenye vyombo vya sheria ili waonekane hawafai.
   
 15. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mnakumbuka mlisema hivi hivi wakati wa swala la wana-chadema 'kumteka' mkuu wa wilaya ya Igunga?
  'Maoni' mengi saana yalitolewa, eti 'ooh, chadema waombe radhi wananchi, ooh, chadema iombe radhi wanawake wa Tanzania'.
  Na baya zaidi, swala lile (kama kawaida) likakuzwa sana na kupewa sura ya udini, nk., mpaka baadhi ya taasisi za dini zikatoa 'ultimatum' kwa chadema kuomba radhi kwa 'kudhalilisha' muumini wao.
  Mnakumbuka ???
  Na zaidi ya hapo (kama kawaida) ikafunguliwa kesi kwa mbwembwe saaana.
  Swali ... Je leo swala lile liko wapi ???
  Watanzania wengi ama ni wanafiki, au ni vipofu saaana wa kuona mbinu za chama tawala kuwabambikizia kesi chadema?
  Kila kitu ni wazi kabisa. Chadema inawindwa sana na serikali na vyombo vya dola ili ibambikiziwe kesi.
  Kama ni swala la kutoa matamshi ya 'uchochezi', nk., basi kila mtoa maneno ya uchochezi ingebidi akamatwe na polisi.
  Ila polisi (kama kawaida) wanachagua nani wa kumkamata. Watanzania bado hawalioni hilo !!!
   
 16. habi alex

  habi alex Member

  #16
  May 10, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Acha ulofa, mtu akiikosea jamii aiombe radhi na wala si funika kombe mwanaharamu apite, aombe radhi vinginevyo nitakidharau rasmi chama cha chadema.
   
 17. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo watu wanakuwa na mapenzi na chama mpaka wanapitiliza kias kwamba hata wanapokosea tunashindwa kuwarekebisha. Wengi tunaipenda chadema lakini, kama mtu una mapenzi ya dhati huwezi kufurahia kila kauli inayotolewa na kiongozi wa chadema hata kama kauli hiyo ni ya upotoshaji na ya kutaka kuwagawa watanzania. Nassari sio malaika ni binadamu na hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu hapa duniani. Mtu yoyote makini anapokosea anapaswa ajitambue na akiri hadharani kwamba amekosea huo ndio ukomavu.

  Marehemu Regia Mtema aliwahi kutoa kauli tata bungeni ya kutaka watu wanaoishi morogoro ambao sio wazaliwa wa morogoro waondolewe na wawaachie wazawa wa morogoro adhi yao. Kesho yake Regia mwenyewe bila hata kushinikizwa alimuomba spika ampe nafasi ili afute kauli yake kwani baada ya kuitafakari aligundua haikuwa kauli nzuri na aliitoa kwa bahati mbaya pengine bila kufikiria kwa kina. Aliwaomba radhi watanzania na akawakaribisha watanzania wote mororgoro kwa kuwa ni ya watanzania wote. Watu wengi sana tulimsifu Regia kwa kutambua kosa lake na tukasema alionesha ukomavu wa kisiasa.

  Tukirudi kwenye kauli ya Nassari, ni wazi kauli aliyoitoa ya kumuhusu rais kikwete na ile ya kusema tugawe mpaka kuanzia mwanza, shinyanga, mara, arusha, manyara ili tujitangazie uhuru kama Sudani ya Kusini sio ya kufurahia wala ya kupigiwa vigeregere. Kauli hii haikufurahiwa hata na mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe ndio maana aliipangua kiaina na kusema kauli ya dogo janja ilikuwa ni kujenga hamasa na sio msimamo wa chadema kwa kuwa wao wanataka tanzania moja. Hivyo basi tunamuomba Nassari ajitokeze na akiri kwamba alitoa kauli hiyo kimakosa. Haitamgarimu chochote bali itamuongezea credit kama ilivyokuwa kwa marehemu Regia Mtema.
   
 18. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #18
  May 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu Wtz hapa lengo kuu hata kama Mh,Joshua Nssari aliteleza katika kuongea wanachokitaka waheshimiwa nikuona kingozi yeyote wa upinzani anapatikana na Dosari. wanaona ndio njia nzuri ya kujiokoa kwenye dhoruba kumbe kwa sasa upepo unavuma kuelekea vijijini kwa watu waliopoteza matumaini.
  Kama maneno ya kejeli, uchochezi, Je? kuwaambia wapinzani wote wana mimba ya CCM nafikili ni tusi kubwa sana hasa ukizingatia kila chama kina watu wa jinsi mbili yaani KE,ME ona ME atakavyoonekana anamimba mbele ya mkewe na bila shaka hata huyo mkewe atakuwa na mimba pengine isiyokuwa ya kwake matusi haya siyo ya kuvunja amani??????? endapo tungeenda kuuliza mimba hizo zina umri gani hali ingekuwaje? Mujwahuzia.
   
 19. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kwa mwendo huu, utadharau vyama vingi saaana hapa Tanzania.

  Labda umesahau, au kama kawaida, unachagua nani wa 'kudharau'.
  Jikumbushe kidogo tu kuhusu jamaa huyu hapa chini kwenye picha...Halafu useme kama 'utakidharau' rasmi chama chake.
  Kumbuka, jamaa huyu alitetewa na katibu mkuu wa chama chake kuwa 'anajibu mapigo'.
  Umnamkumbuka huyu ..... lusinde.jpg ....Kudadadeki !!!
   
 20. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumlazimisha hapana, kwani yeye hana utimamu WA akili? Alipokuwa aikiropoka hayo madudu yake ina Maana hakujua madhara yake? Kama kweli demokrasia iko ndani ya CDM basi wamshughulikie kumnyoosha, aadhibiwe na chama sio kumlazimisha aombe radhi.
   
Loading...