Kumlazimisha Nassari kuomba radhi ni bora zaidi kuliko kumtetea!

Tatizo sio kauli ya Nassary wanaJF wenzangu bali ni UBUNGE wa Arumeru mashariki na Arusha mjini.
 
Nashangazwa sana na serekali inavyo penda kupoteza muda kwenye mambo ya siyo na msingi nilikuwa na fikiri polisi nw wange kuwa busy ku hoji mawaziri walio iba then wana hoji jambo ambalo halina madhara kwa nchi hii. Dola jaribuni kuwa wawajibikaji
 
Mkuu Zubeda Mchuzi, ulichoongea ni sahihi kabisa, jeshi la polisi limekuwa la kipuuzi kabisa,muda wote limekuwa linaangalia CDM wanafanya nini, CDM wamekosea nini, haya mambo ya CDM ndio yamekua their core functions...
 
Hakuna mtu mzima mwenye akili timamu anaweza kuamini for a minute kuwa Nassari anataka watu wa kaskazini wajitenge! Binafsi napinga kabisa. Ni kauli ya kitoto, pengine ni munkari na mbwembwe za kisiasa lakini kamwe sio mkakati wa kujitenga. Yes, si kauli ya kuungwa mkono hata kidogo na mwenyekiti wake aliitolea maelezo pale pale na sasa Nassari mwenyewe amefanunua, ifike mahali sasa for people to grow up na deal with bigger challenges and not some petty petty issues.
Mkuu FJM naamini hata JK hataki waTz wapate tabu wanayopata sasa isipokuwa ni ujinga wa kuamua ufanye lipi na useme lipi kwa wakati gani..........Halafu hii tabia ya kwakuwa CCM wameboronga mambo mazito simply kwakuwa wamekuwa hapo kwa miaka mingi basi tusizungumzie issue za CDM simply kwakuwa hawajawa watawala na hatuwezi kuwahukumu.........kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, hakuna kitu kinaitwa some petty petty issues sababu hizi ndizo saize ya CDM na tutawakosoa wakienda kombo.........
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JMushi nakuunga mkono. Cha muhimu sio matamshi ya Nasari hicho ni kitendo tuu, the motive behind and underlying factors zina justfy kauli ile ni kwa lengo la kuhamasisha na sio kwa lengo la kuvunja nchi!. Mimi nilioa nikiwa kijana sana na nilioa mwana habari mwenzangu tuliekuwa class mates chuoni. Baada ya kuona jinsi wake za watu wanavyotendwa kwenye media nikampiga mkwala kuwa siku nikisikia na wewe unayafanya hayo be it na mabosi au sources, mimi naua!. Lengo la statement lilikuwa ni mkwala tuu to be on her guard. Yeye alinishikia bango eti nimemtishia kumuua!. Sikuomba msamaha mpaka kesho and the rest was history!. Unasimama na unachoamini no matter what!. Vivyo hivyo kwa Nasari kwa vile the motive behind sio kuvunja nchi bali kujenga hamasa, lazima asimame imara na good faith yake!. Hakuna kuomba radhi wala msamaha!. Sasa sana labda afute tuu kauli kwa vile imeeleweka vibaya ila ujumbe ni valid na genuine!.
Mkuu Pasco unaposema alikuwa anahamasisha na si lengo la kuvunja nchi unamaanisha nini? ana muhamasisha nani na kufanya nini?...... Hilo la mkeo siliingilii ingawa unajua wazi hilo ni kosa duniani kote na halijawa halali kwasababu tu hojaomba msamaha kwa mkeo...... Kauli hizi unazoita za mkwara hazina tofauti na za kina Magufuli na kupiga mbizi au watu wale manyasi lakini ndege ya rais inunuliwe...... Tufikie mahali tuweke utaifa kwanza. kauli,matendo, na chochote kile ambacho hakina afya kwa Taifa letu kikifanywa na mtu yeyote tukikemee kwa umoja na si kuanza kuzijengea justfication
 
Last edited by a moderator:
Kwanza hakuna mashtaka yatakayofunguliwa na kama yatafunguliwa kesi itachukuwa muda mrefu sana na hivyo kumpotezea muda Bw. Nasari kushughulikia kero wa wapiga kura wake!

Kinachofanyika hapa ni kupunguza wimbi la wana CCM kuhamia CHADEMA!
 
kabla huyu mzee mganga hajafa aliwah toa kauli Nzito na mbaya kwa taifa linalo amini uhuru wa watu kujitawala.
Kauli yenyewe"Mtu yoyote ambae atachukua form ya kugombea Uraisi na kushindana na aliepo ATAKUFA" Tena kwenye vyombo vya habari.
Je police mliwahi kumuhoji huyu mzee kwa kauli yake hyo.

Ikulu kupitia kurugenzi ya mawasiliano walisema ni Maoni yake kwanini hili tamko la NASSARI kuonekana baya zaidi?

Kama si kumpa umaarufu tu huyu dogo,Kauli za magufuli nazo huwa za uchochezi mbona hamjawah kumuhoji.
Mytake-kamateni wahujumu uchumi maneno hata kwenye kanga yapo.Nassari mtu mdogo sana katika nchi.Potezeni muda kulinda rasmali za watanzania

'Like' peke yake haitoshi. Ulistahili like moja na busu mbili kwa hili ulilolisema.

Tuko bize na maneno ya Nassari huku waliokwiba fedha wanaishia kuondolewa kazini tu.
 
Polisi wenyewe wote chadema hao, kwani unazani wanafurahia mshahara wanaoupata??? basi tu wanatamani sana siku moja CHICHIEMU ing'oke
 
Tatizo sio kauli ya Nassary wanaJF wenzangu bali ni UBUNGE wa Arumeru mashariki na Arusha mjini.

Hapo umenena kinawauma sana.dhambi ya ubaguzi inawatafuna.
Walisema ulimwengu si Mtz
Walisema Bashe si mtz
Walisema Wenje si mtz
Wakasema sumari si mtz
 
Kama CCM mpo humu na hamuoni madhara ya kufungua kesi hiyo nitawambia mkiamua kumshtaki.

Mumshauri huyo mkuu aachane na Maneno ya NASSARI Huyo hana hata Manati ndani kwake yeye analindwa na Mungu,

Na mkimfunga huyo alilolitamka litatimia na Ataongoza nchi hii.TANZANIA hakuna vikundi vya kigaidi. Maneno ni muhimu.
 
Hawa polisi wa CCM ni vihiyo wa maharifa na hekima. Mambo ya kijinga kwao ndio yanayopewa kipaumbele.

1. Didas Masaburi alisema wabunge wa DSM wamuache, kwani wakiendelea kuchonga mdomo na yeye atasema mabaya yao. Hii inadhihirisha kuwa kuna mabaya anayajua na hasemi ili ya kwake yasisemwe. (Black-mail = criminal offence). Sina hakika kama polisi wamelichunguza hili na kumhoji Masaburi

2. Maandamano ya wanaharakati ya kupinga DOWANS kulipwa yalipigwa marufuku kwa madai ya tishio la Al Shaabab. Kama ishu ilikuwa ni kuzuia mkusanyiko, je ni mkusanyiko upi ulikuwa wa hatari, wa Watanzania wanaojadili mambo yao au ule wa uwanja wa Taifa ambapo timu ya Kenya ilikuwa inashiriki michuano ya Challenge (weka akilini Kenya ina majeshi Somalia yakipigana na Al Shaabab)

3. Juzi mkutano wa CDM wa Same stand umezuiwa kwa madai polisi hawakupewa 48hrs notice. Yale maandamano ya kumpongeza JK yalitolewa 48hrs notice ikiwa yalifanyika asubuhi ya siku iliyofuatia tangazo la JK?

Tuna macho na tunaona. Tuna akili na tunatafakari, ole wenu siku yenu ikifika.

Kachunguzeni mchakato wa manunuzi ya RADA na TWIGA wetu waliouzwa Qatar na sio maneno ya siasa.

Kama mnaamini kunywa pombe na kuendesha gari ni makosa, gari ngapi zinapaki baa na kuondoka saa 5.30 usiku huku wamiliki wake wakiwa 'njwii', mbona tigo wasiende hapo kuwakamata mara tu wanapoingia kuyaendesha badala yake wako bize na kuandika fine za madereva waliosahau leseni zao nyumbani. Poh!
 
Mimi sioni sababu ya NASSAR KUOMBA msamaha kwa yoyote...Bob marley kuna nyimbo aliimba ndani yake kuna Sentensi hii"i am tired to see your face"
Nani katika nchi ya Tz Hajachoka kuona
Sura za viongozi wale
Sura za utawala uleule
Sura za mifumo zilezile
Hata mi nimechoka,Kauli ya NaSSARI HAIKUWA NA LENGO BAYA ZAIDI YA HAMASA ila kama angekuwa anahutubia Wanajeshi hapo sasa ndo kingejulikana cha kufanya,Nchi hii kuna kauli za kichochezi nyng na zngne zinatoka Chama tawala mbona hawakamatwi.
Police najua nafahamu mnatumikishwa tu ila mioyo yenu imechoka.
"kauli za kufa watu nchi zilitamkwa bt hakushkwa mtu"
Amini kile unachodhani kina manufaa kwa wengi si kwa wachache.
 
Tatizo sio kauli ya Nassary wanaJF wenzangu bali ni UBUNGE wa Arumeru mashariki na Arusha mjini.

Unachoongea kina ukweli kabisa, jeshi la polisi linatumika ili kudhoofisha upinzani...
 
kabla huyu mzee mganga hajafa aliwah toa kauli Nzito na mbaya kwa taifa linalo amini uhuru wa watu kujitawala.
Kauli yenyewe"Mtu yoyote ambae atachukua form ya kugombea Uraisi na kushindana na aliepo ATAKUFA" Tena kwenye vyombo vya habari.
Je police mliwahi kumuhoji huyu mzee kwa kauli yake hyo.

Ikulu kupitia kurugenzi ya mawasiliano walisema ni Maoni yake kwanini hili tamko la NASSARI kuonekana baya zaidi?

Kama si kumpa umaarufu tu huyu dogo,Kauli za magufuli nazo huwa za uchochezi mbona hamjawah kumuhoji.
Mytake-kamateni wahujumu uchumi maneno hata kwenye kanga yapo.Nassari mtu mdogo sana katika nchi.Potezeni muda kulinda rasmali za watanzania

Kwani hujui kuwa hii ni serikali ya masheikh na ustaadha?
 
badala ya kufuatilia rasilimali za nchi zinavyopotea na kusababisha wawe na maisha magumu, wao kazi yao ni kudili na cdm wanaongea nini?
 
Tatizo sio kauli ya Nassary wanaJF wenzangu bali ni UBUNGE wa Arumeru mashariki na Arusha mjini.

hiyo ni kweli..yani ni bora jimbo ccm wanalopigania likiwa ni la cdm then hata wakishindwa wanajua lilikua sio lao.. lakini arumeru mashariki lilikua ccm lile kwa hiyo kupoteza jimbo ambalo lilikua lako linauma...ni sawa na mtu akuchukulie mke wako..lazima umaindi
 
Hivi karibuni mbunge wa Arumeru Mashariki J. Nassari alikaririwa na vyombo vya habari akitoa matamshi fulani (yanayoonekana kama ya kichochezi) juu ya kanda ya kaskazini kujitenga na kumzuia raisi kufika/kuitembelea Arusha. Kauli hizo za Nassari kwa kiasi chake sio nzuri na wala hazipaswi kutamkwa na kiongozi yeyote na haswa haswa kutoka CHADEMA (kumbuka CHADEMA inahusishwa na ukanda).
Wengi wamejitokeza haswa hapa JF kumtetea Nassari huku wengine wakirefer kauli nyingine mbovu zilizowahi kutolewa na viongozi mbalimbali. Mi naamini kumtetea Nassari hatumsaidii wala hatumjengi kisiasa, jambo la msingi ni wote tukubali kuwa Nassari alikosea na kama tunampenda basi tumlazimishe aombe radhi na kufuta kauli na sio kumtetea wakati kosa lipo wazi na linaonekana kwa kila mtu.

Dogo janja atakua anajua kua ile kauli ni ya kichama filosofia isiyo rasmi kichama ambayo sisi watz wengine wa huku kusini, mgaharibi, na pwani hatuijui, au basi atakua limbukeni aka dongo jinga na atakua mbunge wa miaka 2 na nusu tu bungeni.
 
Back
Top Bottom