Kumekuwa na mauaji ya halaiki Msumbiji

Kumekuwa na mauaji ya halaiki Msumbiji

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
UN: Vijiji vinachomwa na watu wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa halaiki kaskazini mwa Msumbiji

Feb 08, 2020 12:57 UTC

Umoja wa Mataifa umesema, watu wanayakimbia makazi yao ili kujinusuru na wimbi la hujuma na mashambulio katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji ambako mashuhuda wamesema, raia wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa umati huku vijiji vya eneo hilo vikiteketezwa kwa moto.

Maafisa wa serikali wamesema, makundi yanayobeba silaha yameshadidisha hujuma na mashambulio yao katika mkoa huo, ambao umekuwa kitovu cha uasi unaofanywa kwa kutumia jina la Uislamu na ambao umepelekea mamia ya watu kuuawa tangu ulipoanzishwa mwaka 2017.

Eneo hilo la kaskazini mwa Msumbiji ni moja ya sehemu ambazo hivi karibuni zimegunduliwa kuwa na akiba kubwa zaidi ya gesi duniani, huku mashirika makubwa ya mafuta yakiwemo ya Exxon Mobil Corp na Total yakiwa yanaendesha shughuli zao.

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) amewanukuu wanavijiji waliobaki bila makazi wakisema, mauaji, ukataji viungo vya mwili, utesaji na uharibifu wa mazao ya kilimo umekuwa ukifanywa na makundi hayo yanayobeba silaha katika eneo hilo.

[https://media]Nyumba iliyochomwa na kuwalazimisha wakazi wake kukimbia ili kunusuru maisha yao

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva, Mahecic amesema, mashuhuda hao wamesimulia kuhusu raia, hasa wanaume, wanaoandamwa na kukatwa vichwa pamoja na matukio mengi ya wanawake na watoto wanaotekwa nyara au kutoweka kinyemela.

Msemaji huyo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi amebainisha kuwa, tangu ulipoanza mwaka huu wa 2020, mashambulio yasiyopungua 28 yamefanywa katika mkoa wa Cabo Delgado.

Kwa mujibu wa UNHCR, machafuko yaliyozuka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yamewalazimisha watu wasiopungua laki moja kuyahama makazi yao katika eneo hilo.../

4bv605309976301legc_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ww unavyoona raia wakipewa silaha hao magaidi pia hawatozipata!!!maana gaidi hajulikani kwa sura nae atajiingiza kwenye mgao apate silaha, pia raia watauana kwa visasi kwa kisingizio cha shutuma za ugaidi. hapo serikali ifikilie tu kupambana na hao watu kwa njia zengine.
Ina maana serikali ya Msumbiji imeshindwa kulinda raia wake dhidi ya hao magaidi?

Kama serikali imeshindwa kuwalinda ni vyema raia wapewe silaha ili wajilinde wenyewe.

Sio kila raia anapewa ila waunde vikundi maalumu vya ulinzi vitakavyosimamiwa kwa karibu na vyombo vya usalama.

Hivi vikundi vya kiraia vitakuwa viungo Kati ya vyombo vya usalama na raia wa kawaida wanaopatikana maeneo hayo.

Hivi vikundi vimesaidia Sana kule Nigeria kwenye Vita dhidi ya Boko haram (hasa kutoa taarifa za Siri) maana ilikuwa rahisi kuwatambua magaidi au wafuasi wao waliojichanganya na raia, mipango yao ya siri pamoja na maficho yao.
 
Fursa hii kwa sisi watu wa kusini, ngoja sasa nitafute connection na watu UN Moçambique.
 
Hii technic ya kuwapa silaha wananchi wajilinde wenyewe ilishawahi kufanikiwa kwny nchi gani boss?

dodge
Sio kila raia anapewa! ila waunde vikundi vya ulinzi vya kiraia ndio vipatiwe silaha (mfano Nigeria) kwenye kupambana na Boko haram.

Hivi vikundi viwe kama daraja kati ya vyombo vya usalama na raia wa hayo maeneo tena viwe chini ya uangalizi wa vyombo vya usalama.
 
UN: Vijiji vinachomwa na watu wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa halaiki kaskazini mwa Msumbiji

Feb 08, 2020 12:57 UTC

[https://media]

Umoja wa Mataifa umesema, watu wanayakimbia makazi yao ili kujinusuru na wimbi la hujuma na mashambulio katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji ambako mashuhuda wamesema, raia wanakatwa vichwa na kutekwa nyara kwa umati huku vijiji vya eneo hilo vikiteketezwa kwa moto.

Maafisa wa serikali wamesema, makundi yanayobeba silaha yameshadidisha hujuma na mashambulio yao katika mkoa huo, ambao umekuwa kitovu cha uasi unaofanywa kwa kutumia jina la Uislamu na ambao umepelekea mamia ya watu kuuawa tangu ulipoanzishwa mwaka 2017.

Eneo hilo la kaskazini mwa Msumbiji ni moja ya sehemu ambazo hivi karibuni zimegunduliwa kuwa na akiba kubwa zaidi ya gesi duniani, huku mashirika makubwa ya mafuta yakiwemo ya Exxon Mobil Corp na Total yakiwa yanaendesha shughuli zao.

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) amewanukuu wanavijiji waliobaki bila makazi wakisema, mauaji, ukataji viungo vya mwili, utesaji na uharibifu wa mazao ya kilimo umekuwa ukifanywa na makundi hayo yanayobeba silaha katika eneo hilo.

[https://media]Nyumba iliyochomwa na kuwalazimisha wakazi wake kukimbia ili kunusuru maisha yao

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva, Mahecic amesema, mashuhuda hao wamesimulia kuhusu raia, hasa wanaume, wanaoandamwa na kukatwa vichwa pamoja na matukio mengi ya wanawake na watoto wanaotekwa nyara au kutoweka kinyemela.

Msemaji huyo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi amebainisha kuwa, tangu ulipoanza mwaka huu wa 2020, mashambulio yasiyopungua 28 yamefanywa katika mkoa wa Cabo Delgado.

Kwa mujibu wa UNHCR, machafuko yaliyozuka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yamewalazimisha watu wasiopungua laki moja kuyahama makazi yao katika eneo hilo.../

View attachment 1351016

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii provicial ya Cabo delgado sitahisahau niliposhudia mapigano ya wanajeshi na hawa waaasi kwa takribani siku tatu nikiwa ndani

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ina maana serikali ya Msumbiji imeshindwa kulinda raia wake dhidi ya hao magaidi?

Kama serikali imeshindwa kuwalinda ni vyema raia wapewe silaha ili wajilinde wenyewe.

Mkuu hili swali ni sahihi kabisa nashangaa sana maana kuna kipindi waliomba msaada kutoka Tanzania but behind hii fujo ina mkono wa mtu huko huko kwao kujaribu ku disturb uchimbaji wa gasi na mafuta kwenye pwani ya eneo hilo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hii provicial ya Cabo delgado sitahisahau niliposhudia mapigano ya wanajeshi na hawa waaasi kwa takribani siku tatu nikiwa ndani

Sent from my iPhone using JamiiForums

Msumbiji wangali wanafuata HAKI ZA BINADAMU kwamba hata GAIDI ingawa ana bunduki lazima haki zake ziangaliwe kwa makini! Kitendo hicho kimesaidia magaidi kukua na kustawi vilivyo kwamba hata majeshi ya msumbiji hayawezi kukabiliana nao tena!
Wangemalizana nao mapema walipotoka Kibiti kwa kuwapelekea MOTO MKALI leo wasingeumia hivi .
Hii iwe mfano kwa TZ Tuache jpm afanye kazi angalau tubakie salama na familia zetu
 
Jamaa mnapenda kusifu na kuabudu kishenzi,sasa Jpm ameingiaje kwny maswala ya waasi?

Jifunzeni kubalance Shobo.

dodge
 
Sio kila raia anapewa ila waunde vikundi maalumu vya ulinzi vitakavyosimamiwa kwa karibu na vyombo vya usalama.

Hivi vikundi vya kiraia vitakuwa viungo Kati ya vyombo vya usalama na raia wa kawaida wanaopatikana maeneo hayo.

Hivi vikundi vimesaidia Sana kule Nigeria kwenye Vita dhidi ya Boko haram (hasa kutoa taarifa za Siri) maana ilikuwa rahisi kuwatambua magaidi au wafuasi wao waliojichanganya na raia, mipango yao ya siri pamoja na maficho yao.
Nchi ya Msumbiji inatakiwa idiploy jeshi tu huko kaskszini na mambo yatakaa Sawa.
 
Back
Top Bottom