Kumekucha Tanzania ya viwanda: China kujenga viwanda mkoa wa Simiyu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
China itajenga viwanda vya Nguo,Maziwa na Nyama mkoa wa Simiyu kwa kuwa mkoa huo una pamba nyingi na mifugo mingi inayowezesha viwanda hivyo kupata malighafi za kutosha kwa viwanda hivyo.HAPA KAZI TU.Tanzania itakuwa exporter wa nguo badala ya pamba

Source.Taarifa ya habari radio one
 
Angalia akili yako ilivyo ya kiwango cha chini!! Vinakuja viwanda nenda kalime pamba kafuge ng`ombe wa maziwa kwa uwingi Simiyu uwe unakiuzia kiwanda wewe vipi? Fursa zipo unalala akija mgeni unaota ukibarua tu.Mtu mzima hovyo!
Ni viwanda vya kuazalisha au ni vya processing tu Yaani wa-processing waondoke na cream yote sisi tubaki na mabaki na uchafu hahahahaaha, mbona najibu kwa hasira? Huu mchezo hautaki hasira aiseee
 
Tusubiri vijengwe kwanza isije ikawa kama ule wimbo wa kilimo kwanza kumbe deal za wananyinyiemu
 
Bora wakajenge tu labda zao la pamba litarudi tena sokoni, maana serikali mpaka sasa hata hawajafungua kununua hizo pamba
 
Angalia akili yako ilivyo ya kiwango cha chini!! Vinakuja viwanda nenda kalime pamba kafuge ng`ombe wa maziwa kwa uwingi Simiyu uwe unakiuzia kiwanda wewe vipi? Fursa zipo unalala akija mgeni unaota ukibarua tu.Mtu mzima hovyo!
Asante mkuu umemjibu vyema, huwa najiuliza watanzania wakati mwingi hua wanadai vitu bila kujua ni nini hasa wanataka. Tulitaka viwanda sasa vinakuja mtu analalamika kua kibarua but hajui ni manufaa gani atapata. Serikali haiwezi kuendesha viwanda peke yake kutokana na usimamizi mbovu na ukosefu wa maadili miongoni mwa watumishi wa umma. Watu wakiskia taifa lingine linakuja kuwekeza wanalalamika wakati wao hawajachukua hatua ya kuwekeza. Watanzania tunaongoza kwa kulalamika kuliko kuchukua hatua, nadhani ushabiki wa kisiasa pia unachangia hilo, kila kinachofanywa na upande wa pili kinaonekana kibaya kwa kuwa ni kutoka chama tofauti.
 
Ni viwanda vya kuazalisha au ni vya processing tu Yaani wa-processing waondoke na cream yote sisi tubaki na mabaki na uchafu hahahahaaha, mbona najibu kwa hasira? Huu mchezo hautaki hasira aiseee

Kiwanda ni kiwanda kiwe cha uzalishaji au processing.Swala ni kuwa ujio wa kiwanda unafungua fursa nyingi na kubadili maisha.Wataajiri watu waliokuwa hawana ajira,Nyumba za kupangisha zitapata wateja,maduka mengi yatafunguliwa na kupata wateja nk kiwanda kikiweko mahali hufungua fursa kibao.Ikiwemo mapato ya halmashauri na kodi kuongezeka.

Usikiangalie kiwanda tu kama kiwanda!!
 
Hahahahaha kweli hapa ndio tunapishana uelewa wa mambo, usiwe interested na viwanda kama viwanda uwe interested na viwanda kwa maana ya viwanda, vizalishe sis tu-export ready made materials au value added materials hapo ndio tutasema tuna viwanda. Sijui kama uelewa wako ukoje, aftermath ya viwanda ni kubwa sana kwahio lazima ukisema unaanzisha viwanda lazima view viwanda kweli kweli. Mshauri huyo jamaa yako kuwa tunataka viwanda sio "viwanda".
 
Ha ha ha ha ha umenikumbusha mbali mkuu eti kilimo kwanza! Hadi nimekumbuka mzee k.m.p.pinda
 
watu eti tunakuwa vibaria!! mlitakaje? kila jambo lina mwanzo mtakuwa mameneja kwa ujuzi wakujiongelesha hovyo na uvivu?
 
Angalia akili yako ilivyo ya kiwango cha chini!! Vinakuja viwanda nenda kalime pamba kafuge ng`ombe wa maziwa kwa uwingi Simiyu uwe unakiuzia kiwanda wewe vipi? Fursa zipo unalala akija mgeni unaota ukibarua tu.Mtu mzima hovyo!
Hao ndio tatizo katika Taifa
 
Back
Top Bottom