figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Hivi karibuni tumesikia taarifa kwamba makampuni ya siku yataorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na ningependa tuangalie aina hii ya uwekezaji. Tumesikia pia kwamba Klabu ya Simba itafanya marekebisho ya Katiba iwe Kampuni na kuanza kuuza hisa mashabiki.
Tufahamu kwanza Hisa ni nini? Hisa ni sehemu ya mtaji wa kampuni inayomilikiwa na wanahisa. Makampuni hugawanya mitaji yao katika vipande yenye thamani sawa ambapo kila kipande huitwa hisa na huuzwa kwa thamani fulani.
Mtu yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 anaweza kununua Hisa. Wazazi au walezi pia wanaweza kununua hisa kwa niaba ya watoto wao. Unaweza kununua kiasi chochote cha hisa kulingana na uwezo wako kifedha. Unaweza kununua kuanzia hisa 100 na kuendelea.
Mfano: Kama kampuni ina hisa 500,000 na mwekezaji anamiliki hisa 50,000, mwekezaji huyu anamiliki 5% ya kampuni hiyo.
Hizi ni baadhi ya Sifa za Hisa
• Hisa zina thamani
• Hisa zinaweza kukua au kupungua thamani
• Hisa ndio huunda mtaji wa kampuni
• Hisa zinaweza kufa pindi kampuni inapofilisika
• Hisa inamilikiwa kisheria kama sehemu ya mali anayoweza kuwa nayo mtu yeyote kihalali.
• Unaponunua hisa unakuwa na haki ya umiliki katika kampuni.
Nakaribisha maoni, unaionaje aina hii ya uwekezaji?