Naombeni ushauri kama ni sahihi
Nilikuwa na rafiki wangu wa kiume ambaye tuliachana zaidi ya mwaka mmoja uliopita. sasa wakati tukiwa kwenye mahusiano yeye alikuwa chuo anasoma ila alikuwa ameajiriwa na mimi nilikuwa nimeajiriwa. kwa kuwa tulikuwa na mipango mingi ya kimaisha nilikuwa mamshirikisha mipango yangu naye ananishirikisha ya kwake. kuna kipindi nikawa nimefunga biashara yangu na fedha ikawa ipo tu benki sasa akaniambia kwa kuwa hufanyi biashara kwa sasa nipe hiyo fedha niongezee kwenye biashara yangu then ukishafikiria biashara ya kufanya nitakupa fedha yako, mimi nikampa hiyo fedha. ila baada ya kumaliza chuo na kurudi kazini kwake mawasiliano nami yakaanza kupungua na baada ya muda tukawa tumeachana ila hakukuwa na sababu ya msingi ya yeye kuachana na mimi ila akaniambia usijali fedha yako nitakupa sitakurusha. baada ya hapo akanipa asilimia 75% ya hiyo fedha. nilipomuambia kiasi kilichobaki akawa hapokei simu na hata siku moja akampa mwanamke simu anitukane.nilipata maumivu sana sijui kama nilikosea kudai fedha yangu au nilitakiwa nisimdai kwani makubaliano yalikuwa nikibuni biashara anipe fedha. ushauri maana tangu nitukanwe sijampigia tena simu.
Dah umenikumbusha mbaliiiii, hilo ni kosa ambalo sitakuja kulifanya tena kwenye maisha yangu 'KUMKOPESHA PESA BOYFRIEND'!!!! . Hata wewe nakushauri usije kulifanya kosa la aina hiyo tena, MWIKOOOO!!!!. Nikirudi kwenye mada yako una haki zote za kumdai X-wako hela ulizomkopesha, kwa sababu mlikubaliana kwamba takurudishia. Tatizo linalokuja ni kwamba hakuna ushahidi wowote/ mtu aliyeshuhudia wakati ukimpa hizo hela, hivyo inakuwa ngumu. Sikulaumu kwa nn hamkuandikishiana, nafahamu mwanamke anapokuwa kwenye mapenzi huwa tunawaamini sana wapenzi wetu kwa kiwango ambacho utafikiri uko kwenye mahusiano na malaika kumbe ni MAGUMEGUME yetu haya yasiyojua kupendwa. Yaani hao watu hawana maana yoyote, unatakiwa uishi nao kama mgeni aliyekuja mara moja kesho anarudi kwake.
Ili uendelee kuwa na amani na kwa kuwa ameanza kuwatumia wanawake wakutukane anaonekana sio mstaarabu. Achana naye hautapungukiwa na kitu. Halafu Mwanaume anayejitambua huwa hakopi kwa girlfriend wake hata siku moja hapo umeingia kwenye choo cha shimo kilichajaa. Yaani siku hizi hakuna wanaume jamani, mpaka mnafikia hatua ya kutapeli vijisenti vya wanawake, Tumekwisha! teh teh teh.
Na jeje wewe hakuna anachokudai? Maana inawezekana anafanya hivyo kama compensation! Na hiyo 25% ni kiasi gani in shillings? Kama sio material kivile unaweza kuipotezea tu!.. akanipa asilimia 75% ya hiyo fedha. nilipomuambia kiasi kilichobaki akawa hapokei simu na hata siku moja akampa mwanamke simu anitukane..
Ungetushirikisha tangu mwanzo!
Na jeje wewe hakuna anachokudai? Maana inawezekana anafanya hivyo kama compensation! Na hiyo 25% ni kiasi gani in shillings? Kama sio material kivile unaweza kuipotezea tu!
hiyo 25 aliwekeza eeee not simple like thatNa jeje wewe hakuna anachokudai? Maana inawezekana anafanya hivyo kama compensation! Na hiyo 25% ni kiasi gani in shillings? Kama sio material kivile unaweza kuipotezea tu!
Na jeje wewe hakuna anachokudai? Maana inawezekana anafanya hivyo kama compensation! Na hiyo 25% ni kiasi gani in shillings? Kama sio material kivile unaweza kuipotezea tu!
I agree! Lakini si ni lazima kupima pia implications za yeye kudai? Isije kuwa mtu anataka "kuuza ngombe kugharamia kesi ya kuku"!hiyo 25 aliwekeza eeee not simple like that
Ungetushirikisha tangu mwanzo!