Kumbukumbu zisizofutika

Kumbukumbu zisizofutika

Banxbanxson

Senior Member
Joined
Oct 19, 2016
Posts
125
Reaction score
167
Habari ndugu na Jamaa,

Napenda kushare kwa wanajamii forums jinsi ya kunisaidia kusahau au kupata relief ya kumbukumbu ya rafiki yangu..

Hatukusoma pamoja shule ya msingi ingawaje tulitoka kijiji kimoja. Tulibahatika kwenda shule moja ya sekondari wakati huo. Tukawa marafiki wa kushibana kwa kila hali ingawaje sote tulitoka katika familia zenye dhiki. Maisha yetu yalitegemeana na kushare kidogo tulichoweza kupata kwa kufanya vibarua siku za weekend. Napenda kukiri kwamba tuliishi zaidi ya ndugu.

Baada ya kumaliza kidato cha nne Mm nilifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari na yeye alibahatika kujiunga na mafunzo ya jeshi la polisi na hatimae kuajiriwa. Wakati naingia chuo tayari alikuwa ameshapata ajira. Hakika alinisaidia masula yangu kadhaa wakati nikiwa chuoni.

Baada ya kumaliza chuo niliingia kupambana mtaani kutafuta ajira. Alinitia moyo na kunisapport kwa namna alivyoweza. Kwa waliotufahamu ukubwani walijua sisi ni ndugu wa kuzaliwa kwa kuwa mama yake alikuwa mama yangu pia.

Ghafla mwaka 2021 ndiyo kwanza nimepata ajira katika taasisi fulani na kuanza kufurahia maisha pamoja na ndugu yangu tukiwa na matumaini na malengo ya kufanya mambo mengi kwa pamoja, Nikapokea taarifa za kifo chake huko Dodoma bila ya kuugua. Hakuwahi kuwa na tatizo la shinikizo la damu ambalo kutokana na ripoti ya kitabibu ndiyo chanzo cha kifo chake.

Nikiri kuwa nimefiwa na watu wengi ikiwemo wazazi wangu na watu wengine wa karibu lakini kwa ndugu yangu huyu ni miaka zaidi 4 nimeshindwa kabisa kuamini au kukubali kuwa amefariki. Nimekuwa nikimuwaza kupita kiasi, ninaota tukiwa tunapiga stori mara kadhaa. Kuna wakati nikiwa nimekaa mwenye nashika simu yangu kwa lengo la kumpigia tuongee kisha nakumbuka kuwa hayupo duniani..

Hakika machungu ya kumpoteza Cheed bado yamejaa ndani ya kifua kwa kipindi chote hiki.

Labda ndugu na jamaa kutoka hapa kundini mnaweza kuwa na ushauri bora namna ya kuondokana na hili.
Hakika maisha bila ya kuwepo kwake yamenifanya kuwa mpweke sana licha ya kuwa nina Familia na watu wengine wanaonizunguka..

Mungu Ailaze mahali salama rafiki yangu Rashid.
Ahsante
 
mkuu tuji tahidi kuziishi kumbukumbu badala ya. Kuzi shikilia.

sawa tuli wapenda Sana, ila ndio hivyo hawapo. Jambo zuri ni kukumbuka na kuwa enzi mema yao tu.

Kila mtu ana kitu au mtu aliye kuwa attached nae Sana, ila turuhusu muda utuponye.
 
Pole sana mkuu

Watakuja wajuzi kukupa ushauri

Logan Michael_old friend🎧
Tafuta wimbo huo unaendana na ulichokiandika hapo
 
Pole sana kiongozi kwa kumpoteza Rafiki yako, hii hali ni ngumu sana hata mimi nilipitia.
My friend ananitokea hadi ndotoni, sometime I feel its real.
I lost a good friend and a brother.

Kuna marafiki wazuri kuliko ndugu.

Time heals Brother
 
Kwa muda uliopita nilitarajia kuwa ningekuwa nimezoea, Actually hata nikijaribu kupotezea na kukubaliana na ukweli bado inaniwia vigumu.
Kadidri ninavyofanya juhudi kusahau ndivyo uchungu hunikamata na kujikuta nikitokwa na machozi.
 
mkuu tuji tahidi kuziishi kumbukumbu badala ya. Kuzi shikilia.

sawa tuli wapenda Sana, ila ndio hivyo hawapo. Jambo zuri ni kukumbuka na kuwa enzi mema yao tu.

Kila mtu ana kitu au mtu aliye kuwa attached nae Sana, ila turuhusu muda utuponye.
Ahsante sana,, Ninajitahidi kuliondoa hili akilini kwangu na kila siku nahisi ndivyo ugumu unaongezeka
 
Habari ndugu na Jamaa,

Napenda kushare kwa wanajamii forums jinsi ya kunisaidia kusahau au kupata relief ya kumbukumbu ya rafiki yangu..

Hatukusoma pamoja shule ya msingi ingawaje tulitoka kijiji kimoja. Tulibahatika kwenda shule moja ya sekondari wakati huo. Tukawa marafiki wa kushibana kwa kila hali ingawaje sote tulitoka katika familia zenye dhiki. Maisha yetu yalitegemeana na kushare kidogo tulichoweza kupata kwa kufanya vibarua siku za weekend. Napenda kukiri kwamba tuliishi zaidi ya ndugu.

Baada ya kumaliza kidato cha nne Mm nilifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari na yeye alibahatika kujiunga na mafunzo ya jeshi la polisi na hatimae kuajiriwa. Wakati naingia chuo tayari alikuwa ameshapata ajira. Hakika alinisaidia masula yangu kadhaa wakati nikiwa chuoni.

Baada ya kumaliza chuo niliingia kupambana mtaani kutafuta ajira. Alinitia moyo na kunisapport kwa namna alivyoweza. Kwa waliotufahamu ukubwani walijua sisi ni ndugu wa kuzaliwa kwa kuwa mama yake alikuwa mama yangu pia.

Ghafla mwaka 2021 ndiyo kwanza nimepata ajira katika taasisi fulani na kuanza kufurahia maisha pamoja na ndugu yangu tukiwa na matumaini na malengo ya kufanya mambo mengi kwa pamoja, Nikapokea taarifa za kifo chake huko Dodoma bila ya kuugua. Hakuwahi kuwa na tatizo la shinikizo la damu ambalo kutokana na ripoti ya kitabibu ndiyo chanzo cha kifo chake.

Nikiri kuwa nimefiwa na watu wengi ikiwemo wazazi wangu na watu wengine wa karibu lakini kwa ndugu yangu huyu ni miaka zaidi 4 nimeshindwa kabisa kuamini au kukubali kuwa amefariki. Nimekuwa nikimuwaza kupita kiasi, ninaota tukiwa tunapiga stori mara kadhaa. Kuna wakati nikiwa nimekaa mwenye nashika simu yangu kwa lengo la kumpigia tuongee kisha nakumbuka kuwa hayupo duniani..

Hakika machungu ya kumpoteza Cheed bado yamejaa ndani ya kifua kwa kipindi chote hiki.

Labda ndugu na jamaa kutoka hapa kundini mnaweza kuwa na ushauri bora namna ya kuondokana na hili.
Hakika maisha bila ya kuwepo kwake yamenifanya kuwa mpweke sana licha ya kuwa nina Familia na watu wengine wanaonizunguka..

Mungu Ailaze mahali salama rafiki yangu Rashid.
Ahsante
Pole sana. Wala huna haja ya kumsahau. Vyema ukimkumbuka upate kuziishi kumbukumbu zake nzuri. Km kuna fundisho lolote kakuachia ishi nalo.
Kama wewe ni wa imani ya dini basi endelea kumuombea dua na kumtolea sadaka. Na utapojaaliwa kupata baby boy usiache kumwita jina lake ili kuzidi kumuenzi
 
Back
Top Bottom