Kumbukumbu yangu ya Sheikh Ilunga Tanga na Geneva

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,249

1575579542236.png

Sheikh Ilunga akiendesha darsa Thakafa Mwanza 2010
Sheikh Ilunga alikuja Tanga katika miaka ya katika ya 2000 na alikuwa anafanya mihadhara yake katika msikiti mmoja mdogo kwani viongozi wa misikiti mikubwa walikuwa na hofu kwa hiyo waliogopa kumwalika kuzungumza katika misikiti yao.

Nilikuwapo siku ya kwanza katika mhadhara wake wa mwanzo mjini Tanga na alikuwa anazungumza baada ya Sala ya Isha.

Ghafla baada ya Sala ya Isha nikiwa ndani naona watu wakiingia kwa wingi haukupita muda msikiti ule mdogo ukawa umejaa pomoni na watu wengine wamejazana nje ya msikiti hadi barabarani wengine wanachungulia madirishani.

Ikabidi Sheikh Ilunga aombwe asubiri kuanza kuzungumza ili kuwapa nafasi Waislam wanaotoka misikiti ya mbali wafike na ikabidi ziwekwe taa za kutosha nje ya msikiti.

Waislam walikuwa wanampenda Sheikh Ilunga na wanaelewa ujumbe aliokuwa anawafikishia.

Mwaka wa wa 2011 nilikuwa Geneva Switzerland kijana mmoja akanialika nyumbani kwake.

Kijana huyu baada ya kusalimiana na kutulia akaniuliza endapo kama namjua Sheikh Ilunga.

Akanyanyuka alipokaa akaweka DVD ya Iliunga na kuniomba nimwangalie.

Nimeweka picha ya Geneva ya jioni ile.

Picha ya tatu inaonyesha sura ya Sheikh Ilunga katika screen ya TV na mimi nikiwa pembeni.

Hii ni picha nilipiga nyumbani kwa kijana yule siku ile nikiwa mbali sana na Tanzania.

Nilimuomba mwenyeji wa anipige picha ili nichukue kumbukumbuka ya Sheikh Ilunga nikiwa Geneva.

Wakati ule sikujua kama nitakuja kuikumbuka picha hii na nitaiweka kama kumbukumbu baada ya kifo chake.

1575579701218.png

Sheikh Ilunga


 
Mohamed Said, maandiko yako yote ni kuhusu uislam,
Luta...
Naam takriban yote ni kuhusu historia ya Waislam Tanzania tofauti ni maudhui.

Kuna makala na vitabu kuhusu mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni wa Wajerumani na Waingereza.

Hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kuna mada zinazojadili matatizo ya Waislam katika kupata elimu ya juu katika Tanzania huru.

Kuna mada za Uislam na Ugaidi.
Ungependa kujua kwa nini?
 
Yaani Title tu ya kitabu unafanya typing error, sasa humo ndani umeandikaje KUULINGANIA ndiyo mnyama gani,, huwa unajipamba unaandika kwenye international publishing Agent, mambo madogo kama haya yanakufanya uwe mwepesi kwenye hoja zako zenye makengeza,,,,,,,,
tapatalk_1575646303934.jpeg
 
Yaani Title tu ya kitabu unafanya typing error, sasa humo ndani umeandikaje KUULINGANIA ndiyo mnyama gani,, huwa unajipamba unaandika kwenye international publishing Agent, mambo madogo kama haya yanakufanya uwe mwepesi kwenye hoja zako zenye makengeza,,,,,,,,View attachment 1283869
Hamna kosa kama unavyodhani wewe. Kiswahili cha pwani naona hukijui. Mwandishi ni watu wenye uelewa mkubwa kwenye lugha ya kiswahili.
 
Yaani Title tu ya kitabu unafanya typing error, sasa humo ndani umeandikaje KUULINGANIA ndiyo mnyama gani,, huwa unajipamba unaandika kwenye international publishing Agent, mambo madogo kama haya yanakufanya uwe mwepesi kwenye hoja zako zenye makengeza,,,,,,,,View attachment 1283869
Dogo...
Tujaalie nimekosea.

Ilikuwa wewe kunifahamisha kuwa nimefanya makosa nami ikiwa kweli nimekosea nakushukuru na nafanya masahihisho.

Bahati mbaya umeandika kwa nia ya kunifedhehesha.

Lakini mimi sijafanya kosa lolote hivyo ndivyo nisemavyo na ndivyo niandikavyo.

Nimeangalia uandishi wako.
Pitia tena taratibu.

Wala mimi sitakunanga kwani kukosea ni silka yetu wanadamu.

Aliye mkamilifu ni Allah SW.
 
Mwenyezi Mungu Subhana wataalah amrehemu Sheakh Ilunga.. Niliposikia amefariki nilitamani kuja kumzika lkn nikichelewa kufika Dar.. Alizikwa Dar alisaliwa sala yake ya mwisho Msikiti wa kichangani ba kuzikwa nafikili makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni..
 
Yaani Title tu ya kitabu unafanya typing error, sasa humo ndani umeandikaje KUULINGANIA ndiyo mnyama gani,, huwa unajipamba unaandika kwenye international publishing Agent, mambo madogo kama haya yanakufanya uwe mwepesi kwenye hoja zako zenye makengeza,,,,,,,,View attachment 1283869
KUULINGANIA ni typing error ?
Kha, acha bangi, unaonekana huelewi maana ya neno typing error, tukutane jukwaa la lugha tukufunze.
Unakua mshamba hata kwa lugha yako
 
KUULINGANIA ni typing error ?
Kha, acha bangi, unaonekana huelewi maana ya neno typing error, tukutane jukwaa la laugha tukufunze.
Unakua mshamba hata kwa lugha yako
Sheikh Idd,
Umefanya ukali.

Jambo ukilitia upole linapendeza.

Ungemjibu kwa taratibu kumwelewesha sisi watu wa pwani vipi lugha yetu ilivyo huwa inapishana na wengine mara nyingi sana.
 
Back
Top Bottom