Ukitafakari kwa makini mienendo, kauli na maandiko ya viongozi wa chama cha TANU unaweza kwa kiasi kikubwa kujenga picha ya Taifa walilokuwa wanadhamiria kujenga. Ni vigumu kuamini chama hiki cha TANU, kilichopigania uhuru wa Tanganyika, na wana wa Afrika na utu wa mwanadamu bila ya kujali rangi, kabisa au jinsia kime-evolve na kufikia mahali mweka hazina wake anakuwa Rostam Azizi! Naomba nieleweke, hapa siongelei mtu, naongelea leadership & ethics na kwangu mimi hatua ya kumpa DHAMANA ya uweka-hazina Ndugu Rostam ni 'symbol' ya collective thinking ndani ya chama juu Taifa wanalotaka kujenga!
Natambua wakubwa wa ccm na hata wengi wa wanachama wa ccm wanajiandaa kupaza sauti za kusherehekea kuzaliwa kwa TANU, lakini nina uhakika wengi wao kama sio wote dhamira zao zitakuwa zinawahoji uhisiano wa ccm na TANU na kwa vipi wanajiona wao ndio watoto halali (legitimate child) wa TANU.. and what do they know about TANU?
Kwa maoni yangu, TANU inaweza kuwa na mahusiano ya karibu sana na mamilioni ya Watanzania-walalahoi, waliopigika kimaisha, wauza vebiriti barabarani, mama ntilie, wamachinga wanaopigwa na polisi kila kukicha, lakini TANU haiwezi kuwa na uhusiano na CCM ya sasa. Na ninaweza kusema the current ccm is a 'group of imposters' wasiokuwa na mishipa ya aibu wanapita barabarani mchana kweupe wakidanganya umma kuwa mzazi wao ni TANU.