Kumbukumbu isiyo futika milele

Kumbukumbu isiyo futika milele

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,647
Reaction score
4,495
February :
Huu ndio mwezi bora na wenye mizizi yote ihusuyo historia ya maisha yangu.. Nilizaliwa 14th February .. Mwezi ambao inasadikika walizaliwa watu wenye IQ ya khali ya juu mno chini ya mbingu.. Watu wenye taranta ya kuweza kuandika na kujieleza ipasavyo mbele ya uso wa dunia...Ushahidi ni Mtunzi wa NOVEL YA MONEY IS THE SOURCE OF ALL EVILS UNDER THE SUN..
(Pesa ndiyo chanzo cha maovu yote chini ya jua. ) PROFESSOR ELVIS GRAYSON WA HARVARD UNIVERSITY. ''

Pia ushahidi mwingne kuwa February ni zao la watu wanaoweza kucheza mpira mf: Cristiano na Neymar.. Na rafiki yangu aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma.. Utafiti unaonyesha watu waliozaliwa February.. Wana Authority voice na higher convincing power.. Yaani
(wana sauti ya mamlaka na ushawishi wa khali ya juu mno chini ya mbingu. '')..

kwa wanajimu waliobobea Kwenye kusoma nyota na kufanya analysis za matukio ya kale..Wanasema hata YESU KRISTO alizaliwa February... naweza kuamini sababu biblia hakuna sehemu ilipotaja mwezi aliozaliwa Yesu Kristo.. Sijawahi kuichukia February ktk maisha yangu .''

April :
Huu ni mwezi ambao uliwahi kunipa Furaha hisiyo simulika.. Na baadaye ukanipokonya Furaha hiyo, nakuniachia huzuni ya milele.. Na Majuto makubwa kupita umbile la hayati GORIATI.. Na baadaye ukatengeneza uadui na chuki ya kudumu na ubongo wangu..

Mwanamke niliyewahi kuamin atakuwa mama bora wa watoto wangu siku moja .. Mara ya kwanza nilimuona Tarehe 4th April.. Baada ya kumfuatilia kwa miaka 3 mfululizo.. Siku aliyonitamkia ameridhia kuwa na mimi.. Ilikuwa Juma tano, mchana wa saa sita na dakika 3 Tarehe 7 April...

Nakumbuka sikula siku nzima.., kwa Furaha iliyokuwa imejimilikisha himaya ndani ya moyo wangu.. Natarehe 29 hiyo hiyo April.. Akanipa dhamana ya kuwa mwanaume wake wa Kwanza maishani.. '' Hapa mwezi April ulinitendea haki na ulinijengea heshima ya milele kwa binti yule.''

Baada ya mapenzi kudumu miaka mi4.. Na alipomaliza kidato cha sita uku majibu yakiwa yametoka na amefaulu.. Bahati mbaya tukapeana mimba.. Na maamuzi ya mwisho toka Kwenye ubongo wake ikawa tuiangamize damu hisiyo na hatia.. Kweli tukafanya hivyo..kitendo nachojutia hadi hii Leo... YULE MSHENZI BAZAZI AKAFANYA NIUE MIYE .. MORA NIWIE RADHI ILE DAMU ISINILILE.

Baadaye alienda chuo,.. Taratibu moyo wake ukaanza kuyanyausha mapenzi yake kwangu. Na baada ya mwaka kupita. Nikaja kusikia yupo Kwenye mahusiano na mwanaume mwingine.. Hizi habari zilifanya niitamani mauti, ili kuyazika maumivu yaliyokuwa yamejenga ngome ndani ya moyo wangu.. Habari nilizipata mwezi April.. Kuanzia pale hadi Leo ubongo wangu ukatengeneza chuki ya milele na mwezi April. ''. NAICHUKIA April. ''

September :
Nashindwa kuielezea ipasavyo September. Lakini huu ndio mwezi ambao uliitimisha hadithi nzuri ya maisha ya WILIFRED KIRUMBUYO .. Ambaye alikuwa ni baba yangu mzazi... September ndio aliipa dunia mkono wa kwaheri.. Mauti ikampa ticket ya kulala ndani ya mbao ziitwazo Jeneza.. Na kisha wanadamu wakamfukia ndani ya shimo liitwalo kaburi...

Akaniacha uku nikiwa bado nayahitaji mapenzi na malezi yake... Zaidi ya mtu mwenye kiu ayahitajiye maji jangwani. ''.. Mungu amlaze pema peponi baba yangu. September HUWA INANIKUMBUSHA KUTENDA MEMA,,, MAANA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.''
 
Back
Top Bottom