Kumbukizi: Unakumbuka wapi ukiona hii?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Habarini za Hapa

Kwa upande wangu nakumbuka Mbali Sana Enzi hizo kuna Jidada kaniandikia barua wakati ananipa alisema usimwambie Mama ako lakini! Nikapokea kabla sijafungua ilikuwa imeandikwa kiss before open Niliyo yakuta humo ni Makopa Kopa na Dedication kama Vailet by Matonya, Milele by Ray C,Cinderella by Ali kiba na vimichoro kibaoo

Enzi hizo mambo ya Simu Yalikuwa Bado sana, Unakuta Barua inaanza na Apple la barua hii,Lengo la barua hii,Dhumuni la Barua hii na mengine mengi

Wewe Unakumbuka Wapii Ukiona Hii barua

Adjustments.JPG
 
Teknolojia imekuja kuharibu utamu wa mahusiano.

Nakumbuka wakati nipo kidato cha nne nilikuwa nakodisha barua za mapenzi, unampelekea demu anasoma kisha unaichukua na kuipeleka sehemu nyingine.

Zilikuwa barua za kiwango na kama huoni vizuri utasema imechapwa kwa kompyuta.
 
mimi na mwanangu tuliokota barua ya dada mkuu,aisee tuliishi kama wafalme,tuliitumia ile barua kumuendesha tunavyotaka sisi yule dada,hatukuw tukifanya kazi shule na alituletea tulichokitaka...melisa ***** nakukumbukaga sana
 
Nimeandika barua kwa juliet hapo niko stnd 4 halaf nikaisahau mfukoni.Ilikua ijumaa na nikapata safar ya kikanisa kwahiyo mama akawa na jukum la kutufulia nguo kwakua sipo ili jumatatu ziwe safi.Dooh nilikoma nilivyorud,... nilikula bakora za kutosha sana maana maza aliifuma ile barua ...
 
mimi na mwanangu tuliokota barua ya dada mkuu,aisee tuliishi kama wafalme,tuliitumia ile barua kumuendesha tunavyotaka sisi yule dada,hatukuw tukifanya kazi shule na alituletea tulichokitaka...melisa ***** nakukumbukaga sana
Hoply melisa lwitiko.
 
Nimeandika barua kwa juliet hapo niko stnd 4 halaf nikaisahau mfukoni.Ilikua ijumaa na nikapata safar ya kikanisa kwahiyo mama akawa na jukum la kutulia nguo kwakua sipo ili jumatatu ziwe safik.Dooh nilikoma nilivyorud nilikua bakora kutosha sana maana maza kaifuma barua ...

 
Mbali sana,maisha yanakwenda kasi sana. Niliwahi kuandika barua kwa mwangaza wa mbalamwezi,nikampa mdogo mtu usiku usiku. Nyege hazina adabu.
 
dah umetukumbusha mbali mkuu, niliwahah andikiwa barua na kabint nikiwa darasa la5, wimbo ule wa mr nice "kila ndege hutua mti aupendao, krb geto nikupe mambo ya mwambao" dah esta popote ulipo pitia huku
 
Dah mapenzi ya zamani jaman tulikuwa tunatongozwa vizuri adi raha....nakumbuka tuko shule ule muda wa Prep's ukikaribia kuisha usiku unaandaa unampa shem anapeleka fasta class kwao naye anarudi na ya kwako kutoka kwake yaan wee M.....nakukumbuka na mwandiko wako mahondaw manengelo Khantwe sjui mnakumbuka izi barua
 
Miaka hiyo mm nilikuwa bado USA so sikufanikiwa kuandika wla kupokea barua Kama hizo nilivyorudi zishapitwa na wakat
 
Nimekumbuka mbali aisee..vikopa kopa vya stika Mara virose..

Mwisho anamalizia "nataka kuwa na wewe Kama rayc"
Vichombezo kibaoo..
 
Mwanangu mmoja ndio alikua ananiandikia hizo barua zangu maana mimi limuandiko langu la kizembe lilikua

ukishapewa barua yako unaificha kati kati ya daftari,sasa siku moja nina mawenge nimekusanya daftari ndani lina barua

na madftari monitor kashayachukua kayapeleka staff yapo mezani yanasubiriwa kusahishwa,aseeeeeee ile siku nilikaa shule mpk watu wakanishangaaa, school bus imekuja nimeenda jificha toilet gari ikaondoka nikaachwa Hapo nipo natafuta taiming niingie ofisini nikachukue daftari langu nitoe ile barua.

wakati naranda randa shule mlinzi akaniona akaniita "wewe kuja huku" akaanza nitwanga maswali kwann sijaenda nyumbani,nikamdanganya nipo tuition akaniachia.

kuhangaika kote huko sikufanikiwa pata upenyo wa kuingia staff,matokeo yake kesho yake class niligeuka mfano kwa wanafunzi wote na kesi yangu ilifika hadi school baraza nlikomaga mimi jamani, barua hizi pputtuuuuuuu
 
Ushimen,
Hahaha! Mukubwa wakati umepita kweli facebook na vilongalonga vimeuzima mchezo huu.........Kuna ile unanunua daftari kwaajili ya kubandinga love song za magazetini hapo big G lazma iwe gundi.
 
Kuna jamaa yangu alikua na good hand writing so nikawa namtumia yeye aniandikie then nampa ela ampelekee mtoto hio barua, kumbe wote madomo zege viwango vya fly over yule mpuuzi ela zangu anakula na barua hapeleki lakini akija kwangu ananipanga basi nafurahi mwenyewe kumbe demu hajui chochote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom