Kumbuken haya wapendwa dada zangu.........

Kumbuken haya wapendwa dada zangu.........

Mapigo1

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
256
Reaction score
90
Kumbukeni haya wapendwa dada
zangu
1} Kamwe usimtegemee mpenzi wako
wa kiume kama baba yako, jaribu
kumwonyesha ajue kuwa kabla ya
kukutana ulikuwa unajiweza na hata
ukiachana nae utaendelea kujiweza.
2} Usimkane mpenzi wako kwa kuwa
yeye ni masikini sasa, kwani tajiri wa
leo ni masikini wa kesho na mtu
hawezi kuwa fukara maisha yake
yote, Utajiri ni sawa na vitambaa vya
meza vinabadilishwa kila siku
3} Usiseme kuwa hakuna wanaume
wa ukweli katika maisha yako wakati
wewe kila kitu kwako ni feki,
Kumbuka utampaka mtu kulingana
na wewe ulivyo na maisha yako,
ukiwa feki utakutana na feki
mwenzako... kuwa real
4} Usiseme wanaume wanautaka
mwili wako tuu wakati mavazi yako
yanauonyesha mwili wako kila
sehemu zikiwa wazi. Jinsi unavyo vaa
ndio watu wanavyo kuthaminisha na
kukulinganisha na tabia zako.
5} Usilalamike kuwa umekaa nae
kwenye mahusiano kwa muda mrefu
lakini bado hataki kuyafanya
mahusiano yafungue ukurasa mpya
wa kuwa mme na mke, Dada yangu
sio kila mahusiano ni lazima yaishie
kwenye ndoa.
6} Usiseme wanaume wote wako
sawa baada ya kuumizwa, Kumbuka
hata vitabu vya dini
vinasema: kama ambavyo nyuso zetu
zatofautiana ndivyo hata tabia zetu
zinavyotofautiana.
7} Usiyachukie mahusiano kwa
kutokana na kumbukumbu zilizopita,
zaidi kumbuka kila
mahusiano yana funzo la kukupa, na
usifunge macho kwa kuogopa kuona
mambo magumu kwani unaweza kuja
kufumbua macho na
kugundua kuna mazuri yalipita na
bila wewe kuona... Usikate tamaa
katika mapenzi
8} Usikimbilie katika kuolewa kwani
kama Mungu ajuavyo siku yako ya
kuzaliwa na ya kufa hivyo hivyo
anafahamu kila mipango juu
yako kwani sisi ni kama sisimizi
machoni mwake, Muda wako wa
kuolewa utafika kwa wakati kama
ilivyo kwa kifo kinavyokuja bila
hodi.
9} Unasema wanaume hawako siriazi
na wewe, wakati historia yako na
matukio yako ya nyuma
yako kwenye vyumba vya hotel, simu
za wanaume mabali mbali na hapa
facebook una marafiki 5000 na kila
picha yako inaonyesha
jinsi ulivyo na wasifu mbaya, kila
gari wewe umefanya gesti na pia kila
mtandao upo na una wanaume
wengi wengi umejianika vya kutosha,
Kitu ambacho kinauonyesha umma
kuwa umeathirka kifikra na msimamo
10} Kila siku mbukuka mambo
yanatokea vile Mungu atakavyo....
 
Na nyie muwe real maana mko feki feki tu wanaume
 
Ukitaka feki utapata feki ukitaka real man utapata real man xo Kaz ni kwako mdada

e730bd637bb12dc6c6b60551b97ae72bedc5bebe7371aaceb11d98d6da2c546c.jpg
 
Naona mnaanza kuvaliana vibwebwe...
 
Bahati mbaya wengi wao hutawaona katika sredi hii...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom