Kumbe Zitto Kabwe alishapokea ‘’mlungura’’ wa Barrick Gold, tutapona kama Taifa?

Bora yeye kaomba kujengewa shule,serikali & CCM iliomba kuingiziwa 'mlungura' katika akaunti za 'walafi' wake. Pathetic...
 
Unapotuhumu kampuni and then kampuni inakuziba mdomo kwa kukujengea shule what do you expect.
Kwenye zilizoendelea hiyo ni scandal kubwa Zitto angejiuzulu haraka.
Tutegemee mengi kutoka Barrick hawawezi kukubali aibu hii iwe yao watasema mengi.
Kwa sasa nimekuelewa vizuri.
 
Nadhani TAKUKURU itakuwa wameiona hii na wanaifanyia kazi. Lazima Zitto aunganishwe na akina Chenge, Dalali, Karamangi na Mwanyika kwenye sakata hili la mchanga. Yaanj huu mchanga utaenda na wengi na haujali itikadi ya chama cha siasa. Masikini Zitto anaishia pabaya katika harakati zake za kisiasa.
 
MsemajiUkweli Unatakiwa Utambue kuwa kwa sera za nchi hii, adui wa taifa ni adui wa kila mtanzanania na vivyo hivyo kwa kinyume chake.

Zitto kabwe alipambana kadiri ya alivyoweza, lakini alishindwa kuwafanya lolote kwani walikuwa wanakingiwa kifua na serikali, na hapa ndipo usemi usemao "IF YOU CAN'T BEAT THEM, JOIN THEM" (Kama huwezi pambana nao, basi ungana nao). ZZK hakupenda kufanya hayo unayotaka kutuaminisha, bali mfumo mzima ulikuwa haupo upande wake na ulimlazimisha kufanya na kutenda kinyume na maono na misimamo yake.
Mkuu MANDELAA KIWELU

Kumbuka two wrongs don't make a right.

Mwanasiasa makini lazima awe na principle zinazokubalika na jamii kubwa na katika principle hizo lazima aziishi.
 
Hayo ndio mambo na kazi ya INED (Independent Non-Executive Director)niliyoyaeleza jana kwenye uzi huu Sakata la Makinikia: Balozi Juma Mwapachu anajiondoaje ktk "lawama za kuingamiza" Tz kwa wawekezaji?

INED anarafuta "fox MPs" anapeleka orodha kwenye kampuni ya kibeberu,wanatengewa miradi ya maendeleo kwenye majimbo yao,then wanatulizwa kama maji ya mtungi....Makinikia hayajawahi kumuacha mtu salama
Nimeisoma thread yako na kama kawaida inafikirisha na kutoa somo pana kwa watu wenye fikra pana.

Serikali inatakiwa ijipange vizuri katika kukabiliana na ujanja na vituko vya makampuni yanayotoka nchi za Magharibi.
 
Hii taarifa ukiisoma, unaona kwa dhahiri ni jinsi gani maliasili zinaibwa na kuwanufaisha wawekezaji kuliko hii nchi.
Yaani unaona jinsi wanavyotuchukulia kama watoto vile.
Angalau Zitto kawezesha hii kampuni kutoa vifaa vya kukarabati shule moja. Na kwa kebehi kabisa, imeandikwa hapo ni 'low cost' msaada kwa elimu ya jimbo, kwani hutoa viji misaada vidogo vidogo, kwa kebehi wanaviita 'miscellaneous', wakitolea mfano art workshop, yaani maonesho ya sanaa kwa watoto wa mitaani wa Dar! Haya maonesho yanagharimu kiasi gani, kama sio milioni moja? Maana ni kuwa na rangi mbali mbali na makaratasi, watoto wakachora picha zao, yakabandikwa ukutani, picha zikapigwa, basi siku imekwisha, tuonane tena mwakani.
Hii taarifa ni ya mwanafunzi wa chuo kikuu huko Canada, akiwaonesha jinsi tulivyo wajinga. Zitto atalaumiwa kwa kupewa vifaa, sio hela za kuingizwa katika akaunti yake, na iko wazi kiasi kwamba leo tunaizungumzia, je walioenda kutia sahihi huko huko, na tena wamerudi, hawakusema kama wamesaini mkataba, wanaulizwa wakakana, mpaka baadae ndio wanakubali na hata kuuonesha mkataba ilikuwa ni kwa mbinde, wameingiziwa kiasi gani katika akaunti zao? Aliyeandika hii taarifa, kaandika kwa kuwa hata hao Barrick, wameutaja msaada kwa Zitto kwa kuwa si rushwa, na wanajionesha kuwa wanasaidia jamii. Je hakuna zilizotolewa kwa kificho ikiwa ni rushwa rasmi kwenda iwe ni kwa Zitto au mtu mwingine yeyote?
 
Mwanasiasa pekee ninayemuamini ni JPM.....anahukumu kwa haki...na haki unaiona.
 
Madini yote ya Tanzania yanachukuliwa kifisadi Tanzania kwa sheria na mikataba mibovu. Na karibu wabunge wote Tanzania (zaidi ya asilimia 70) wote upinzani na CCM wamejengewa miundombinu mbalimbali na hao matapeli wa madini. So tukihoji sana ya Zitto tunaweza fanya uchunguzi na kubaini kwamba wako wengi hata wa CDM au CCM ambao majimboni kwao ni the same. Kwanza kujengewa shule haikuwa zawadi bali ulikuwa ni wajibu wao wa kushiriki katika marndeleo kwenye jamii iko kwa mujibu wa sheria, Zitto aliwakumbusha wajibu wao.
 
Kumbe ndiyo maana alikimbia lile jimbo na kwenda kugombea jimbo lingine ili kukwepa kashifa
 
akili za wabongo bana sasa hivi wamewageukia wapinzani utazani ndio wali sign mikataba mibovu, hii nchi kwa jinsi inavyokwenda kama tusipobadilika hata miaka 100 tutakuwa hivi hivi hata kama tutakuwa na maliasili kuliko nchi yoyote duniani, wananchi wajinga, viongozi wabunafsi, wachache wanaopigania maslai ya nchi ndio wanaonekana wasaliti wa nchi,
 
Zito alipewa cheki kwa ajili ya kujenga/kukarabati shule kwenye jimbo lake. Swali la kujiuliza ni je, shule husika ilijengwa/ilikarabatiwa? Imaitwaje? Kamati ya shule hiyo ina taarifa zozote kuhusiana na msaada huo, na ilishirikije kufanikisha hilo - kuanzia maandalizi ya proposal hadi kutekeleza mradi na kufanya tathmini yake?
 
Wakuu, mwenye fursa ingia kwenye website ya TRA nenda sehemu iliyoandikwa Library then chagua decided tax cases ....pale fungua TRA V African Barrick Gold mine PLC ( Appeal No. 128 of 2013 dated 9th July 2015) ....ni very interesting case hasa kwa hili linaloendelea ....tumuunge mkono Rais wetu kwa nguvu zote ....inatosha kuibiwa ....
CC MsemajiUkweli
 
Mzee Warioba jana alishauri tuache ya nyuma tuangalie mikataba mipya.
Ukiangalia kauli hii ni muhimu kwani hili Barrick halitaacha mtu salama
Mkuu kwa nini unasema Barrick halitaacha mtu salama?

Mimi nadhani tusubiri uchunguzi ufanyike ili tujue mbivu na mbichi.
 
Back
Top Bottom