Kumbe wanaopanda daladala bure wanaitwa maiti na mizoga?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Nikiwa katika daladala nimewasikia kondakta na dereva wakiwa katika mazungumzo yao ambayo sikuwaelewa mapema walichokuwa wakizungumza mpaka baadaye nilipouliza walikuwa wanazungumzi vitu halisi au walikuwa wanazunguza kimafumbo ili abiria wasijue.

Konda: Mshikaji tumepakia maiti weee sasa wameona haitoshi wanataka tupakie na mizoga;
Dereva: Hawa wenye mabasi nao ni wa...nge tu wao wanakwenda kupatana tupakie watu bure halafu hawashushi hesabu wanafikiri sisi tutapata wapi za kuwalipa na sisi tubaki na chochote
Konda: Kwa mtindo huu bora kupakia Washeli nyingi kuliko hizo maiti na mizoga. Tripu za kwanza asibuhi na za jioni zitakuwa hasara sana kwani ndio muda wa maiti, mizoga na washeli

Nikagundua kumbe walikuwa wanawazungumzia askari na walimu kuwa wao ndio maiti na mizoga. Hili neno mizoga ndio linatumika kwa walimu sasa lakini la maiti lilikuwepo muda mrefu. washeli ni wanafunzi ambao wao angalau wanalipa nauli kuliko askari na walimu ambao nao wanaingizwa katika mstari wa kutolipa nauli.

My take: Mimi naona kama alivyosema mbunge mmoja kuwa kuwaambia walimu wapande bure ni kutawadhalilisha sana mbele ya jamii ni bora wangeongezewa kidogo kwenye mishahara yao kwani wataanza kudhihakiwa tofauti na wenzao askari ambao wao wanaogopwa hata kama makonda hawapendi lakini wanalazimika kuwapakia na kunyamaza huku wakiugulia mioyoni. Lakini wanaweza wasiwavumilie sana walimu. Maneno Maiti na Mizoga sio matusi ila ni rejesta ya mawasiliano kwa makondakta na madereva wa daladala ingawa haipendezi sana hasa kwa hadhi za watu wanaokusudiwa
 
JiWe ni mtu anayeanzia mwanzo wa kituo mpaka mwisho wa kituo bila.kushuka...makonda pia wanachukia kupakia mawe
 
Back
Top Bottom