Prezidah
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 750
- 182
Mtakubaliana na mimi kuhusu nguvu kubwa iliyopo kwenye muziki katika kufikisha ujumbe kwa jamii. Uzuri wa muziki ni kwamba unarahisisha ujumbe kiasi cha kuweza kueleweka kwa watu wa rika zote watoto, vijana na hata wazee. Ndio maana wasanii wanatumika katika kampeni mbalimbali ikiwemo za siasa.
Leo nataka niwakumbushe kidogo historia ya nguli wa muziki nchini Prof. Jay hasa kwa upande wa kushiriki harakati za ukombozi wa watanzania kupitia sanaa ya muziki. Ni jukumu letu ni wimbo uliobeba ujumbe mzito kuhusu hali ya uchumi nchini na umuhimu wa kila mtanzania kushiriki katika kujenga tanzania. Nanukuu baadhi ya mistari "tanzania imegubikwa na umasikini wa kila hali wapo wanaokosa chakula, ada, maji na huduma za afya. Alafu akasema "ni jukumu letu wananchi wote mimi na wewe na maoni yetu yawezayo kupunguza umasikini kwa taifa letu hivyo yatupasa tuwe makini ni jinsi gani tutaweza kuongeza kipato nchini"
NDIYO MZEE
Kupitia wimbo wa "Ndiyo mzee" akagombea na kushinda urais (wimbo) baada ya kumwaga ahadi nyingi zikiwemo mabomba kutoa maziwa......
NANG'ATUKA
Nang'atuka nimeshaikosea jamii nikajiita Mungu mtu nikajiita nabii, Nang'atuka Mwenyenzi kumbuka na nafsi hii napiga goti natubu daima nitakutii. Hapa anaomba radhi baada ya kutotimiza ahadi.... ..........
Kwa maoni yangu naona anastahili kukamilisha ndoto yake hiyo na Namtakia kila la kheri