G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,598
- 36,023
Ama kweli hii ni ya aina yake. Leo nikiwa njiani mara nikaona konda wa daladala akijibishana vilivyo na askari wa usalama barabarani nusura kushikana mashati.
Nikasogea karibu kuona kinachojiri. Hapo ndo nikamsikia yule konda wa daladala akilalamika kuwa yule askari polisi aliyemkamata na kumpa kile kirisiti cha TRA anamuonea kwani jana jumamosi alikamatwa kwa kosa hilohilo na kupewa kirisiti cha TRA! Kwa jumla amesema kuwa leo na jana ametozwa shilingi (T) 60000 yani kila siku shilingi (T) 30000
Nilipomuuliza yule konda kwani kosa hasa ni lipi hapo ndipo nikastaajabu! Kosa lenyewe ni gari kutoa moshi! Eti gari inatoa moshi kupita kiasi!
Mbaya zaidi yule askari polisi akawa anasema kuwa malengo aliyopewa na boss wake ni lazima yatimie! Hapa sisemi! Nikisema huwa naonekana mpinga Maendeleo!
Kama haya ndo mapato TRA wanayosema kuwa wamevuka lengo kila wakija kwa waandishi wa habari basi huu ni uonevu wa dhahiri!
Magari mengi hasa ya serikali ni chakavu hilo halina ubishi! Mbaya zaidi magari haya ya serikali ni chakavu kusiko kawaida! Nenda kaangalie magari ya wakurugenzi wa taasisi mbalimbali uone! Haya huwa hayatozwi ushuru kwani serikali tukufu itajipunja mapato na kushindwa kufikia malengo na kuyavuka!
Kwa barabarani serikali inakamua vilivyo na mbaya zaidi yule polisi ni vigumu sana kukukosa na kosa.
Kila lakheri!!