Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi.

Naanza na kanuni ya haki duniani inayoitwa "the presumption of innocence until proven guilty" Yaani mtuhumiwa yoyote anahesabiwa kuwa hana hatia hadi atakapotiwa hatiani, na mahakama yenye mamlaka sahihi, hivyo Paul Christian Makonda anaendelea kuwa ni Paul Christian Makonda na Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka hapo itakapo thibitishwa vinginevyo, tena without any reasonable doubt kuwa Paul Christian Makonda ni mtu mwingine, na Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli na kupata sifuri, akaiba jina na vyeti vya Paul Christian na kuvitumia kujiendeleza as if yeye ni Paul Christian hivyo ni kweli huyu Paul Christian Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam ni kiongozi fake, anayetumia majina fake, vyeti fake na mtu halisi ni Daudi Albert Bashite aliyefeli darasa la Saba na kupata division 0 kidato cha nne!.

Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye hii fani hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, IJ, ila nimeamua kujikita katika kuandika habari za kimaendeleo tuu, "developmental news" ambazo ni habari zenye maslahi na impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ya udaku ambayo haina maslahi chanya kwa taifa, lakini kwa vile wabongo wengi wanapenda sana udaku hivyo hapa nitatoa maelekezo namna ya kupata uthibitisho wa uzushi na uongo huu unaoenezwa kumhusu Makonda kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite, na kuwa ameiba jina baada ya kufeli shule, na ame foji vyeti na kujiendeleza.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ukisemwa sana, bila kukanushwa mwishowe kugeuka kuwa ni ukweli.
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Sasa nimebadili msimamo baada ya kugundua kuwa, uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo tuu hata ukisemwa vipi au mara ngapi, hauwezi hata siku moja kugeuka ni ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli tuu hata usiposemwa. Ukituhumiwa kwa tuhuma zozote za uongo au kuzushiwa jambo baya lolote, as long as unajua ni uongo, huna haja ya kukanusha, wewe jinyamazie tuu kimya, ule msemo wa "tell the truth and the truth will set you free" ni msemo wa uongo, kanuni yangu ni "just keep silent about the truth, and the truth will remain the truth".

Uthibitisho kuwa tuhuma hizi ni uzushi, ni huu ukweli bayana uliopo mbele yetu hadi sasa kuwa Mhe. Paul Christian Makondo ni mteule wa rais wa JMT aliyefanyiwa vetting na vyombo husika na kuthibitisha pasipo shaka wasifu wake hivyo akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa hapa tunavyozungunza, Paul Christian Makonda, ndiye Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, na huu ndio ukweli bayana na ukweli halisi uliopo, mkubali, mkatae, ukweli unabaki kuwa ukweli, mengine yote ni uzushi tuu!.

Jee wewe Mtanzania mwenzangu, kati ya wazushi hawa wanaomzushia Makonda kuwa ana jina la bandia na vyeti vya kughushi, na rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyemwamini Makonda hadi kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kuendelea kumwani mpaka hii leo, licha ya kuibuka kwa tuhuma hii, unamwamini nani kati ya wazushi na rais wako?.

Kwa maoni yangu Mkweli ni Rais wa JMT, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, kwa sababu tangu kuibuka kwa tuhuma hii, serikali kupitia vyombo vyake, ingeishafanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Anne Kilango alipodangwanywa tuu, alitumbuliwa pale pale!. Kitwaga alipopata kidogo tuu pale Bungeni, alitumbuliwa pale pale lakini kitendo cha Paul Makonda, hadi dakika hii, bado ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwangu ni uthibitisho tosha kuwa tuhuma hizi ni za uongo, ni za uzushi, ni za kutunga na za kubuni, haiwezekani kabisa mteule wa rais Paul Christian Makonda akaiba jina, akafoji cheti!. Huu ni uzushi wa kupuuzwa kabisa na ndio maana hata Makonda mwenyewe amezipuuza, na Rais hajachukua hatua yoyote, na wala hata chukua hatua yoyote kwa sababu soon wengi mnaojua Kuwait Paul Makonda ndiye yule ambages... "Huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu, ninaye pendezwa naye", hata akifanya nini, mtapiga tuu kelele za kujisumbua bure!, ndio maana mpaka sasa watu wametulia tuu na kuzipuuzia hizi kelele zote za kizushi huku wazushi wakiendelea kupiga kelele.

Wengi mliujua uwezo wa Makonda, alipoanza vita na wauza unga, sisi wengine, tuliujua uwezo wa Makonda toka akiwa DC na tulitoa ushauri ufuatao kwa Magufuli
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Tena tumependekeza
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana ...

Watanzania tupunguze kushadadia uzushi, tujiunge na rais wetu kumtia moyo Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda endelea kuchapa kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa wasiolitakia mema taifa letu.

Nawatakia Jumatano Njema ya Majivu, leo ni siku ya kufunga kwa sisi Wakristo Wakatoliki, tunaanza mfungo wa siku 40 za Kwaresma.
Kwaresma Njema
Paskali
Update.
huu pia ni uthibitisho wa jinsi watu walivyo waongo na wazushi kumhusu mtu huyu. Mkuu wetu wa Mkoa jina lake halisi na la ukweli ni Mhe. Paul Christian Makonda. Vyeti vyake viko kwenye mamlaka yake ya ajira ambayo sio hapa jf. Zile habari za Daudi Albert Bashite ni uongo wa mchana kweupe wala hakuna mtu kama huyo duniani, wala hakuna yoyote mwenye vyeti vya Bashite ulikuwa ni uongo tuu.

Mkuu wetu wa mkoa anaendelea kuchapa kazi za ujenzi wa taifa as if nothing has happened. Kelele za mlango hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

Paskali.
 
Wewe ni mwandishi wa habari sawa lakini wa level ya chini sana,kama Tanzania inategemea waandishi kama wewe basi tumekwisha
Habari unazohangaika nazo kila kukicha zinasaidia nini nchi yetu kama sio kukuonyesha udhaifu wako wa umbeya,achana na hizo habari hazitusaidii tena
 
Utumwa wa fikra huo.....

Wapo waliokwenda kwa wazazi wao na kuwahoji ... majibu yapo.

Kijijini kwao sio mbali, tulioko jijini Mwanza tumeishapewa ukweli wa kila kitu ...

Muulize kama hawafahamu akina Poneja ... wanamfahamu vizuri sana hata yeye anajua hilo.

Kama unataka akujali kwenye maslahi yako binafsi useme ila hatutaki uongo hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…