streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 476
Kitu gani mkuu?Bora hata ulivyouleta huu uzi umenikumbusha kitu
Kina nani hao?Wale jamaa lazima waje hapa.
Hatuna kitu cha kujivunia,Kitu gani mkuu?
Umelenga penyewe haswaa.Nimejitahidi kuumba uhalisia wa Mwanadamu kuhusu maisha yake na mahusiano yake na Mungu, mazingira na roho yake, nimegundua hakuna kitu chochote mwanadamu anachomiliki. Kwa kuanza na roho yake, binadamu kapewa kutoka kwa Mungu, na pia akapewa na mwili ili roho ipate kujihifadhi kuendana na Mazingira. Sikuhishia hapo nikayatazamana mazingira anayoishi mtu huyu nikagundua kuwa yaliandaliwa na Muumba wake ili yamfae katika kumtumikia. Nikamalizia na kuangalia vitu alivyotengeneza na kuvumbua mwanadamu ni matokeo ya matumizi ya akili yake aliyotunukiwa na Muumba wake. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi kua ni kipi hasa binaadamu anamiliki katika dunia hii kama roho,mwili na akili inayomfanya ajivune na maendeleo aliyonayo hasa yakiteknolojia, kumbe sio yake bali ni matokeo ya akili aliyopewa na muweza wa wote? Nikapata na mshangao kuwa kumbe binaadamu anapokufa ni huwa roho yake inachukuliwa na anaacha kila kitu alichokuwa nacho! Na kama angekua anamiliki hasa uhai angekua na maamuzi nao, ivyo Mungu ndio mmiliki sahihi ndio maana maamuzi yake kwenye maisha yetu hayapingwi na yeyote au chochote. Nikahitimisha kuwa Mwanaadamu hana kitu zaidi ya kupata upendeleo wa utashi kuliko wanyama wengine na ivyo anapaswa kumtumikia Mungu maana ata Uhai anaoringa nao sio mali yake. Asanteni kwa kuelewa.
Wakija hapa utajua tu kuna watu wamekuja.Kina nani hao?
Asante sana mkuu,Mungu akubariki.Umenena yaliyo ya kweli kabisa na nakuombea Mwenyezi Mungu azidi kukuongoza. Amiin
Nimejitahidi kuumba uhalisia wa Mwanadamu kuhusu maisha yake na mahusiano yake na Mungu, mazingira na roho yake, nimegundua hakuna kitu chochote mwanadamu anachomiliki. Kwa kuanza na roho yake, binadamu kapewa kutoka kwa Mungu, na pia akapewa na mwili ili roho ipate kujihifadhi kuendana na Mazingira. Sikuhishia hapo nikayatazamana mazingira anayoishi mtu huyu nikagundua kuwa yaliandaliwa na Muumba wake ili yamfae katika kumtumikia. Nikamalizia na kuangalia vitu alivyotengeneza na kuvumbua mwanadamu ni matokeo ya matumizi ya akili yake aliyotunukiwa na Muumba wake. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi kua ni kipi hasa binaadamu anamiliki katika dunia hii kama roho,mwili na akili inayomfanya ajivune na maendeleo aliyonayo hasa yakiteknolojia, kumbe sio yake bali ni matokeo ya akili aliyopewa na muweza wa wote? Nikapata na mshangao kuwa kumbe binaadamu anapokufa ni huwa roho yake inachukuliwa na anaacha kila kitu alichokuwa nacho! Na kama angekua anamiliki hasa uhai angekua na maamuzi nao, ivyo Mungu ndio mmiliki sahihi ndio maana maamuzi yake kwenye maisha yetu hayapingwi na yeyote au chochote. Nikahitimisha kuwa Mwanaadamu hana kitu zaidi ya kupata upendeleo wa utashi kuliko wanyama wengine na ivyo anapaswa kumtumikia Mungu maana ata Uhai anaoringa nao sio mali yake. Asanteni kwa kuelewa.
Asante mkuu, Mungu azidi kukuzidishia yaliyo mema.Hakika unapaswa sana kumshukuru MUNGU muumba kwa huu uwelewa na hekima yake aliyokupatia ya kufahamu haya yote.Barikiwa sana kiongozi.Nami nitabaki kusema yakuwa laiti kama sote tungekuwa na huu uwelewa japo hata kwa kiasi kidogo,ni yangu matumaini ya kuwa "CHUKI,WIVU,MAJIVUNO,TAMAA MBAYA,MAJUNGU,KUJIKWEZA,UONEVU BAINA YA MWENYENACHO NA ASIYE....etc yotee haya yangelipungua sana.
Nimependa sana uzi wako na uzidi kubarikiwa ndugu!!......πππππ