streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 475
Nimejitahidi kuumba uhalisia wa Mwanadamu kuhusu maisha yake na mahusiano yake na Mungu, mazingira na roho yake, nimegundua hakuna kitu chochote mwanadamu anachomiliki. Kwa kuanza na roho yake, binadamu kapewa kutoka kwa Mungu, na pia akapewa na mwili ili roho ipate kujihifadhi kuendana na Mazingira. Sikuhishia hapo nikayatazamana mazingira anayoishi mtu huyu nikagundua kuwa yaliandaliwa na Muumba wake ili yamfae katika kumtumikia. Nikamalizia na kuangalia vitu alivyotengeneza na kuvumbua mwanadamu ni matokeo ya matumizi ya akili yake aliyotunukiwa na Muumba wake. Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi kua ni kipi hasa binaadamu anamiliki katika dunia hii kama roho,mwili na akili inayomfanya ajivune na maendeleo aliyonayo hasa yakiteknolojia, kumbe sio yake bali ni matokeo ya akili aliyopewa na muweza wa wote? Nikapata na mshangao kuwa kumbe binaadamu anapokufa ni huwa roho yake inachukuliwa na anaacha kila kitu alichokuwa nacho! Na kama angekua anamiliki hasa uhai angekua na maamuzi nao, ivyo Mungu ndio mmiliki sahihi ndio maana maamuzi yake kwenye maisha yetu hayapingwi na yeyote au chochote. Nikahitimisha kuwa Mwanaadamu hana kitu zaidi ya kupata upendeleo wa utashi kuliko wanyama wengine na ivyo anapaswa kumtumikia Mungu maana ata Uhai anaoringa nao sio mali yake. Asanteni kwa kuelewa.