Kumbe huu utapeli bado upo?

Dah, huyo dogo poyoyo sn. Huo utapeli wa kizamani mno.
 
Aisee umenikumbusha!

Siku moja majira ya saa mbili usiku. Ilikua jumapili nakumbuka. Nimefika zangu mqkumbusho nasubiri gari la kwenda mbagala. Mgongoni nina begi lililotuna


Wakati nimesimama pale magari ya mbagala yanapoingilia (mkabala na mesuma plus), akaja mzee mmoja akaniuliza wapi ilipo bank ili akafanye exchange ya $ to madafu (tshs) Akawa anasema katoka kulipwa na wasomali ujira wake wa miaka 3
. Akatoa ka-kitita hivi akanionyesha.

Na nukuu machache " Nsaidie mdogo angu, siku hizi watu ni matapeli. Nisaidie unipeleke nitakupatia hela ya maji"

Nkamwambia leo ni jumapili alafu sasa hivi ni ni usiku, ni ngumu kupata msaada hadi kesho (jumatatu yaani)

Wakati naendelea kumsikiliza akaja kijana mmoja kavaa casual (kama mtu flani hivi anaejiheshimu). Nikajua nae anasubiri daladala, akatuuliza kuna nini, nikamweleza kwa niaba ya yule mzee.

Akasema, "kuna mtu anamfahamu anashughulika na mambo hayo, ngoja nimpigie nimuulize yuko wapi atusaidie"

Akapiga, nikaongea na huyo mzee (wa bureau exchange) ili nijiridhishe maana machale yalishanicheza. Jamaa akasema twende, tutamkuta BIASHARA COMPLEX. nikakubali kuongozana nao though nlikua nasitasita. Sasa yule mzee mwenye madola akaomba tumlipie nauli afu akishachange hela atatukatia chetu. Nikasema sio kesi.

Tukaenda hadi biashara complex kwa bahati nzuri nauli hatukulipa (nahisi konda alisahau). Sasa pale tukamkuta yule jamaa kwenye gari. Kijana mtanashati akasema tuingie kwenye gari ili tubadilishiwe hela.

Asee Roho ilikataa katakata. Nikawaambia badilisheni mtanikuta nje. Yule mzee mwenye dola akashuka na kunifuata (maanq alishaingia kwenye gari). Akaanza kunchombeza "mimi nakuamini wewe na blah blah " . Nikamwambia umetaka uonyeshwe na tayari umeonyeshwa.

Hapo akarudi kwenye ile gari (kama crown hivi) wakaondoka wote. Nikawa najiuliza watu muonane leo afu muaminiane kiasi kwamba muondoke wote kwenye gari moja !

Nilipona kwa staili hiyo.

NILICHOJIFUNZA: Ni muhimu kuwa na hela , kama ningekua mweupe (sina hela) ningekua na tamaa ya kupata pesa. UMASKINI MBAYA SANA



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umesahau ulitoka Narungombe ukaingia Livingstone ulipofika Mtaa wa Mahiwa ukaleta ujanja wako huo nikaponyoka kukutapeli, Siku hizi umekuwa mjanja heee
 
Ukiponea Uzi na sindano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ulibakiza kidogo tu wakutapeli na pengine wangekupeka chaka wakakuulia huko. Ulifanya kosa kubwa sana kufuatana na watu usiowafahau. Jiulize, dunia ya leo mtu hakujui kwanini akuamini kiasi hicho? Somo la kwanza: ukikutana na mtu yeyote ambaye humjui na ukaone anakuchangamkia usimchekee. Kuwa serious kabisa na vaa sura ya hasira kali. Akijifanya kuelezea mambo ambayo kwa hali ya kawaida mtu mgeni hapaswi kukuelezea, mfukuze.
 
Kuna jirani yetu alipigwa style hii nikiwa primary, nimefika form two natoka mchikidown kucheki ratiba nashuka Tandika nikakutana nao wakaniimbisha but nikawastukia nikawa nawaza jinsi ya kuwatoka pindi wapo busy kuniimbisha mie sipo kabisa pale kimawazo. Ikafika time ya kuacha vitu kwa mwenzio jamaa akaenda kanipa wallet ile anapotea tu nikamwona mmama anapita kwa mbali nikamwambia mganga huku natoka nduki kwamba naenda kumuita mama yangu yule anapita aje asikie matatizo niliyonayo ndiyo kimoja hiyo
 
Suala la msingi ni kuacha tamaa na shortcut. Wanaotapeliwa ni wenye nacho, huwezi tapeliwa kama huna kitu. Kuwa na hela sio suluhisho la kutotapeliwa maana wewe ndio mlengwa wa kutapeliwa. Muhimu ni kuridhika na ulichonacho. Never trust a stranger.
 
Umeongea mambo ya msingi. Watu wafuate ushauri huu.
 
Hii ya pochi mjomba wangu ambaye sasa ni marehemu aliwahi kutapeliwa mjini Moshi mwaka 1970! Imagine mpaka sasa bado mtindo unatumika.
Hii ilinikuta makambako miaka ya 2006-2007 hivi. Alipita jamaa na baiskeli yupo nduki mara nikaona bunda kubwa la noti la sh.500 hivi limedondoka. Mara ghafla akapita mtu toka nyuma yangu akawahi lile bunda kuokota akawa anashangaa kwa sauti, akaona mimi sina time kabisa wala sijawehuka na lile bunda basi akaondoka zake. Kama ningeonyesha kuwehuka angesema twende tukagawane, halafu huko wangenikaba na kuiba kila kilicho changu.

Nilishtuka mapema kwasababu nilishawahi simuliwa story kama hii siku za nyuma. Mwenyezi MUNGU alinipa wasaa wa kuepuka utapeli ule.
 
Wewe ulikuwa unaibiwa huku unajua kuwa unaibiwa, tatizo lako ulikuwa muoga, ulishindwa kujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…