Kumbe hata Azam wanaweweseka!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe hata Azam wanaweweseka!!

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jul 31, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mojawapo wa utofauti ambao nimekuwa nikiamini umeletwa na team ya Azam ni undeshwaji wa kisasa wa team hiyo inayomilikwa na mmoja wa matajiri wakubwa sana hapa nchini. Katika team hii sikutarajia kuona/kusikia mambo ambayo nimekuwa nikiyaona na kuyasikia kwenye team za Simba na Yanga,ni lazima niseme nimesikitishwa sana na shutuma zilizotolewa na uongozi wa team hii kuwa kuna wachezaji walicheza chini ya viwango vyao ili kuruhusu Yanga kuchukua ubingwa....jamani nyie ni Azam haya mambo ya kushikana uchawi ooh fulani kafungisha fulani kacheza chini ya kiwango embu ziachieni hizi team 2 (za Simba na Yanga),ni wajibu wenu kujitambua kwani nyie hata akina Mzee Akilimali hamna kila kitu mnaendesha kisasa sasa inakuwaje mnajisahaulisha kuwa mchezo wa mpira una matokeo ya aina 3 kushinda,kushindwa na kutoka sare.
  Eti Salum Aboubakar,Mrisho Ngassa na Dida wamewahujumu kwenye mechi na Yanga,mbona hamkuwashutumu kwenye mechi na Simba fainali ya Urafiki ambako mlifungwa,au hujuma ni pale mnapofungwa na Yanga tu? acheni kuweweseka bwana mnawavunja mioyo hawa Vijana wadogo wanaochipukia,mtaharibu.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  hawana ujanja hao.
   
 3. daniel don

  daniel don Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamezidiwa na uzoefu, bado wachanga hao...Yanga bado itabaki Yanga milele..wana kipigo kingine Ligi kuu wasubiri!
   
 4. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wataweweseka sana mwaka huu ngoja ligi ianze hasira zote za mwaka jana zitawaishia.
   
Loading...