jitwangabalogi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2018
- 480
- 638
Kulipo na Wakuu hawakosi Matowashi ... Ila wote nawasalimu kwa jina la Mungu wangu HAMJAMBO!?
Leo nitawapa kisa hiki ambacho kilinitokea ndugu yenu mpendwa, Nilibahatika kupata demu mmoja dar mzuri kwelikweli kwa sura , rangi na hata shepu yake. Ni msichana mwenye wastani wa miaka 24" baada ya kutokea kupendana hivyo tukaamua wote kukaa pamoja, lakini ndani ya miezi mitatu maisha yalibadilika sana kwa upande naweza kusema hivyo nikwa sipendi kabisa kwenda kazini na hata bosi akiniuliza natoa sqbabu zisizo na msingi wowote, yaani kwa wiki nikienda kazini mara tatu yani hapo nimejitahidi sana na nikiwa kazini kazi yenyewe sifanyi, baadae huyu demu alinishauri niache kazi na bila pingamizi nikamkubalia kabisaa na kazi nikaitema simpo tu ila yeye akiendelea, baadae nikawa ni mtu wa kulala ndani kuanzia usiku mpaka usiku, kazi zote za nyumbani kupika, kuosha vyombo na hata kufua ikawa ni mimi nazifanya, ilifika mda huyu demu anaweza kuondoka na kurudi mda anaotaka au asirudi kabisa na sina la kumfanya, na hata pale nitakapomuuliza chochote huwa mkali kwelikweli na hata kama kosa ni lake ila mimi ndie nitakayemuomba msamaha, kingine zaidi ilikuwa ni pale ninapokula huwa napata radha tofauti na chakula kilivyo au mda mwingine kinakuwa kama kimemwagiwq mchanga hivi,siku nyingine naamka kama nilijimwagia ungaunga hivi usoni, siku nyingine nikute unga mweupe umemwagwalangoni n.k na yote hayo nikimuuliza huwa ni mkali kweli hivyo huamua kukaa kimya tu, na pia chochote nachofanya huyu demu ni lazima ajue tu, na marafiki zangu wengi niliowatambulisha huyo demu asilimia kubwa waliniambia niachane nae kwani hanifai au hatuendani, lakini niliwachukia wote wale ambao wangenishauri niachane nae maana niliona kama wao ndio wanamtaka, siku moja sijui ni nini kilinitokea tu , nilishituka usiku usingizini nikamuona huyo demu kajifunga kitambaa cheusi kichwani na kiunoni kajifunga nguo nyeusi na pembeni kulikuwa kumewashwa mshumaa na mbele ya mshumaa kulikuwa na fimbo yenye urefu na unene wa wastani mfano wake ni kama zile wanazoshika wakuu wa polisi, chumba kizima kilikuwa kimejaa moshi wenye harufu ya ajabu sana yaani nilibaki nimeduwaa nikimwangalia na yeye akabaki ananiangalia tu, tulikaa hivyo kwa dakika kama tatu tunashangaana tu ila baada nikaanza kuona macho yanakuwa mazito na yanalazimisha kufumba kwa nguvu, nilijilazimisha sana kuyazuia yasifumbe lakini baadae nilishindwa na hapo hapo nikapitiwa na usingizi mzito sana.....
Punde nitakuja malizia kisa hiki...naomba pia mnisamehe maana mimi sio mwandishi mzuri.