Kumbe ccm mmeoza kiasi hiki sikujua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe ccm mmeoza kiasi hiki sikujua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Joblube, Nov 15, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikufuatilia hoja mbalimbali hasa kuhusu mustakabali wa uongozi wa nchi yetu. Moja ya hoja hizo ni kuwa kunaombwe la uongozi ndani ya CCM chama tawala kama kinavyopenda kujiita na nikweli ni tawala badala ya kuwa kiongozi. Lakini sikujua kuwa CCM imepoteza maono na fikra kwa jinsi inavyojidhihirisha sasa hasa katika hili la uundaji wa Katiba. Hivi kweli CCM haioni umuhimu wa kuwa na katiba inayotokana na wananchi kwa kuzingatia matakwa ya wananchi ama kweli waswahili walisema sikio la kufa halisikii dawa. Hivi kukiwa na tume huru ya kusimamia katiba inayoaminiwa na watu wote isiyotokana na Rais mtapoteza nini. Hivi hata hawo wazee wenu wameishiwa busara kiasi hicho kushindwa kuona kuwa hayo mnayongania mtaleta machafuko ambayo yanaepukika kwa kufanya mchakato wa wazi usio na mawaa. Kwa jinsi mmnovyofanya mambo sidhani hata kama mnajua kuwa Watanzania tumebadilika sasa sio wale wa ndio mzee tena, wenyeupeo wa kujua nani mwongo nani mkweli ,ipi pumba na upi mchele. Ushauri wangu ni huu nimegundua kuwa kweli CCM mnakufa lakini wakati mnakufa kateni roho taratibu msije mkaicha nchi vipandevipande mimi si mpenzi wa maandamano kwa hili lakatiba ambalo ndio uhai wangu na vizazi vyangu vijavyo nitaandamana nangoja watangaze siku yakuanza maandamano.
   
Loading...