onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Nimejisikia vibaya baada ya spika Ndugai kuwauliza wabunge kuwa ni lini walipitisha Sheria mbaya na kandamizi ya kutaifisha mifugo pale wanapoingia katika hifadhi. "Hivi hii Sheria ilipitishwa Lini..tulikuwa tumesinzia au ilipitishwa wakati sipo".
Jamani nchi hii Kuna baadhi ya watu wametumia vibaya madaraka yao kuwaumiza wenzao. Eti mifugo ikikanyaga tu kwenye hifadhi inataifishwa na kupigwa Bei! Kama aliyekuwepo na mtu anayesimamia na kuona Sheria zenye manufaa zinajadiliwa na kupiitishwa ndio anaanza kujishangaa, Sasa sisi wananchi tufanye lipi.
Kumbe mle bungeni wapo tu kwa kivuli Cha CCM na hakuna lolote linalofanyika. Kujishangaa ni dalili za wehu. Pesa zetu zinaliwa bure na watu wasio na hili Wala lile.
Hata hivyo ukiwa mtenda maovu siku ukianza kujitambua kuwa unayoyatenda siyo sahihi ujue God anakuhitaji ili akuhifadhi. Katiba mpya inahitajika Sana ili tusiweze kujishangaa.