Kumbe asili inaponya!

Kumbe asili inaponya!

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,456
Reaction score
5,134
Watu wanaishi maisha, wanayapenda mpaka inafika hatua hawako tayari kuacha kuishi, yaani hawataki kufa. Hii ni kwa jamii zote, lakini kwa sisi waafrika ni tofauti. Mwafrika wa kawaida kabisa, yaani kipato cha kati anaweza ishi muda mrefu bila ya kuugua. Hapo anatumia vitu asili na visivyo asili vikiwa vingi. Huyo mtu anaweza ishi muda mrefu lakini, kama atapata changamoto ndogo kiafya ni rahisi kufa au kuzeeka na matatizo mengi.

Tunapenda kuishi lakini je, tunapenda kuishi bila kuugua kwa mda wetu wote? Je mnapenda kama waafrika kuwa na mwisho mzuri(natural death)? Au unapenda siku zako ziishe ukiwa umezungukwa na watu waliofunika pua, wamebeba mikasi,gloves,visu na vifaa vingine huku tayari wameshakupasua mwili wako?
Wengi mnapenda muwe na mwisho wenye amani, kiasi ambacho hata jamii itabaki inashangaa. Kuweza kutimiza yote uliyopanga, kuzungumza na kuacha maagizo muhimu kwa unaowapenda.

Haya ndio maisha walioishi babu zetu, jamii za kale, watu waliopenda asili na asili ikawalinda mpaka mwisho. Hawa waliacha msingi mzuri, ila kama jamii tukaona haifai waliyoyaishi ni mabaya hivyo tufanye njia tofauti. Hii ndio imetufikisha hapa tulipo ambapo ugonjwa kama blood pressure imekua fashion, vivo hivyo kwa kisukari,cancer, watoto kuzaliwa na mapungufu, magonjwa mapya na madhaifu mengi. Haya yote hayana unafuu hata kidogo, baya zaidi ni kua wale tunao wategemea kua ndio waangalizi muhimu wa afya zetu, wamekiri kua hayo ni matatizo sugu na hayana tiba.

Wakati huo bado fahamu zinatuambia kabisa kua tiba ipo na tiba ni asili uliyoachiwa na waliokutangulia, ila kwa kiburi cha elimu unakiri hiyo ni ya zamani na imepitwa na wakati. Lakini ndio nyinyi kama jamii ambapo yanapotokea matatizo hasa misiba kwa mnao wapenda mnalia na kuhuzunika. "Ooh God why, God this God that". God ni kitu gani? God si hiyo asili ulioyo iacha? Je kama ungekua umejali asili yako toka mwanzo ungelia God why?. Imefikia hatua kama jamii, tumeshindwa kuzitawala afya zetu kabisa.

Watu wapo katika msiba wa mpendwa wao ayekufa kwa kisukari, pressure n.k na katika risala wanakiri mateso na harakati zilizo fanywa ili kuokoa uhai wa mpendwa wao, ila hapo hapo msibani wewe umekamata vinywaji visivyo asili, vyakula na vinginevyo na mnakula kama hamna akili nzuri. Mnashindwa kuona kua misiba ni fumbo, magonjwa ni mafumbo na mmewekewa ili mjifunze mbadilike hali hiyo isijirudie tena, ila kama jamii hilo hatulioni.

Kila muda mnaokaa mezani ili mpate chakula mna commit a delicious suicide of your own. Yaani tusiwashangae wanaojinyonga na kunywa sumu,ila tushangae kua sisi tunaokula vyakula ambavyo vinatengeza mwisho wa maumivu na mateso. Hivi sasa watoto wadogo wanaugua kisukari, magonjwa ya ukubwa wa moyo n.k. Ila yote hayo sio makosa yao, ni makosa ya wazazi wao, nyinyi. Mmeishi maisha feki yasiyo na asili yenu, dawa zisizo za asili yenu, vinywaji visivyo vya asili yenu na vyakula unnatural pia. Halafu mkajoin na kujenga watoto wenye madhaifu mengi, hayo si makosa yao, ni nyinyi kama jamii na wazazi ndio mnajiangamiza wenyewe na uzao wenu mnaufanya uteseke.

Kwa hali inavyo elekea kwa jamii za kiafrika itafika hatua kua mzee wa miaka 50-60 kama hana pressure au kisukari yeye basi si mzee, Si ndio? Yaani kua mtu akizeeka basi ni lazima apate either kisukari, magonjwa ya mifupa, pressure n
.k.

Hii sio sawa. Kama jamii za kiafrika option ya kubadilika ipo, nyinyi mna asili zenu, vyakula, dawa na aina ya maisha. Kama mkiamua kuziishi hizo asili basi zitawalinda, mkizikimbia na zenyewe zitawakimbia, na kuumia ni lazima. Tuchukulie mti, mti ukakua halafu ukapakwa rangi ya kiwandani, Je huo mti utapendeza? Je rangi itaondoa asili nzuri na rangi asili ya mti? Jibu ni hapana, na huo mti utakua na sura mbaya, hapa ndipo jamii za kiafrika zilipofikia.

Pia tupande mche wa mti kwenye udongo mzuri, tuumwagilie maji ya sabuni kila siku, huo mti utakua wa hovyo. Kama jamii za kiafrika imefika hatua tuseme hapana, magonjwa haya yanayochangiwa na mifumo ya maisha tusiyaruhusu kwenye familia zetu, kwakua tiba tunazo katika koo na asili zetu, tiba iwe ni chakula na chakula kiwe tiba na visitengane, hapo kisukari, cancer, pressure, stroke n.k yote mtayasahau.

Siku fulani nikiwa maeneo ya hospitali, katika nje ya wodi ya wazazi kulikua na akina mama watano wa kimasai, wote wametandika rubega chini wanaota jua nje na hawana habari, na niwajawazito, ila akina mama wa kiswahili wako upande mwingine na kwakuwaangalia tu ni kua wanateseka kwa maumivu hata kwa kutembea. Ukifuatilia unakuata hata akina mama hao wakimasai si mara yao ya kwanza kua kwenye hali hiyo na huenda hata njia waliyotumia kupata mtoto ni ya asili na si kwa visu na mateso. Sasa kama ni hivyo kwanini akina mama wa jamii zisizoza kimasai wanakua katika taabu na mateso hivyo? Mbona bibi zao walipata watoto hadi 12 bila ya mateso na wengine wapo hai hadi leo?

Jibu ni moja tu, kua asili ziliwalinda na kuepusha mateso, magonjwa na watoto kuzaliwa na matatizo. Hivyo basi asili inaponya, mkubali au mkatae asili inalinda mateso. Tuamkeni kama jamii za kiafrika, tupende na turudie asili zetu ili zitulinde. Afya zetu zipo mikononi mwetu na tiba asii zimetuzunguka kila mahali, na nyingine zinaota hata nje kwako. Hiyo tiba inayoweza kutibu kisukari, pressure, cancer n.k kwanini usiitumie kila mara uishi vizuri? Kwanini uidharau uje kuzungukwa na mikasi na visu mpaka mwisho? Tupende na tuheshimu asili zetu, tusiwe kama miti iliyopakwa rangi ya kiwandani. Badilika wewe, familia yako na jamii yako.

We Africans.
We Unite.
Peace.
 
NLITAKA NISICHANGIE CHOCHOTE LAKINI NMEONA HAPANA, SITOUTENDEA HAKI UAFRIKA WANGU
GOD BLESS AFRICA
 
Hata mimi navuta kitu cha asili kabisa jani lililopandwa shambani,na sio sigara ambazo ni artificial zimetoka kiwandani
 
Nimekuelewa. Lakini je tusiogee sabuni au tutafute sabuni ya asili ambayo mbali na majani ya mpapai ntaomba kufahamishwa.
Ktk suala sa upatikanaji wa watoto nakuunga mkono US has children shortage kwa sababu ya huu usasa lakini haiondoi fact kuwa hata ukiishi kiasili kiasi gani lazima magonjwa yatakupata tu. Hata hao mababu zetu walipata magonjw wakafa pia.
 
Mkuu nami nimekuelewa saana, na nimekua nikijiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu kwamba kwa nini siku hizi magonjwa yamekua mengi namna hii? Je wazee wetu walikua wakitumia nini mpaka wasiwe na kuugua kusiko isha? Mbaya zaidi hata wale watoto wachanga wasio na ubaya wowote ndio kila leo hawaishi kwenda hospitali, ninini shida?

Lakini je huko kwenye asili tutarudije angali wazee wetu hawakutupa maelezo ya miti waliokua wakitumia kujitibu?
 
Njoo mkowa Wa kagera tukufundishe Daw
 
Well, tatizo lolote la kiafya kwa binadamu ni lazima uangalie kwenye sehemu mbili.
1. Sababu za nje. Hapo kuna usafi, aina ya maji ya kujisafisha, hewa, na vitu vinavyokuzunguka, hapo utapata matatizo kama alegi n.k

2.Sababu za ndani. Hapa tunaangalia maisha kwa ujumla mfano vitu unavyokula na vilivyoingia mwilini ndani kwa njia nyinginezo nyingi.

Yote haya yanaondolewa na kwa kutoa sumu mwilini na ku maintain ph level ya damu iwe 7.365. Kama ikiwa chini ya hapo lazima utakua dhaifu.

Well, visafishiaji vinaweza kua na mdhara kutegemeana na uwezo wa ngozi na mwili kiujumla kupambana na madhara. Hapa unakuta kuna watu hutumia sabuni kutokana na reaction za aleji zao.
Ila mafuta mazuri ya karafuu na nazi ni mazuri kama ukiweza yapata.

Wazee wetu kufariki kwa maradhi ni generation change. Mfano kama kwenye ukoo wenu mnajua mna madhaifu ya pressure na kisukari, ni vyema toka mtoto anaandaliwa hadi anakua, wazazi wabilishe mifumo ya mlo na maisha. Mnaenda mkiresist hivyo ili kuua hiyo gene ya magonjwa hayo. Mkiacha basi kinawatafuna.

Hivyo kwa ujumla ni kua intune na afya yako, the only solution ya kuepuka maradhi mara kwa mara ni kufanya ditoxing ya mwili mzima kila mara.
Detoxing ya mwili inafanywaje??
 
what is the point? we are all going to die one day, enjoy life while you can for it won't last forever
 
Kifo kipo tu dawa ni kuwa na kiasi katika matumizi ya kila kitu.Magonjwa mengine kama cancer zipo za life style zipo za bahati mbaya .Presha sio sababu ya chakula tu watu wana stress na maisha haya,pesa haitoshi,mshahara mdogo,uhakiki,kodi uwezekano wa kupata pressure unakua mkubwa.
 
Watu wanaishi maisha, wanayapenda mpaka inafika hatua hawako tayari kuacha kuishi, yaani hawataki kufa. Hii ni kwa jamii zote, lakini kwa sisi waafrika ni tofauti. Mwafrika wa kawaida kabisa, yaani kipato cha kati anaweza ishi muda mrefu bila ya kuugua. Hapo anatumia vitu asili na visivyo asili vikiwa vingi. Huyo mtu anaweza ishi muda mrefu lakini, kama atapata changamoto ndogo kiafya ni rahisi kufa au kuzeeka na matatizo mengi.

Tunapenda kuishi lakini je, tunapenda kuishi bila kuugua kwa mda wetu wote? Je mnapenda kama waafrika kuwa na mwisho mzuri(natural death)? Au unapenda siku zako ziishe ukiwa umezungukwa na watu waliofunika pua, wamebeba mikasi,gloves,visu na vifaa vingine huku tayari wameshakupasua mwili wako?
Wengi mnapenda muwe na mwisho wenye amani, kiasi ambacho hata jamii itabaki inashangaa. Kuweza kutimiza yote uliyopanga, kuzungumza na kuacha maagizo muhimu kwa unaowapenda.

Haya ndio maisha walioishi babu zetu, jamii za kale, watu waliopenda asili na asili ikawalinda mpaka mwisho. Hawa waliacha msingi mzuri, ila kama jamii tukaona haifai waliyoyaishi ni mabaya hivyo tufanye njia tofauti. Hii ndio imetufikisha hapa tulipo ambapo ugonjwa kama blood pressure imekua fashion, vivo hivyo kwa kisukari,cancer, watoto kuzaliwa na mapungufu, magonjwa mapya na madhaifu mengi. Haya yote hayana unafuu hata kidogo, baya zaidi ni kua wale tunao wategemea kua ndio waangalizi muhimu wa afya zetu, wamekiri kua hayo ni matatizo sugu na hayana tiba.

Wakati huo bado fahamu zinatuambia kabisa kua tiba ipo na tiba ni asili uliyoachiwa na waliokutangulia, ila kwa kiburi cha elimu unakiri hiyo ni ya zamani na imepitwa na wakati. Lakini ndio nyinyi kama jamii ambapo yanapotokea matatizo hasa misiba kwa mnao wapenda mnalia na kuhuzunika. "Ooh God why, God this God that". God ni kitu gani? God si hiyo asili ulioyo iacha? Je kama ungekua umejali asili yako toka mwanzo ungelia God why?. Imefikia hatua kama jamii, tumeshindwa kuzitawala afya zetu kabisa.

Watu wapo katika msiba wa mpendwa wao ayekufa kwa kisukari, pressure n.k na katika risala wanakiri mateso na harakati zilizo fanywa ili kuokoa uhai wa mpendwa wao, ila hapo hapo msibani wewe umekamata vinywaji visivyo asili, vyakula na vinginevyo na mnakula kama hamna akili nzuri. Mnashindwa kuona kua misiba ni fumbo, magonjwa ni mafumbo na mmewekewa ili mjifunze mbadilike hali hiyo isijirudie tena, ila kama jamii hilo hatulioni.

Kila muda mnaokaa mezani ili mpate chakula mna commit a delicious suicide of your own. Yaani tusiwashangae wanaojinyonga na kunywa sumu,ila tushangae kua sisi tunaokula vyakula ambavyo vinatengeza mwisho wa maumivu na mateso. Hivi sasa watoto wadogo wanaugua kisukari, magonjwa ya ukubwa wa moyo n.k. Ila yote hayo sio makosa yao, ni makosa ya wazazi wao, nyinyi. Mmeishi maisha feki yasiyo na asili yenu, dawa zisizo za asili yenu, vinywaji visivyo vya asili yenu na vyakula unnatural pia. Halafu mkajoin na kujenga watoto wenye madhaifu mengi, hayo si makosa yao, ni nyinyi kama jamii na wazazi ndio mnajiangamiza wenyewe na uzao wenu mnaufanya uteseke.

Kwa hali inavyo elekea kwa jamii za kiafrika itafika hatua kua mzee wa miaka 50-60 kama hana pressure au kisukari yeye basi si mzee, Si ndio? Yaani kua mtu akizeeka basi ni lazima apate either kisukari, magonjwa ya mifupa, pressure n
.k.

Hii sio sawa. Kama jamii za kiafrika option ya kubadilika ipo, nyinyi mna asili zenu, vyakula, dawa na aina ya maisha. Kama mkiamua kuziishi hizo asili basi zitawalinda, mkizikimbia na zenyewe zitawakimbia, na kuumia ni lazima. Tuchukulie mti, mti ukakua halafu ukapakwa rangi ya kiwandani, Je huo mti utapendeza? Je rangi itaondoa asili nzuri na rangi asili ya mti? Jibu ni hapana, na huo mti utakua na sura mbaya, hapa ndipo jamii za kiafrika zilipofikia.

Pia tupande mche wa mti kwenye udongo mzuri, tuumwagilie maji ya sabuni kila siku, huo mti utakua wa hovyo. Kama jamii za kiafrika imefika hatua tuseme hapana, magonjwa haya yanayochangiwa na mifumo ya maisha tusiyaruhusu kwenye familia zetu, kwakua tiba tunazo katika koo na asili zetu, tiba iwe ni chakula na chakula kiwe tiba na visitengane, hapo kisukari, cancer, pressure, stroke n.k yote mtayasahau.

Siku fulani nikiwa maeneo ya hospitali, katika nje ya wodi ya wazazi kulikua na akina mama watano wa kimasai, wote wametandika rubega chini wanaota jua nje na hawana habari, na niwajawazito, ila akina mama wa kiswahili wako upande mwingine na kwakuwaangalia tu ni kua wanateseka kwa maumivu hata kwa kutembea. Ukifuatilia unakuata hata akina mama hao wakimasai si mara yao ya kwanza kua kwenye hali hiyo na huenda hata njia waliyotumia kupata mtoto ni ya asili na si kwa visu na mateso. Sasa kama ni hivyo kwanini akina mama wa jamii zisizoza kimasai wanakua katika taabu na mateso hivyo? Mbona bibi zao walipata watoto hadi 12 bila ya mateso na wengine wapo hai hadi leo?

Jibu ni moja tu, kua asili ziliwalinda na kuepusha mateso, magonjwa na watoto kuzaliwa na matatizo. Hivyo basi asili inaponya, mkubali au mkatae asili inalinda mateso. Tuamkeni kama jamii za kiafrika, tupende na turudie asili zetu ili zitulinde. Afya zetu zipo mikononi mwetu na tiba asii zimetuzunguka kila mahali, na nyingine zinaota hata nje kwako. Hiyo tiba inayoweza kutibu kisukari, pressure, cancer n.k kwanini usiitumie kila mara uishi vizuri? Kwanini uidharau uje kuzungukwa na mikasi na visu mpaka mwisho? Tupende na tuheshimu asili zetu, tusiwe kama miti iliyopakwa rangi ya kiwandani. Badilika wewe, familia yako na jamii yako.
We Africans.
We Unite.
Peace.
Unaposema asili ndio maana halisi ya neno uungu na Mungu, kwani katika lugha ya kale ya kimisri neno Mungu ni vitamkwa NETER AMBALO ndio limetupa neno nature kwa lugha ya kiingereza. Kimsingi modern medicine ilianza vizuri baadae ikageuka biashara, wakaanza kutengeneza magonjwa ili wauze dawa. Kuna watu hawapati ugonjwa wa ukimwi, wanakinga Kali mno ya asili
 
Back
Top Bottom