Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,739
- 92,164
Naamini Mods hawataunganisha uzi huu.
Tangu week iliyopita Dodoma kumekua na rundo la Polisi, wakizagaa kila mahali. Nikajiuliza hivi hawa watu wote hapa wanalipwa na nani?Maana lazima uwalipe Posho, hata kama ni shilingi 500 kwa siku bado na yenyewe ni pesa. Kwanini pesa hizo zingetumika kuboresha nyumba zao? hata nyumba moja tu? au mafuta yanayotumika kuzungusha magari hayo kwa kipindi chote hicho, hizo running cost nani anazibeba? Kama suala ni kuzuia mikutano ya Chadema kwanini wasingekaa meza moja na kuyamailza? Polisi wanapata shida gani kuwaita mezani Chaedma wakaongea nao?
Nadhani na ninaamini resources zote zinazoteketea Dodoma sasa hivi zingetumika vyema na kwa usahihi basi Yule Jambazi wa Mwanza asingeweza kuwatoroka Polisi kijinga vile, huku Polisi wakikosa majibu, hizo resources zinazoteketezwa Dodoma zingetumika ku-invest kwa Traffic police basi ajali zingepungua na kuokoa maisha.
Kama zingetumika vyema kwa kulinda wananchi wote kwa usawa, huenda ndugu zetu kule Tanga wasingepoteza maisha yao kwa kuchinjwa, huenda kama zingetumika vizuri kwa wote badala ya kulinda kundi Fulani tu basi migogoro ya ARDHI kati ya Wakulima na Wafugaji ingepungua maana Polisi wangeweza kufika on-time.
Huenda Polisi wangekua na vifaa vizuri vya mawasiliano na hivyo kudhibiti uharamia kila mahali. Lakini ingewezekana tu kama hizo rasilimali chache zingetumika kwa usahihi