KULIPISHWA GHARAMA MARA MBILI MBILI KIVUKONI

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
1,259
1,052
Heri ya Mwaka Mpya wanajamvi wote.
Leo nimekuja na kero moja ya kivuko. Mtu ukiwa na gari let say mmetoka kifamilia mkifika kwenye kivuko mnaambiwa shukeni nyote... Hapo sasa utalipia gharama ya kuvusha gari na pia wale watu wote utaambiwa walipe nauli upya.
Hivi hii imekaaje wadau??
 
Mie nahis huwa unalipia gari na dereva, abiria wanajitegemea. Mfano kama hata abiria wangekuwa hawalipii basi watu tungeomba lift kwenye Prado au Noah ili kukwepa foleni ya kulipia 200. Happy new year
 
Suala hapa ni kwa nini abiria washushwe badala ya kuchajiwa nauli wangali ndani ya gari? Kama ni sababu za kiusalama sawa ila kama ni sababu za kimapato nadhani ni udhaifu wa kiutawala.
 
Happy New Year Mkuu
 
Suala hapa ni kwa nini abiria washushwe badala ya kuchajiwa nauli wangali ndani ya gari? Kama ni sababu za kiusalama sawa ila kama ni sababu za kimapato nadhani ni udhaifu wa kiutawala.
Kuna siku walinijibu wenyewe wanachaji chombo cha usafiri na mzigo wake na si abiria.. Kwa sababu nilkuwa na njaa nikasave nguvu ya kugombania gari
 
Heri ya Mwaka Mpya wanajamvi wote.
Leo nimekuja na kero moja ya kivuko. Mtu ukiwa na gari let say mmetoka kifamilia mkifika kwenye kivuko mnaambiwa shukeni nyote... Hapo sasa utalipia gharama ya kuvusha gari na pia wale watu wote utaambiwa walipe nauli upya.
Hivi hii imekaaje wadau??

Si kweli kuwa unalipa nauli mara mbili. Utaratibu ni kwamba dereva pekee anapaswa kuingia na gari ndani ya kivuko, na hii ni kwajili ya usalama tu, mara kadhaa magari yamekuwa yakitumbukia baharini ya kwasababu tofauti kwa uzembe wa dereva au kwauzembe wa dereva mwingine na hata kwa uzembe wa abiria. Na hata kama ukiweza pita na abiria wako ndani ya gari lazima watatakiwa kulipa nauli sawa na vile wanaopita kwa wasio na magari. Hivyo si kweli nauli hulipwa mara mbili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom