Wakuu kuna kitu huwa sikielewi vizuri naomba mnitoe ujinga.
Watumishi mbalimbali wa umma wanapokuwa na vikao vya kazi hujilipa mi-posho mikubwa mikubwa eti wanaita 'working sessions' tofauti na posho za kujikimu wanazolipwa za malazi na vyakula 'perdiem' wakiwa nje ya vituo vyao vya kazi. Wengine hulipwa hata mafuta au nauli za usafiri au kusafirishwa ili wafike kwenye maeneo ya matukio 'Vikao' husika. Lakini kama hiyo haitoshi, watumishi wengi (wanaoshiriki kwenye hivyo vikao) wanalipwa mishahara mwisho wa mwezi. Mfano:
1. Wabunge kazi yao ni kuwakilisha wananchi ndani ya Bunge huku wakilipwa mishahara kila mwezi, lakini wakiwa ndani ya Bunge na kupewa viburudisho vyote kama chai, maji nk bado wanalipwa tena posho za vikao!
2. Watendaji wa taasisi na wajumbe wa Mabodi, wakiwa kwenye vikao vya Bodi wanalipana posho 'working session'!
3. Mikutano mbalimbali ya kiutendaji kwa watumishi, watu wanalipana posho!
Wadau wenye uelewa wa haya mambo nifungueni.