Kulikuwa na tatizo gani wanyama kupelekwa Qatar?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
 
Tatizo ni kupeleka wanyama wetu Qatar... Wanyama hawatakiwi wasafirishwe nje ya nchi.. Full stop
 
Kawaulize maafisa wa Ikulu wa Jakaya Kikwete wakuambie ni kwanini sio tatizo kusafirisha wanyama maana wao ndio wahusika wakuu
 
Kama ulijua hauna jibu kulikuwa na haja gani hata ya kujaza nafasi?
 
wewe ni mjinga na natumaini hauna hata Elimu ya juu .bado ubajiita thinker

swissme

Mimi siyo huyo thinker unayemuongelea na wala sijawahi kujiita hivyo na ndiyo maana nauliza kulikuwa na tatizo gani kuuza wanyama pori? Sasa wewe thinker unaweza kunisaidia hapo kama ukipenda!
 
Unafikiri wanyama wote wakihamishwa mtalii gani toka uarabuni atakuja tena kwenye mbuga zetu?Na vizazi vijavyo watawaona wapi hao wanyama live!
 
Kuuza wanyama hai inakuwa si tatizo kama sheria iliwaruhusu,wao wamewabeba kinyemela pasipo mamlaka husika kuruhusu na mbaya zaidi wamebeba hadi Twiga ambao ni nembo ya Taifa, mnyama ambaye huruhusiwi kumuwinda, utapewa vibali vya kuwinda wanyama woote, lakini siyo Twiga.
Kingine hata hizo pesa zilizopatikana kutokana na mauzo hayo, hazijulikani ziliingia mfuko upi!.
Ngoja na wengine watajazia
 
Kama ulijua hauna jibu kulikuwa na haja gani hata ya kujaza nafasi?
Usitake kutufanya wapuuzi ,wewe hujaona mada iliyoletwa hapa kuhusiana na hilo la wanyama na kuhusika kwa ikulu ya Jk ? Kulikua na haja gani ya kuleta hii thread wakati ipo huku na imeshajadiliwa
 
Kuuza wanyama hai inakuwa si tatizo kama sheria iliwaruhusu,wao wamewabeba kinyemela pasipo mamlaka husika kuruhusu na mbaya zaidi wamebeba hadi Twiga ambao ni nembo ya Taifa, mnyama ambaye huruhusiwi kumuwinda, utapewa vibali vya kuwinda wanyama woote, lakini siyo Twiga.
Kingine hata hizo pesa zilizopatikana kutokana na mauzo hayo, hazijulikani ziliingia mfuko upi!.
Ngoja na wengine watajazia

Hilo ndilo nililotaka kuelewa kama fedha hazikulipwa hapo naweza kuelewa lkn kama fedha zililipwa sioni tatizo liko wapi
 
Usitake kutufanya wapuuzi ,wewe hujaona mada iliyoletwa hapa kuhusiana na hilo la wanyama na kuhusika kwa ikulu ya Jk ? Kulikua na haja gani ya kuleta hii thread wakati ipo huku na imeshajadiliwa

Kama ningeiona nisingekuwa na haja ya kutaka kufahamu ni kwa nini ni ishu kuuza wanyama pori!
 
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
Ninavyojuwa mie ni "SOKO HURIA" na Uhalali wa biashara huwa hainaga mipaka au ukomo!! Mteja analipa $$$$ na muuzaji anatoa Rasilimali yake !!
 
Athari .
Mapato watakuja kuangalia twiga huku while wapi Dubai so tutapoteza ..

Kupotea kwa hao wanyama kama wakichukua Mara kwa Mara mwishowe tutabaki na mapori tu...

Kikubwa hapo ni mapato na kupoteza wanyama wetu
 
Kwan sababu ya ww kujua kwamba kuna twiga alisafirishwa ni ipi!!?? mbali na kwamba ulisikia twiga amekamatwa akisafirishw? Kama walimkamata ina maana wahusika hawakuw na kibali wangekuwa nacho hata ucngeckia kwan ni wanyama wangap wako ughaibuni na hawajawah kuuliziwa!?
 
Athari .
Mapato watakuja kuangalia twiga huku while wapi Dubai so tutapoteza ..

Kupotea kwa hao wanyama kama wakichukua Mara kwa Mara mwishowe tutabaki na mapori tu...

Kikubwa hapo ni mapato na kupoteza wanyama wetu

Lakini hawa wanyama wanakwenda kuwekwa zoo kwa matumiozi binafsi na siyo kwenye mbuga, kwa maana mbuga huko Uarabuni hakuna na watalii wanaokuja TanZania wanakuja kwa sababu ya Serengeti na siyo wanyama peke yake kwa maana kama ni hivyo wasingekuja kabisa kwa maana kila nchi ina hawa wanyama karibia kila Mzungu au Mwarabu, ameshaona wanyama wote huko kwao zoo tangu wako wadogo Wazungu wanakwenda zoo, hivyo kinamcholeta ni ile Serengeti ambayo hawezi kuwa nayo kwao na Uhuru wa wanyama!

Kuhusu wanyama kupotea sikubaliani na wewe kwani wanyama wanazaana na kamwe hawawezi kuisha kwanza huwa wanazidi mpaka wanaharibu mazao ndiyo maana nashindwa kuelewa tatizo liko wapi sisi kuwauza na kuingiza mapato kama exports nyingine tu?
 
Lakini hawa wanyama wanakwenda kuwekwa zoo na siyo kwenye mbuga na watalii wanaokuja TanZania wanakuja kwa sababu ya Serengeti na siyo wanyama peke yake kwa maana kama ni hivyo wasingekuja kabisa kwa maana kila nchi ina hawa wanyama karibia kila Mzungu au mwarabu, ameshaona wanyama wote huko kwao zoo, hivyo kinamcholeta ni ile Serengeti ambayo hawezi kuwa nayo kwao na Uhuru wa wanyama!

Kuhusu wanyama kupotea sikubaliani na wewe kwani wanyama wanazaana na kamwe hawawezi kuisha kwanza huwa wanazidi mpaka wanaharibu mazao ndiyo maana nashindwa kuelewa tatizo liko wapi sisi kuwauza na kuingiza mapato kama exports nyingine tu?
We jamaa ni mbishi sana. Unajua hao waarabu na wazungu hizo zoo ni artificial ambapo hutaona uhalisia wa yale mazingira ya mnyama anapostahili kuwepo.
Halafu hao wanyama, unaosema kamwe hawawezi kuisha, hebu fikiria utamkacho kabla hujaandika. Uliza sensa ya Tembo miaka mitano iliyopita ufananishe na leo. Hawa wanyama wewe kuwaona ni juhudi zimefanyika za kuzuia uwindaji haramu. Vinginevyo ungekuwa ukiona kwa picha,kama yule mjusi mkubwa.
 
Lakini hawa wanyama wanakwenda kuwekwa zoo kwa matumiozi binafsi na siyo kwenye mbuga, kwa maana mbuga huko Uarabuni hakuna na watalii wanaokuja TanZania wanakuja kwa sababu ya Serengeti na siyo wanyama peke yake kwa maana kama ni hivyo wasingekuja kabisa kwa maana kila nchi ina hawa wanyama karibia kila Mzungu au Mwarabu, ameshaona wanyama wote huko kwao zoo tangu wako wadogo Wazungu wanakwenda zoo, hivyo kinamcholeta ni ile Serengeti ambayo hawezi kuwa nayo kwao na Uhuru wa wanyama!

Kuhusu wanyama kupotea sikubaliani na wewe kwani wanyama wanazaana na kamwe hawawezi kuisha kwanza huwa wanazidi mpaka wanaharibu mazao ndiyo maana nashindwa kuelewa tatizo liko wapi sisi kuwauza na kuingiza mapato kama exports nyingine tu?
Sasa kama naweza kumwona twigs zoo kwa gharama ndogo na kuna kutafuta mbugani gharama kubwa uoni kama zoo itakuwa na watu wengi zaidi kuliko mbugani?
 
Back
Top Bottom