kulikua na ulazima wa kumteua mwandosya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kulikua na ulazima wa kumteua mwandosya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, May 8, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hivi kulikua na sababu yeyote ya msingi jk kumteua mzee mwandosya kuwa waziri wakati ni wazi kabisa inaonyesha hali yake kiafya bado haijatengemaa sawasawa??

  Je watanzania tutegemee mchango gani kutoka kwa mzee wetu huyu mtaalam aliyebobea kwenye masuala mazima ya mazingira ambae dunia imekua ikimtumia kwenye masuala hayo kipindi alipokua na afya nzuri?  Pichani chini:Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Waziri asie na Wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kunduchi jijini Dar es salaam kumjulia hali May 7, 2012.

  [​IMG]

   
 2. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  JK awahitaji kina MWA la sivyo wataenda Chadema kama wimbi lilivyo sasa.
  mtandao wa Mwa ni kubwa mno kulipoteza.
   
 3. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kuugua sio kwamba hatapona. Huyu ndo nguzo ya ccm ktk mkoa wa mbeya. Kuto mjumuisha katika baraza la mawaziri lingekuwa pigo kwa ccm katika mikoa ya ukanda huo. Hajapewa wizara specific kwani bado hajawa fit ki afya ila lazima jina lake liwemo kwenye baraza kwa manufaa ya ccm.
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  hii thread haina umuhimu kwa sasa
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka kubagua wagonjwa? Mbona anaweza kuperform kabisa huyo.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  linganisha na kazi alizolifanyia taifa hata kabla ya kupata uwaziri kisha utajua kwamba Jk alikuwa sahihi kumpa wizara hiyo.

  Usifikiri Rais anatoa fursa hiyo kwa kila kiongozi ni fursa idimu kupewa na nadra sana kukutana nayo ni viongozi wangapi wamepishana na fursa hii.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwandosya amejitahidi sana kupishana na orodha ya mafisadi ya Chadema ni dalili njema kwa kiongozi kushinda tuhuma za wapinzani.
   
 8. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Get well soon Hon Mark
   
 9. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuuuuuuu, handsome boy masikini kwishnei
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Halafu tunasema Tanzania ni nchi masikini ambayo haina umeme wa uhakika, haiwezi kuwalipa madaktari vizuri na haiwezi kuwalipa walimu lakini inaweza kumpa mtu uwaziri bila yule mtu kufanya kazi yeyote. Watanzania ni wa pole sana!!!
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu, JK yuko makini sana ndio maana hadi kina VIck Kamata, Betty Mkwasa wanapata nyazifa...
   
 12. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli mwandosya amechoka, hiyo "sumu" waliyompa ni kiboko...
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwisha habari yake, JK ameshaandaa ile kalamu yake ya kwenda kusaini vili vitabu kama kwa kanumba....
   
 14. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lakini tunaomlipa ni sisi walipa kodi
   
 15. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona kaenda kujuliwa hali na waziri mkuu nyumbani kwake na si ofisini kwake?
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ni bora hata Rais kumtetea na kumueka mwandosya kuliko alivokua anawatetea akina ngeleja na majambazi wenzie...
   
 17. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe acha ushabiki,jk hana cha kupoteza mleta mada kama humjamuelewa lengo lake ni kuonyesha matumizi mabaya ya serikali,mwandosya kwa kuteuliwa tu ataliowa mshahara na malupu lupu kama mawaziri wengine,sasa kwanini tumlipe mgonjwa mapesa hayo?kwanini tusimlipie matibabu tu then yeye abaki nyumbani ashughulike na afya yake kwanza mpaka itakapoengemaa?kulikua na haraka gani ya kumchagua kabisa?
   
 18. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo n i afya yake kaka
   
 19. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jk hana huruma na fedha za walipa kodi,na ndiyo sababu anazifuja atakavyo.
   
 20. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Elimu ni nzuri sana, ukikosa elimu unakuwa kama mtumwa wa milele. Hivi katika mawazo yako unafikiri Rais anateua watumishi au Mawaziri ili kukuridhisha wewe na familia yako? Tambua kuwa kabla ya Ujeuzi Rais anashauriana na jopo la watu wenye heshima sana na Elimu ya kutosha na kupata ushauri wa kina.


  Rais hawezi kukusikiliza wewe unayefikiria wajomba zako na binamu zako ndiyo wateuliwe. Nchi huendeshwa kwa umakini sana na ndivyo Rais anafanya, sio kusikiliza mawazo potofu kama yako.

  Prof. Mwandosya ni mtu muhimu sana katika nchi hii, duniani na Chama cha Mapinduzi, hivyo lazima Serikali iendelee kumtumia kwa faida ya Watanzania wote na siyo kwa faida ya Wajomba zako.

  Tatizo lako hujui hata mahusiano mema kazini, ukimwajiri Housegirl nyumbani kwako, alafu ghafya huyo binti akaanza kuumwa, usifikilie kumfukuza kazi kwa vile tu hawezi kukupikia kande kwa wakati huo na huku ukiwaza gharama za kumtibu. Kwanza fikiria kumtibu ili arudi katika hali yake ya kawaida alafu endelea kumtumia.


  Ingekuwa nchi hii inaendeshwa na wajinga kama nyinyi pangechimbika kwani immediately ukisikia Waziri, Katibu, Mhasibu, Tarishi, Mfagizi wa choo katika Ofisi za Serikali anaumwa wewe ungekuwa ni kuulizia faili lake ili kumsimamisha kazi mpaka atakapopona au akichelewa kupona unamfukuza kazi.

  Big up JK, Prof. Mwandosya nchi hii bado inamwitaji usisikilize hawa walevi.
   
Loading...