Kulikoni vyeo vya RC na DC - Vinahitajika???

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
Habari za mihangaiko wanaJF

Katika mchakato wa kuandaa katiba mpya kuna haja ya kuangalia mambo mengi lakini tukifanya vizuri kwenye mambo ya msingi, yaweza kutoa mafanikio yaliyokusudiwa ambayo ni kuleta maendeleo.

Kuna wananchi wengi sasa wanahoji uwepo wa mfumo wa wakuu wa mikoa na wilaya na jinsi hizo nafasi zinavyopatikana. Wengi wanadai hazina vigezo kuzipata bali inategemea uswahiba kati ya mchaguaji na mchaguliwa na endapo nchi ina raisi asiye makini au mwenye malengo anayoyajua yeye (uko mbeleni) huenda tukajikuta tunavuna machungu.

Sasa mimi naomba wana jf tuliangalie suala hili kwa mtazamo wa kiuchumi zaidi badala ya kisiasa zaidi.
Je kuna mwanajamvi anayeweza kutupa estimates (makadirio) ya gharama za kuendesha ofisi hizi kwa na ni jinsi gani tukiziokoa kwa kubadilisha mfumo huu tuzielekeze wapi katika mustakabali mzima wa uendeshaji wan chi.

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom