Wadau,
Zikiwa na historia ya zaidi ya miaka 17 tangu zianzishwe Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (KTMA) ndizo zinaonekana kama Tuzo za "Taifa".Ni Tuzo ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu kila mwaka hususani kwa wapenzi na wadau wa Muziki pamoja na wanahabari.
Sio jambo la kushangaza kukuta watanzania wakikesha kufuatilia kwenye runinga zao takribani vipengele 22 vya Tuzo hizo kila zinapofanyika na kuonyeshwa mubashara.
Takribani miaka miwili sasa Tuzo hizo hazijafanyika tangu zifanyike kwa Mara ya mwisho msimu wa 2014/2015.
Sio wandaaji,BASATA ,wala wadhamini TBL kupitia bia ya Kilimanjaro ambao wametoa taarifa yoyote rasmi.
Ni dhahiri Tuzo hizo zilikuwa na changamoto nyingi pamoja na malalamiko mengi karibia kila mwaka.
Vipengele ambavyo vimekuwa "hot" kwamfano msanii bora wa mwaka,wimbo bora wa hiphop,video bora ya mwaka,mtayarishaji bora, n.k ndivyo kwa hakika vimeleta malalamiko mengi.
Nakumbuka mwaka 2009 Hamisi Mwinjuma "MWANA FA" aliziponda Tuzo hizo kwa kukosa uhalisia na hiyo ni baada ya "hit" song yake "Bado nipo nipo" kukosa Tuzo yoyote
Pia wasanii Khalidi Mohammed"TID" pamoja na Abdul Sykes "Dully Sykes" wao walishajitoa kwenye mchakato wowote unaohusisha Tuzo hizo.
Miaka ya karibuni waandaaji walianzisha utaratibu wa kufanya semina(pre-seminars) kwa washiriki "nominees"pamoja na wanahabari kabla ya kilele cha Tuzo zenyewe.
Hill limesaidia sana kupunguza malalamiko kutoka kwa washiriki na hivyo kuongeza ubora wa Tuzo hizo.
Swali kuu ambalo wadau wa Muziki Tanzania wanajiuliza Je Tuzo za KTMA zimekufa?au tusubiri msimu mpya.
Time will tell..