Kulikoni mamlaka ya vitambulisho vya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni mamlaka ya vitambulisho vya taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Las Mas Bobos, Jun 24, 2012.

 1. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jana nimeshuhudia viashiria kadhaa vya kuanza kufeli kwa zoezi la uandikishaji wa wananchi mitaani katika zoezi zima la utoaji wa vitambulisho vya Taifa.

  Nilipita katika ofisi za kata za MAKUBURI, KIMARA na MANZESE na kukuta mikusanyiko ya watu wa jinsia tofauti ambayo kwa kata ya Manzese na Makuburi ilikuwa kulikuwa na mizozo ya hapa na pale.

  Katika kuuliza nini kimejiri, niliambiwa wale ni watu watakaoendesha zoezi la uandikishaji wa wananchi na mizozo na mikusanyiko ile ni katika kumsubiri mhasibu ambaye anawajibika kugawa posho ya kujikimu ya mafunzo ya kazi kwa siku mbili.

  Kilichonishangaza ni kwamba (kwa maelezo ya mmoja wao) walikuwa hapo wakisubiri ujio wa huyo mhasibu tangu saa 5 asubuhi mpk saa 11 ile niliyowakuta. Mbaya zaidi, hata saa 1 usiku nilipopita tena Makuburi nikirejea nyumbani, bado watu wale (wengi vijana) walikuwa bado mahali pale chini ya miti mhasibu hajaja.

  Nilichoweza kukibaini ni kuwa NIDA, wanatumia Mhasibu mmoja kugawa fedha katika kata 32 za Wilaya ya Kinondoni. Mhasibu huyu anafanya kazi hii peke yake kwa hiyo ametumia siku 2 kugawaa posho lkn bado hakuweza kuwafikia watu wa Makuburi kwani hadi asubuhi saa 5 leo bado hawajalipwa na baadhi ya kauli pale kwenye zogo zilitamka kuwa kama mwenendo ndio huu J3 hamna kazi.

  Kinachonishangaza ni utaratibu wa NIDA. Hivi ni lazima malipo yote yafanywe na mhasibu? Wale wasimamizi wa KATA kwa nini wasipewe hizi posho za watu wao wakawasainisha baada ya kumaliza training mpk watu wawekwe zogo tangu asubuhi mpaka saa 1.30 usiku na bado asifike?

  Haya ndio yanayotuharibiaga kazi mitaani. Huu sio utaratibu hata kidogo. Endapo kauli zile zikitekelezwa, hili zoezi litaingia dosari. Wahasibu wasitegemewe kuwa ma-cashier jamani.

  Pia nilisikia kuwa kuna muda fulani zoezi hilo la ulipaji lilisimama kwa kuwa gari la fedha lilimpeleka Mkurugenzi airport! Sikuwa nikifahamu awali kuwa NIDA wana gari moja tu. Na kama ni hivyo kwa nini Mkurugenzi asikodi teksi badala ya kusimamisha zoezi muhimu kama hilo.

  Kama kuna mwenye kulifahamu hili na updates kama wameshalipwa tafadhali aweke hapa.
   
Loading...